*UMOJA WA VIJANA WA CHAMA CHA MAPINDUZI MKOA WA MBEYA-UVCCM UNAPINGA MAAMUZI YA BASATA KUMFUNGIA MSANII WEMA SEPETU KWA MUDA USIOJULOKANA.*
Akinukuliwa na moja ya chombo cha habari alipoulizwa kuhusu maoni ya UVCCM kufuatia Wema Sepetu kufungiwa na BASATA kwa kile kinachoitwa kusambaza picha na video za utupu mtandaoni, Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Mbeya bwana Mashango ameeleza kwamba wamesikitishishwa sana na kitendo cha BASATA kumfungia Wema Sepetu ikiwa tayari ameshajutia na kuomba msamaha kwa jamii na mamlaka husika juu ya picha na video zilizoeneoa mtandaoni zikimuonesha akiwa mtupu.
"Kuna haja gani ya kumuadhibu mtu ambaye ametambua makosa na kuomba msamaha, tumefundishwa kusamehana inapolazimu". Ameeleza Mashango
Ameeleza kwamba sehemu kubwa ya wasanii ni vijana na wamekuwa sehemu ya ushindi wa CCM 2015 ,na kwa hivyo wanapoonewa na mamlaka yoyote UVCCM itaendelea kuwatetea kwa kadri ya uwezo wake.
"CCM imewakosea wasanii mara kadhaa wakati wa chaguzi lakini hawajawahi iadhibu kama wanavyoadhibiwa na BASATA" aliongeza Mashango.
Mashango ameeleza kwamba watawasilisha maoni yao kwa uongozi wa UVCCM Taifa ili Serikali iingilie na kuzuia manyanyaso kwa wasanii yanafanywa na BASATA.
Imetolewa na ofisi ya Katibu -UVCCM MBEYA.
Adia Rashid.