VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Kwanza,nyinyi mnasemwa kama vijana mnaotumika na makundi ya Urais 2015. Hivyo,nyinyi UVCCM,si wamoja. BAVICHA hawana makundi na wamebaki wamoja.
Tena,BAVICHA inathubutu hata kufanya mikutano ya hadhara kupitia viongozi wao. Wanahutubu na kusikilizwa. UVCCM mko nyuma. Mnaogopa au kukosa kitu gani. Semeni msaidiwe. Shirikini mikutano na midahalo.
Mabaraza ya Vijana vyamani ni chemchem ya kuzalisha viongozi waliopikwa wakapikika. Si mahali pa kukaa ofisini bila tija. Kukaa bila ya kufanya kazi inayostahili.
Binafsi,sijaiona tena UVCCM ya Nchimbi. Ilikuwa moto. Hii imepoa na inazidiwa ujanja na BAVICHA. Thubutuni kuhutubia na kutangaza sera za chama chetu kwa vijana. Isifikie wasemaji wa vijana nchini wawe BAVICHA.
Punguzeni au muache kabisa woga na utegemezi. BAVICHA wanawazidi ujanja. Msikubali.
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam