gogo la shamba
JF-Expert Member
- Mar 1, 2013
- 6,669
- 2,165
hapo ni sawa na kuisema serikali ndani ya bunge la zima utapambana na wabunge wa ccm,hao ni watu waliopoteza dira hawajui waendako wala watokapo
UVCCM wapuuzwe. Hawa UVCCM ni watoto wa Mafisadi, wametumwa kuwalaghai watanzania.
Ewe Mtanzania, amka na sumbua akili yako kidogo na tafakari haya Maswali hapa chini:
A - Shule za kata hazina waalimu, hazina maabara.
B- Kama waalimu wapo wachache, hata hao wachache wanakosa mshahara na wanakosa moyo wa kufundisha hivyo kuleta Division zero nyiingi sana. Wanaoathirika ni watoto wa walalahoi- hawa watoto wa UVCCM wanasoma International schools na ni watoto wa vigogo.
C- Ajira ni shida kwa vijana. Wengi waliomaliza form 4 na kupata div 0, wanakuwa wamachinga na wanapigwa mabomu na serikali ya CCM, baba zao UVCCM.
D - Mikopo Chuo kikuu ni shida, watoto wa masikini hawapati.
Sasa naomba muwaulize UVCCM haya maswali. Mbona matamko kuhusu haya masuala hapo juu hawatoi???? Watanzania amkeni, kataeni propaganda za mwaka 47'.