UVCCM Morogoro wampinga Malecela

UVCCM Morogoro wampinga Malecela

hii nguvu inayotumika kumsafisha Lowasa ni kwa maslahi ya nani?
Ni kwa maslahi ya kutunza demokrasia ndani ya ccm, kama alivyofafanua Mh Nape alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huko Mbeya. Aliongeza kwa kusema kwamba hakuna chama chenye demokrasia pana kama ccm hapa nchini.
 
wanatakiwa wanasiasa jasiri kama makonda kusema ukweli na kutooogopa

tunajua chaguo lenu ni asha migiro na january yusufu..tunaombea apite lowassa sababu kazi itakuwa nyepesi kuwaondoa wakoloni weusi.
 
ccm kuna udikteta,hakuna demokrasia..mtendeeni haki lowassa..au kwa vile ananadi sera ya chadema ya elimu bure?
 
Toa tamko M/Kiti wa tawi la vyuo. Kwani hujui kusema; Nimetoa tamko?? Ka hujui sema tukusemeee. Kyama Kimekufa Kyenyewe hikyoooo. Wow! CCM is no moreeeeeee
 
UVCCM MORO YAMTOLEA UVIVU MALECELA
Kutokana na malumbano yanayoendelea kati ya Wanachama wa Chama cha Mapinduzi hususani Jumuiya ya Umoja wa vijana (UVCCM) kutokana na matamko yanayoendelea kutolewa.

Ni jambo la kushangaza sana kumuona Mzee Mashuhuri na nguli wa Chama cha Mapinduzi Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM Mstaafu kumuunga mkono kijana aliyekiuka katiba ya Chama cha Mapinduzi na kanuni za Umoja wa Vijana Paul Makonda kutokana na kauli yake ya kuudanganya Umma kuwa tamko alilolitoa la kumkashifu Waziri Mkuu Mstaafu na Mjumbe wa NEC ndugu Edward Lowassa kuwa ni la Umoja wa Vijana. Vifungu vilivyo kiukwa kikanuni na kikatiba ni vifuatavyo:-


Makonda amekiuka katiba ya CCM Ibara ya 14(4) Mwanachama yeyote atakuwa na haki zifuatazo "Haki ya kujitetea au kutoa maelezo mbele ya kikao cha CCM kinachohusika katika mashtaka yoyote yaliyotolewa juu yake. Pamoja na haki ya kukata ya kwenda katika kikao cha juu zaidi cha CCM kama kipo endapo hakuridhika na hukumu iliyotolewa"
Kwa kuwa kifungu hiki kinatoa fulsa kwa Mwanachama kujitetea juu ya tuhuma zinazomkabili.


Je Chama cha Mapinduzi kiliwahi kumuita Mh. Edward Lowassa na wengineo wote wenye kashfa za rushwa na kutangaza nia ya Urais kumhoji na kumsikiliza na Chama kufanya maamuzi? Lakini kutoa matamko kupitia kofia ya Chama ni makosa makubwa yaliyofanywa na Makonda na anapaswa awajibishwe. Tunamshangaa pia Mzee Malecela kuunga mkono mtu aliyekiuka haki za mwanachama na utaratibu wa Chama. Huu ni ukweli kuwa tegemeo la Wazee wa CCM kusimamia haki na wajibu wa Chama umetoweka.


Lakini pia Mzee Malecela anamtuhumu Edward Lowassa kuchangia harambee, kugawa tisheti na kutoa misaada katika nyumba za Ibada Kanisani na Misikitini. Mbona wapo wanachama wengi wanaofanya harambee kama hizo mfano ni Benard Membe, Sumaye, Samwel Sitta na January Makamba wao pia wanatenda matendo ayatendayo Lowassa mbona hawajatolewa matamko. Wametengeneza hadi na kalenda kama sehemu ya kujinadi mwaka 2015. Kwa nini hawakukemewa wote kwa pamoja?.Lakini pia Paul Makonda amewakashifu viongozi wetu wa dini kwa kuwafanisha na wasaka pesa kwahili tunamtaka awaombe viongozi hawa wote msamaha haraka,Vilevile ieleweka viongozi wa dini ni nguzo ya vijana wa taifa hili na uvccm inawathamini na pia tunatoa rai kwa mtanzania yoyote mwenye imani na roho ya upendo na wa dii yoyote kufanya kazi na viongozi wa dini na kujenga nchi pamoja nao,Je Mzee Malecela anaunga mkono Paulo Makonda kuwakashifu viongozi hawa wa dini?.Tulitegemea sana Mzee kama Malecela angekemea matendo haya kwa wanachama wote lakini ameonesha chuki binafsi kwa ndugu Edward Lowassa. Lakini hatupaswi kumshangaa maana hata Hayati Mwl Nyerere aliposema kama Mzee Malecela atagombea Urais narudisha kadi ya CCM,

Hatukumuelewa Mwl Nyerere alimaanisha nini lakini kwa sasa tumepata picha kamili ni jinsi mzee huyu asivyo na busara na anaweza kukizamisha chama kwa chuki zake binafsi na maneno yake ya kupotosha watanzania.

Mzee Malecela anapaswa kuomba radhi kwa Umoja wa Vijana wa CCM kwa kumuunga mkono Paul Makonda ambaye si msemaji wa UVCCM kwa mujibu wa Kanuni za Umoja wa Vijana. Wasemaji wakuu wa Jumuiya ni Mwenyekiti na Katibu kwa ridhaa ya vikao na maadhimio yaliyofanywa katika vikao wao ndo wenye mamlaka hayo. Lakini pia Makamu mwenyekiti Mboni Mwita amekana kutolitambua tamko la Umoja wa Vijana bali ni la kwake binafsi tunashangaa Mzee Malecela kwa nini anamuunga mkono Paul Makonda.


Tunatoa wito kwa Chama cha Mapinduzi kupiga marufuku matamko yote yanayoendelea nchini na kuwachukulia hatua wale wote wanaotangaza nia ya kugombea Urais kabla ya wakati na tunamuomba Mh. Mwenyekiti wa Chama ndugu Jakaya Mrisho Kikwete kukemea hali hii kwa nguvu zake zote ili kukisalimisha Chama na kuwepo kwa utii wa Kikatiba. Kuachwa kwa hali kama hii itakuza migogoro na makundi ndani ya Chama.
Imetolewa na Komredi Heri Hoza ni Kada wa muda mrefu wa UVCCM na Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya baraza la Umoja wa Vijana wa ccm Mkoa wa Morogoro. Pia ni Mwenyekiti wa CCM wa tawi jipya la Chuo Kikuu huria (Morogoro branch).

This is funny,

Unapinga watu kutoa matamko huku wewe ukitumia njia hiyo hiyo kutoa matamko?


Kama Makonda amekiuka kanuni,kwani wewe usipeleke kwenye vikao vya chama?Wewe umefuata katiba ipi iliyokuruhusu kumshutumu Makonda na Malecela hadharani?

Je ukiambiwa na wewe umuombe msamaha Mzee Malecela utaona umeonewa?


Yaani kada wa muda Mrefu wa UVCCM ndiyo anaweza kweli kuja hadharani kwa hoja dhaifu na za aibu namna hii?Hii ndiyo hazina ya CCM? Kweli hii chama hakiwezi kuunda serikali bila mawaziri mizigo na in the near future tutarajie the worst.

Unasema makonda kadanganya,je ukiulizwa ni lini Lowassa alistaafu U-waziri mkuu utatujibu kwa weledi na kutuondolea mashaka juu ya kauli na dhamira yako?

-Hivi,hili Tamko ni lako Binafsi kama mwenyekiti wa hilo tawi au la taasisi unayowakilisha?
 
This is funny,

Unapinga watu kutoa matamko huku wewe ukitumia njia hiyo hiyo kutoa matamko?


Kama Makonda amekiuka kanuni,kwani wewe usipeleke kwenye vikao vya chama?Wewe umefuata katiba ipi iliyokuruhusu kumshutumu Makonda na Malecela hadharani?

Je ukiambiwa na wewe umuombe msamaha Mzee Malecela utaona umeonewa?


Yaani kada wa muda Mrefu wa UVCCM ndiyo anaweza kweli kuja hadharani kwa hoja dhaifu na za aibu namna hii?Hii ndiyo hazina ya CCM? Kweli hii chama hakiwezi kuunda serikali bila mawaziri mizigo na in the near future tutarajie the worst.

Unasema makonda kadanganya,je ukiulizwa ni lini Lowassa alistaafu U-waziri mkuu utatujibu kwa weledi na kutuondolea mashaka juu ya kauli na dhamira yako?

-Hivi,hili Tamko ni lako Binafsi kama mwenyekiti wa hilo tawi au la taasisi unayowakilisha?

mbona wewe ulipotoa kashfa kwa kiongozi wako wa chama enzi hizo akiwa naibu katibu mkuu hukuchukuliwa hatua? halafu kwa kosa hilo hilo la zitto kukashifu uongozi yamemkuta.......
Chadema itakufa kabla ya CCM
 
Komredi Heri Hoza umesahau pia kuwa Nyerere alimuuliza Lowasa utajiri huo kautoa wapi? Unakumbuka ya Malecela tu! Unapendekeza CCM wazuie matamko na wewe unatoa tamko! Unasema Mzee Malecela (ambaye pengine analingana na babu yako) kuwa Hana busara, je wewe busara yako ni ipi kusema hayo?

Vijana jitambueni, mnaelekea kusiko na mnapeleka taaifa kusiko.
 
Tatizo Mzee Malecela anaamini watanzania wa sasa wanamsikiliza. Angefanya utafiti kidogo angeshangaa sio watu watu wengi hawamsikilizi lakini hawajui yeye ni nani?!
 
Malumbano yanayoendelea ni katika kukua kwa demokrasia ndani ya chama. Siasa si uadui kama ilivyo ndani ya CHADEMA

siku hizi imekuwa hivyo tena?? Ccm kiboko,mnajuwa sana kujipooza na kujiliwaza kwakweli,, lakin kifo chenu tayar kimesha fika, nyambafu.
 
Back
Top Bottom