Nimesikitishwa sana na kitendo cha UVCCM wa Zanzibar kutishia kumnyanganya na kumfuta uanachama wa CCM kada wake mkongwe mzee Nassoro Moyo eti kwa sababu tu anatetea na kusimamia wananchi wanyonge!Vitoto hivi, tena vinavyonuka mkojo na maziwa, vinapata wapi ujasiri wa kumdhalilisha mzee wetu. Mnatishia kumfukuza mzee wa watu kutoka CCM kana kwamba akitoka kwenye chama atakufa? Mnadhani ni ndani ya CCM tu ndipo kwenye uhai? Msijaribu kufananisha CCM na wanachama kama maji na samaki. Samaki ukimtoa ndani ya maji atakufa. Ingekuwa CCM ni maji na wanachama ni samaki, hilo tishio la kumtoa ndani ya chama lingekuwa na mashiko. Ni wanachama wangapi wamejitoa CCM na bado wanaendelea kuwatetea wananchi wakiwa nje ya chama hicho? Kwani akina Maalim Seif walitoka wapi? Acheni kuwa na akili mgando.
Tukumbuke kwamba huyu mzee ni mwanamapinduzi aliyepigania uhuru wa Zanzibar hadi akamungoa sultani. Moyo amepigania uhuru wa Zanzibar tangu zamani sana, hata kabla wazazi wa hayo makinda (ya kunguru) yanayopanua midomo kumdhihaki mzee wetu, hawajaliona jua. Sasa iweje watoto wadogo hawa wamdhihaki huyu mwanamapinduzi huku viongozi wa juu wa CCM wamekaa kimya? Au ndio tuseme kwamba ukiona kifaranga juu ya kichuguu, mama yake yupo chini ya kichuguu hicho?
Ni lini hasa wanaCCM wataanza kuthamini uhuru wa mawazo miongoni mwa makada wake? Tumekuwa tukisikia makada wengi wa CCM wakienda kinyume na mawazo ya kikandamizaji ya chama chao lakini hatukuwahi kusikia wakitishiwa kunyanganywa kadi au kufutwa uanachama. Mifano halisi ni Mohamed Raza na mzee Sabodo. Raza amekuwa akienda kinyume na ukandamizaji wa CCM mara nyingi sana. Lakini kwa kuwa anazo fedha za kukifadhili chama, hatukuwahi kusikia akitishiwa kufutiwa uanachama. Aidha, mzee Sabodo, kada maarufu wa CCM, ameenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kukifadhili Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na huyu mzee kwa kuwa huwafadhili CCM pia hatukuwahi kusikia vitisho vyovyote dhidi yake.
Hata mtu uende kinyume na maagizo ya CCM, ilmradi tu unawafadhili fedha, hawana taabu nawe. Shida iliyopo ni kama mwanacham ataenda kinyume na mawazo yao halafu ukawa hana ufadhili wowote kwenye chama. Hata mfadhili angekuwa fisadi, mchafu au mnyonyaji, hawezi kufukuzwa uanachama. Kwa maana hiyo CCM ni chama kisichokuwa na ubaguzi wa aina ya wanachamani kama dodokihuzoa kila aina ya uchafu ilmradi tu huo uchafu uwe na manufaa kwa chama. Kamwe tusitarajie kwamba mafisadi wataisha ndani ya CCM. Hilo haliwezekani hata kidogo.
TANGANYIKA KWANZA
:yield:
Watu na waseme CCM siyo Mama Yao! Ukifukuzwa tambua kuna vyama kibao, tafakari na jiunge na chama kingine kinacho vumilia uhuru wa MAWAZO.
Nimesikitishwa sana na kitendo cha UVCCM wa Zanzibar kutishia kumnyang'anya na kumfuta uanachama wa CCM kada wake mkongwe mzee Nassoro Moyo eti kwa sababu tu anatetea na kusimamia wananchi wanyonge!Vitoto hivi, tena vinavyonuka mkojo na maziwa, vinapata wapi ujasiri wa kumdhalilisha mzee wetu. Mnatishia kumfukuza mzee wa watu kutoka CCM kana kwamba akitoka kwenye chama atakufa? Mnadhani ni ndani ya CCM tu ndipo kwenye uhai? Msijaribu kufananisha CCM na wanachama kama maji na samaki. Samaki ukimtoa ndani ya maji atakufa. Ingekuwa CCM ni maji na wanachama ni samaki, hilo tishio la kumtoa ndani ya chama lingekuwa na mashiko. Ni wanachama wangapi wamejitoa CCM na bado wanaendelea kuwatetea wananchi wakiwa nje ya chama hicho? Kwani akina Maalim Seif walitoka wapi? Acheni kuwa na akili mgando.
Tukumbuke kwamba huyu mzee ni mwanamapinduzi aliyepigania uhuru wa Zanzibar hadi akamung'oa sultani. Moyo amepigania uhuru wa Zanzibar tangu zamani sana, hata kabla wazazi wa hayo makinda (ya kunguru) yanayopanua midomo kumdhihaki mzee wetu, hawajaliona jua. Sasa iweje watoto wadogo hawa wamdhihaki huyu mwanamapinduzi huku viongozi wa juu wa CCM wamekaa kimya? Au ndio tuseme kwamba ‘ukiona kifaranga juu ya kichuguu, mama yake yupo chini ya kichuguu hicho'?
Ni lini hasa wanaCCM wataanza kuthamini uhuru wa mawazo miongoni mwa makada wake? Tumekuwa tukisikia makada wengi wa CCM wakienda kinyume na mawazo ya kikandamizaji ya chama chao lakini hatukuwahi kusikia wakitishiwa kunyang'anywa kadi au kufutwa uanachama. Mifano halisi ni Mohamed Raza na mzee Sabodo. Raza amekuwa akienda kinyume na ukandamizaji wa CCM mara nyingi sana. Lakini kwa kuwa anazo fedha za kukifadhili chama, hatukuwahi kusikia akitishiwa kufutiwa uanachama. Aidha, mzee Sabodo, kada maarufu wa CCM, ameenda mbali zaidi hadi kufikia hatua ya kukifadhili Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Na huyu mzee kwa kuwa huwafadhili CCM pia hatukuwahi kusikia vitisho vyovyote dhidi yake.
Hata mtu uende kinyume na maagizo ya CCM, ilmradi tu unawafadhili fedha, hawana taabu nawe. Shida iliyopo ni kama mwanacham ataenda kinyume na mawazo yao halafu ukawa hana ufadhili wowote kwenye chama. Hata mfadhili angekuwa fisadi, mchafu au mnyonyaji, hawezi kufukuzwa uanachama. Kwa maana hiyo CCM ni chama kisichokuwa na ubaguzi wa aina ya wanachama-ni kama dodoki-huzoa kila aina ya uchafu ilmradi tu huo uchafu uwe na manufaa kwa chama. Kamwe tusitarajie kwamba mafisadi wataisha ndani ya CCM. Hilo haliwezekani hata kidogo.
TANGANYIKA KWANZA
:yield:
Hivi yule shekhe anaelilia wazee hayupo amlilie mzee moyo?
Shekh hawezi kumlilia Nyerere huyo ni mlilia Tumbo.na ukweli kabisa shekh hawezi toka BAKWATA.
na wewe jeuri ya kuwasemea wazanzibar amekupa nani. unacheza ngoma usiyoijua.