UVCCM mmekosa adabu kwa Mzee Moyo

UVCCM mmekosa adabu kwa Mzee Moyo

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,458
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imesema imechoshwa na vitendo vya muasisi wa chama hicho, Hassan Nassor Moyo, kwa madai ya kukisaliti na kukidhoofisha chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, aliwataka viongozi wakuu wa CCM kuchukua hatua za kinidhamu na kumnyang'anya kadi ya uanachama muasisi huyo. Moyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ambayo ilihusika wakati wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na ni mtetezi wa muundo wa serikali tatu.

Shaka alisema kwa muda mrefu Mzee Moyo amekuwa akikihujumu CCM bila ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu, na kwamba hali hiyo linakidhoofisha chama hicho na kukivunjia hadhi mbele ya wananchi, hivyo wakati umefika kwa muasisi huyo kufukuzwa CCM. ‘CCM kina mtaji wa wanachama, viongozi na waasisi wengi, si maskini, heri wabaki wachache kuliko kuendelea kubaki na wanachama wasaliti na wakorofi," lisema Shaka.

Shaka alisema Moyo amekuwa akitumia mwavuli wa uanachama wa CCM kukivuruga na kukisaliti chama hicho kupitia Kamati ya Maridhiano ambayo alisema haikuundwa kwa mujibu wa sheria wala Katiba ya Zanzibar na kwamba Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, alishasema hadharani kwamba kamati hiyo haitambui.

"Hii ni kamati ya upekepeke inayomzunguka na kumyumbisha Rais Shein, haikuundwa kisheria, haina hadidu za rejea, haifahamiki kazi zake, kwanini ipande jukwaa la CUF na kuliogopa la CCM?" alihoji Shaka. Mzee Moyo alipoulizwa, alisema hashughulishwi na maneno yao na kuwa ni mwanachama wa CCM, ana haki ya kutoa maoni na anaona Serikali tatu ndizo zinazofaa.
 
Ngoja nikwambie...UVCCM imerundika Watoto wa Viongozi wa ngazi za juu wa chama cha Mapanya.

Imethibitika kuwa watoto wote wa viongizi wa CCM hawana malezi mazuri.

Inaaminika kuwa malezi ya hovyo wanayarithi kwa Baba/mama zao mfano Juma Athuman Kapuya mtoto wake. Mtoto wa Mwenyekiti ndio msambaza 'unga' kwa 'mateja' wote hapa Dar.

Hawa watoto walimtukana Lowassa pale Kibaha tena kwenye hicho kikao Ridhiwani Jakaya Mrisho Kikwete alikuwepo.

Nape(Moses Nnauye?) naye alitukana wazee eti wanasubiri kufa.

Martine Shighela naye akawa anafanya kazi ya kutafuna tu watoto wa watu kwa gharama za Chama. Alikuwa anawapeleka Zanzibar kuwatafuna. Huko Zanzibar kuna siku niliwaona na Juliana Shonza, sijui walikuwa na program gani...

Kwaiyo kinachowasumbua Vitotobvya UVCCM ni malezi wanayoyapata kutoka kwa Baba zao. Unategemea toto la John Komba litaacha kuwa litukanaji?
 
Last edited by a moderator:
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imesema imechoshwa na vitendo vya muasisi wa chama hicho, Hassan Nassor Moyo, kwa madai ya kukisaliti na kukidhoofisha chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar, Shaka Hamdu Shaka, aliwataka viongozi wakuu wa CCM kuchukua hatua za kinidhamu na kumnyang’anya kadi ya uanachama muasisi huyo. Moyo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maridhiano ambayo ilihusika wakati wa kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) na ni mtetezi wa muundo wa serikali tatu.

Shaka alisema kwa muda mrefu Mzee Moyo amekuwa akikihujumu CCM bila ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu, na kwamba hali hiyo linakidhoofisha chama hicho na kukivunjia hadhi mbele ya wananchi, hivyo wakati umefika kwa muasisi huyo kufukuzwa CCM. ‘CCM kina mtaji wa wanachama, viongozi na waasisi wengi, si maskini, heri wabaki wachache kuliko kuendelea kubaki na wanachama wasaliti na wakorofi,” lisema Shaka. Shaka alisema Moyo amekuwa akitumia mwavuli wa uanachama wa CCM kukivuruga na kukisaliti chama hicho kupitia Kamati ya Maridhiano ambayo alisema haikuundwa kwa mujibu wa sheria wala Katiba ya Zanzibar na kwamba Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, alishasema hadharani kwamba kamati hiyo haitambui.

“Hii ni kamati ya upekepeke inayomzunguka na kumyumbisha Rais Shein, haikuundwa kisheria, haina hadidu za rejea, haifahamiki kazi zake, kwanini ipande jukwaa la CUF na kuliogopa la CCM?” alihoji Shaka. Mzee Moyo alipoulizwa, alisema hashughulishwi na maneno yao na kuwa ni mwanachama wa CCM, ana haki ya kutoa maoni na anaona Serikali tatu ndizo zinazofaa.

Wangekua na staha wangeanza kumuadhibu Captain Komba na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo waliomtukana Warioba na Dr.Salim mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM
 
uvccm ni janga kwa vijana wastaarabu,wenye malezi mema na wanaojitambua.kwa pamoja tuukatae huu umoja wa wehu
 
Wangekua na staha wangeanza kumuadhibu Captain Komba na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo waliomtukana Warioba na Dr.Salim mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM

Baada ya Komba na Bulembo kuporomosha matusi kwa Warioba, CCM waliandaa party ya kuwapongeza. Uvccm waliitwa kwenye party kupata mafunzo ya matusi kwa wengine
 
What is politics. What it takes to be a follower of a party and duties thereon. I always see posts tending to ruin opponents reputation and credibility and always paint good image for own party. Pros and cons are not an issue. To date ask me wht is the prevailing economic policy for any party in Tz I won't tell. Use same effort to spread ur economic social and cultural ideology as well. This guarantee ur rising. Character assassination never have predictable outcome.

You might be seen as hater or with jealous.

I confess to love strong opposition for our free from corruption Tz
 
CCM imekuwa GENGE la Wahuni tu hata hawaheshimiki tena
 
UVCCM ni genge la vijana wanaowatumikia wakubwa kwa maslahi ya wakubwa na familia zao! Kijana wa mtanzania masikini hawezi kupatikana ndani ya umoja huu hata kidogo! Viongozi wa umoja huu hupata maelekezo toka baadhi ya vigogo wasioitakia mema taifa letu!
 
Tatizo la Ccm hawataki kuambiwa ukweli halisi,Mtu Kama Mzee Moyo,Warioba na kila atakaye waambia ukweli lazima wamuone adui,na bahati mbaya kwa MiCcm hao Wazee wamekataa usaliti kwa Watanzania angalia ukoo wa Panya unavyoweweseka.Tuungane Watanzania wote kuukataa ukoo huu ulio laaniwa nawa asisi wa Chama cha Zamani
 
Nimesikitishwa sana na kitendo cha UVCCM wa Zanzibar kutishia kumnyang'anya na kumfuta uanachama wa CCM kada wake mkongwe mzee Nassoro Moyo eti kwa sababu tu anatetea na kusimamia wananchi wanyonge!Vitoto hivi, tena vinavyonuka mkojo na maziwa, vinapata wapi ujasiri wa kumdhalilisha mzee wetu. Mnatishia kumfukuza mzee wa watu kutoka CCM kana kwamba akitoka kwenye chama atakufa? Mnadhani ni ndani ya CCM tu ndipo kwenye uhai? Msijaribu kufananisha CCM na wanachama kama maji na samaki. Samaki ukimtoa ndani ya maji atakufa. Ingekuwa CCM ni maji na wanachama ni samaki, hilo tishio la kumtoa ndani ya chama lingekuwa na mashiko. Ni wanachama wangapi wamejitoa CCM na bado wanaendelea kuwatetea wananchi wakiwa nje ya chama hicho? Kwani akina Maalim Seif walitoka wapi? Acheni kuwa na akili mgando.

Tukumbuke kwamba huyu mzee ni mwanamapinduzi aliyepigania uhuru wa Zanzibar hadi akamung'oa sultani. Moyo amepigania uhuru wa Zanzibar tangu zamani sana, hata kabla wazazi wa hayo makinda (ya kunguru) yanayopanua midomo kumdhihaki mzee wetu, hawajaliona jua. Sasa iweje watoto wadogo hawa wamdhihaki huyu mwanamapinduzi huku viongozi wa juu wa CCM wamekaa kimya? Au ndio tuseme kwamba ‘ukiona kifaranga juu ya kichuguu, mama yake yupo chini ya kichuguu hicho'?

Ni lini hasa wanaCCM wataanza kuthamini uhuru wa mawazo miongoni mwa makada wake? Tumekuwa tukisikia makada wengi wa CCM wakienda kinyume na mawazo ya kikandamizaji ya chama chao lakini hatukuwahi kusikia wakitishiwa kunyang'anywa kadi au kufutwa uanachama. Mifano halisi ni Mohamed Raza na mzee Sabodo. Raza amekuwa akienda kinyume na ukandamizaji wa CCM mara nyingi sana. Lakini kwa kuwa anazo fedha za kukifadhili chama, hatukuwahi kusikia akitishiwa kufutiwa uanachama. Aidha, mzee Sabodo, kada maarufu wa CCM, ameenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kukifadhili Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na huyu mzee kwa kuwa huwafadhili CCM pia hatukuwahi kusikia vitisho vyovyote dhidi yake.

Hata mtu uende kinyume na maagizo ya CCM, ilmradi tu unawafadhili fedha, hawana taabu nawe. Shida iliyopo ni kama mwanacham ataenda kinyume na mawazo yao halafu ukawa hana ufadhili wowote kwenye chama. Hata mfadhili angekuwa fisadi, mchafu au mnyonyaji, hawezi kufukuzwa uanachama. Kwa maana hiyo CCM ni chama kisichokuwa na ubaguzi wa aina ya wanachama-ni kama dodoki-huzoa kila aina ya uchafu ilmradi tu huo uchafu uwe na manufaa kwa chama. Kamwe tusitarajie kwamba mafisadi wataisha ndani ya CCM. Hilo haliwezekani hata kidogo.

TANGANYIKA KWANZA
:yield:
 
Mkuu ulevi wa madaraka ni mbaya kuliko ulevi wa mvinyo
Hivi vitoto vingi vimelewa madaraka tena ya kifalme
Vingine vishaona kama nchi hii ni yao peke yao na baba zao
Matokeo yake ndio kukosa adabu mbele ya mtu kama mzee Moyo
Dawa yao ipo na inachemka ipo siku watahama hii nchi tena sio siku nyingi
Ukawa kazini
 
Nimesikitishwa sana na kitendo cha UVCCM wa Zanzibar kutishia kumnyang’anya na kumfuta uanachama wa CCM kada wake mkongwe mzee Nassoro Moyo eti kwa sababu tu anatetea na kusimamia wananchi wanyonge!Vitoto hivi, tena vinavyonuka mkojo na maziwa, vinapata wapi ujasiri wa kumdhalilisha mzee wetu. Mnatishia kumfukuza mzee wa watu kutoka CCM kana kwamba akitoka kwenye chama atakufa? Mnadhani ni ndani ya CCM tu ndipo kwenye uhai? Msijaribu kufananisha CCM na wanachama kama maji na samaki. Samaki ukimtoa ndani ya maji atakufa. Ingekuwa CCM ni maji na wanachama ni samaki, hilo tishio la kumtoa ndani ya chama lingekuwa na mashiko. Ni wanachama wangapi wamejitoa CCM na bado wanaendelea kuwatetea wananchi wakiwa nje ya chama hicho? Kwani akina Maalim Seif walitoka wapi? Acheni kuwa na akili mgando.

Tukumbuke kwamba huyu mzee ni mwanamapinduzi aliyepigania uhuru wa Zanzibar hadi akamung’oa sultani. Moyo amepigania uhuru wa Zanzibar tangu zamani sana, hata kabla wazazi wa hayo makinda (ya kunguru) yanayopanua midomo kumdhihaki mzee wetu, hawajaliona jua. Sasa iweje watoto wadogo hawa wamdhihaki huyu mwanamapinduzi huku viongozi wa juu wa CCM wamekaa kimya? Au ndio tuseme kwamba ‘ukiona kifaranga juu ya kichuguu, mama yake yupo chini ya kichuguu hicho’?

Ni lini hasa wanaCCM wataanza kuthamini uhuru wa mawazo miongoni mwa makada wake? Tumekuwa tukisikia makada wengi wa CCM wakienda kinyume na mawazo ya kikandamizaji ya chama chao lakini hatukuwahi kusikia wakitishiwa kunyang’anywa kadi au kufutwa uanachama. Mifano halisi ni Mohamed Raza na mzee Sabodo. Raza amekuwa akienda kinyume na ukandamizaji wa CCM mara nyingi sana. Lakini kwa kuwa anazo fedha za kukifadhili chama, hatukuwahi kusikia akitishiwa kufutiwa uanachama. Aidha, mzee Sabodo, kada maarufu wa CCM, ameenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kukifadhili Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na huyu mzee kwa kuwa huwafadhili CCM pia hatukuwahi kusikia vitisho vyovyote dhidi yake.

Hata mtu uende kinyume na maagizo ya CCM, ilmradi tu unawafadhili fedha, hawana taabu nawe. Shida iliyopo ni kama mwanacham ataenda kinyume na mawazo yao halafu ukawa hana ufadhili wowote kwenye chama. Hata mfadhili angekuwa fisadi, mchafu au mnyonyaji, hawezi kufukuzwa uanachama. Kwa maana hiyo CCM ni chama kisichokuwa na ubaguzi wa aina ya wanachama—ni kama dodoki—huzoa kila aina ya uchafu ilmradi tu huo uchafu uwe na manufaa kwa chama. Kamwe tusitarajie kwamba mafisadi wataisha ndani ya CCM. Hilo haliwezekani hata kidogo.

TANGANYIKA KWANZA
:yield:

CCM mbele ya pesa huwa ni vipofu!ccm ilishakosa dira.Marehemu Kolimba tunakukumbuka
 
Mbona mnaongea kama hamjui jaman?
ccm CHAMA CHA MAJAMBAZ haina mjadala hapa,
Chama kiko kama mbu anakunyonya dam baadae akishiba sn anapasuka ndo ccm hii iliyoko,
Imeiba rasilimali za nchi hii mpaka sasa wanakaribia kupasuka ma hatimae kufa kabisa!!
Kikwete mwizi, mtoto wake muuza unga je? Hawa wa chini watakuwaje?
 
yani wakina lusinde, nnauye, mwigulu wamewaambukiza wenzao matusi ona walivyo hawana adabu mzee moyo asiwaambie ukweli matusi mmmh
 
Wanaongelea hayo wakiwa Zanzibar wakija Dodoma Wanaufyata na kina Nape Wanaufyatua.
 
Back
Top Bottom