- Feb 10, 2006
- 4,542
- 16,811
Maxence MeloWakuu,
Mtakumbuka mnamo mwezi Machi/Aprili (kama sijakosea) mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko UVCCM Hussein Bashe aliahidi kutuomba JF ushauri juu ya reforms ndani ya chama.
Ametuomba kumpa ushirikiano (kama huna mapendekezo, bora usiandike) katika hili na hivyo naleta rai kwenu ambao mngependa au mpo tayari kutoa ushirikiano kwake (positive and negatives bila kujali itikadi za vyama) juu ya masuala yafuatayo:
- Ni yepi mangufu ndani ya UVCCM katika:
Maeneo haya matatu ndiyo kaomba tumpe maoni ili ayawasilishe na atakiri ni ya wana JF na anaomba wale ambao wangependa kumtumia maoni personally na si kuandika kwenye thread hii (ambayo watajitahidi kuifuatilia kwa karibu) amwandikie - maoniuvccm@yahoo.com au hussein@newhabari.com
- Muundo
- Mfumo wa upataji viongozi
- Mfumo wa mawasiliano wa UVCCM
Mkuu, nimemuelewa Maxence. Anamaanisha kama huna mapendekezo ni afadhali usiandike kabisa. Neno 'bora' limetumika kama 'afadhali'. Jaribu kurejea tena kusoma, ni makosa ya uwasilishaji tu.Kabla sijatoa mapendekezo bora unayoyataka tuwekane sawa kwanza hiyo 'bora' unaipimaje maana mtoa hoja anaweza kuona mawazo yake ni bora kumbe kwako si bora, kwa vile umesema unahitaji mawazo yeyote yawe positive au negative mimi ninayo mapendekezo bora lakini negative je yatakufaa.
NAHISI UKO SAWAA.......Lakini unadhani watasikiliza haooo??/!!!..UNDENI CCM mpyaaa.... yenye watu wapya... tatizo top rank mnarithishana....tena hawana elimu.... utasikia kasoma India, USA..... ni scraperz..... nahsi ni CHHAMA CHA KIKOO 2015UVCCM wafanye Outreach kwa Ratiba maalumu. Wawe Independent katika kuendesha mabaraza yao na wafanye kazi kwa karibu zaidi na secretariet ya chama chao.
Uwakilishi wao kwenye kamati kuu ya chama inabidi uongezeka kwa kuzingatia population kubwa ya watanzania ambao ni vijana
Waache kuumarisha magenge ya kihuni na badala yake wawaeke mechanism ya kulea viongozi wa sasa na wa baadae.
Kwa kuwa wana vitega uchumi vya kutosha, basi waanzishe vyuo vya kufundisha makada wao kutoka sehemu zote Tanzania na kuwaingiza kwenye majimbo na wilaya
Tungeni katiba yenye mwanya wa watu kuunda petition pale wanapoona viongozi wao wajuu wanaenda vibaya au kuwa na mwelekeo wa kutumiwa na watu nje ya umoja wa vijana.
Tafsiri Itikadi yenu na muelekeze katika mitaala ya chuo mtakachoanzisha.Tumieni mtaji mkubwa mlio nao kiuchumi kuwekeza na kushinikiza utungaji wa sera zenye maslahi kwa vijana na muwe sharp kuji-associate na hizo sera
Wape umoja wa vijana meno ya kukosoa hata viongozi hadharani na kuwapa nguvu ya kushinikiza kujiuzulu kwa viongozi goi goi ili kurejesha heshima,nguvu na mvuto wa Umoja wenu
Kwa sababu nimepita tu haraka haraka nikaona nitoe mapendekezo ya dhati kabisa labda nikipata muda baaade nitatoa mchango wangu.
Siasa si uadui
Vunjeni kabisa na muanze usajili upya bila kuwa na upendeleo wala uroho wa madaraka ya ukuu wa wilaya.
Wakuu,
Mtakumbuka mnamo mwezi Machi/Aprili (kama sijakosea) mwenyekiti wa kamati ya Mabadiliko UVCCM Hussein Bashe aliahidi kutuomba JF ushauri juu ya reforms ndani ya chama.
Ametuomba kumpa ushirikiano (kama huna mapendekezo, bora usiandike) katika hili na hivyo naleta rai kwenu ambao mngependa au mpo tayari kutoa ushirikiano kwake (positive and negatives bila kujali itikadi za vyama) juu ya masuala yafuatayo:
- Ni yepi mangufu ndani ya UVCCM katika:
Maeneo haya matatu ndiyo kaomba tumpe maoni lakini anakaribisha maoni hata kwa mapungufu mengine (not limited) kwa uwazi bila kubanwa na hayo matatu juu, ili ayawasilishe na atakiri ni ya wana JF na anaomba wale ambao wangependa kumtumia maoni personally na si kuandika kwenye thread hii (ambayo watajitahidi kuifuatilia kwa karibu) amwandikie - maoniuvccm@yahoo.com au hussein@newhabari.com
- Muundo
- Mfumo wa upataji viongozi
- Mfumo wa mawasiliano wa UVCCM
kamanda, hayo marekebisho yaanze hata na namna approach ya improvement ilivyoletwa hapa jamviniSafi sana Max......Ukweli ni kwamba UVCCM inahitaji marekebisho makubwa sana....