UVCCM kwachafuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UVCCM kwachafuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Oct 25, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  • MADAI YA RUSHWA YATAWALA,
  • MALISA, SHIGELLA, BASHE, NYALANDU WATUHUMIWA,
  • MAKONDA ATOA KAULI NZITO
  MATOKEO ya uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) yametangazwa jana huku kukiwa na harakati za kuyapinga kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

  Kati ya mambo yaliyotajwa kupindisha taratibu za uchaguzi huo uliofanyika juzi ni kile kilichoelezwa kuwa ni kutawaliwa na vitendo vya rushwa.

  Baada ya Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutangaza matokeo, baadhi ya vijana waliyapinga na kuanza kukusanya saini 340 ili kuyapinga.

  Katika kuonyesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, baadhi ya wajumbe walibeba mabango yenye ujumbe wa kutokubaliana na matokeo, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein baada ya kumaliza kufunga mkutano huo.

  Moja ya bango hilo lilikuwa na maneno: "Jumuiya si ya Lowassa na wafuasi wake (Benno, Bashe, Zungu, Zabein…..) hivyo jumuiya itakuwa na kambi mbili ya kwanza jukwaani na kambi ya mezani."

  Bango jingine lilisomeka: "Jumuiya imara hujengwa na uchaguzi wa haki na siyo rushwa za Bashe, Benno na Zungu."

  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ni miongoni mwa makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kambi yake imekuwa ikitajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

  Kwa tafsiri ya mabango hayo, Benno (Malisa) alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Bashe (Hussein) naye alikuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo ambaye amemaliza muda wake
  .
  Maofisa usalama na walinzi wa jumuiya hiyo ambao walikuwa wakijaribu kuwanyang'anya vijana hao mabango walishindwa, hivyo kulazimika kusubiri dakika kama tano hivi hadi msafara wa Dk Shein ulipoondoka walipowatoa nje ya eneo la ukumbi wa mkutano
  .
  Tukio hilo lilizua tafrani baada ya walinzi hao kuwanyanyua juujuu vijana wawili kati ya sita waliokuwa na mabango, huku wengine wakionekana kutaka kuwapiga lakini polisi waliingilia kati na kuwatoa nje.

  Baadaye polisi waliondoka na vijana watatu katika tukio ambalo lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu na baadhi ya wagombea ambao walishindwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa UVCCM.

  Vijana walalama

  Mapema jana asubuhi, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walikutana na waandishi wa habari na kulalamika kwamba rushwa ilitawala huku wakiwatuhumu viongozi wa UVCCM na baadhi ya makada wa chama hicho kwa kuhusika na vitendo hivyo.
  Waliotajwa ni pamoja Malisa, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, Bashe na mtoto wa Lowassa, Fredy.

  "Kama Rais Jakaya Kikwete kweli yuko makini na kauli zake ni za dhati, basi atengue matokeo ya uchaguzi huu maana kanuni zimekiukwa na kusema kweli rushwa ilitawala. Atumie nafasi yake kurejesha hadhi ya chama, huu uchaguzi ni batili," alisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Morogoro, Augustine Matefu.

  Walidai kuwa Bashe ndiye aliyekuwa mratibu wa uingizaji wa fedha katika eneo la mkutano ambazo zilitumika kugawanywa kwa wajumbe na kwamba Malisa na Shigela waligawa Sh1 milioni kwa viongozi wa mikoa kama hatua ya kumpigia kampeni mmoja wa wagombea walioshinda.

  Kada mwingine, Livamba Adinan Selemani alisema: "Vijana kweli tumempuuza Rais, kweli mtu ambaye hana hela hawezi kupata uongozi UVCCM, kwa maana nyingine nchi yetu inakwenda pabaya. Watu wachache wenye fedha wanaweza kuamua kufanya wanachotaka, hivyo ndivyo uchaguzi wetu wa vijana ulivyokuwa."

  Mjumbe mwingine, Kichanta Selemani alisema malalamiko ya viongozi wa UVCCM kuwapendelea baadhi ya wagombea yalifikishwa kwa Lukuvi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

  Wakati makada hao wa CCM wakizungumza na waandishi wa habari, lilitokea kundi jingine la makada wa chama hicho ambao walianza kuzozana na wenzao wakisema kuwa malalamiko yao yanatokana na kushindwa na kwamba walitaka kutumia: "Viongozi wa ngazi za juu za CCM" kuwachagulia vijana viongozi.

  Kundi hilo la pili lilidai kuwa katika uchaguzi huo kundi hilo la kwanza ndilo lililohonga fedha na kumtaja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwamba alikuwa akiwashawishi wajumbe kwa fedha kumchagua mmoja wa wagombea.

  Akizungumzia tuhuma hizo, Nyalandu alisema kupitia ujumbe wa simu yake ya mkononi: "Mimi siyo mjumbe wala mgombea na wala sihusiki kwa lolote. Nilikwenda ukumbini na waziri mwenzangu na baadaye tukaondoka pamoja. Hao ni waongo wakubwa na wazushi wachache wanaonunua haki."

  Hakuna mtu yeyote niliyeongea naye wala kutoa hela yoyote kwa sababu zozote zile na tulikuwa ukumbini baadaye nje wote pamoja (na waziri). Shame to them who lie (aibu kwao wanaosema uongo) na wataje majina yao tuyasikie."

  Alimtaja Waziri aliyekuwa naye kuwa ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tzeba kwa lengo la kuwasalimia vijana ambao walikuwa wakiendelea na mkutano wa uchaguzi.

  Watuhumiwa wanena

  Kwa nyakati tofauti, wakijibu tuhuma hizo watuhumiwa wote walikanusha kuhusika kutoa rushwa na kuwataka wanaolalamika kupeleka ushahidi wao Takukuru na kufikisha malalamiko hayo katika vikao vya ulinzi na maadili vya CCM.

  Shigela kwa upande wake, akizungumza na waandishi wa habari alisema kinachotokea sasa kuhusu tuhuma hizo kilitarajiwa kwani ni kawaida watu wanaposhindwa katika uchaguzi kutoa malalamiko hata kama hawana ushahidi wa tuhuma husika.

  Shigela alikanusha yeye na Malisa kutoa fedha kwa viongozi wa mikoa akisema kwa nafasi yake asingeweza kupata fursa ya kufanya hivyo kwani alikuwa mratibu mkuu wa uchaguzi kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.

  "Kama kuna watu hawakuridhika kuna taratibu za chama inabidi zifuatwe, kwa mujibu wa taratibu zetu kuna siku 14 za malalamiko na hizo mtu anaweza kuzitumia kuandika malalamiko yake na yapelekwe kwa viongozi wahusika ili wachuke hatua," alisema Shigela na kuongeza:

  "Vinginevyo taratibu za chama haziruhusu kutoa au kupokea rushwa kwa namna yeyote, kwa hiyo kama mtu anadhani ana uwezo aitumikie jumuiya popote pale alipo kwa sababu wote hatuwezi kuwa viongozi kwa pamoja."

  Kwa upande wake, Malisa alisema: "Nimefanya kazi yangu na kutekeleza wajibu wangu kwa ukamilifu, kama kuna jambo lolote ambalo linahusu UVCCM, basi kamuulizeni mwenyekiti wa jumuiya maana yupo."

  Bashe alikanusha kuhusika na vitendo vya rushwa na kuwataka wanaotoa madai hayo, kama wana ushahidi waupeleke Takukuru au kufikisha suala hilo katika vikao vya chama hicho.

  "Waambieni kwamba wasilete siasa za shule za sekondari UVCCM, maana kama wangeshinda ni dhahiri kwamba wasingelalamika. Ninawapa ushauri wa bure, kwanza kama wana ushahidi wa madai hayo kwamba mimi Hussein nimetoa rushwa, basi wapeleke ushahidi wao Takukuru lakini pia ndani ya chama tunayo Kamati ya Maadili na Usalama wapeleke malalamiko yao huko ili yafanyiwe kazi."

  Alisema hawezi kujihusisha na rushwa kwani hata Rais Kikwete katika hotuba ya ufunguzi alikemea vitendo hivyo.

  Fredy akizungumza kwa simu alisema: "Tuhuma hizo siyo za kweli kwani mimi licha ya kwamba nilipata barua ya mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo sikuenda Dodoma kutokana na kubanwa na kazi.

  "Kwanza mimi si mjumbe wa mkutano mkuu japokuwa ni Katibu wa Uhamasishaji wa Mkoa wa Arusha. Nilipata mwaliko lakini sikuweza kufika huko (Dodoma) nimetingwa na kazi nyingi," alisema.

  Matokeo ya uchaguzi

  Lukuvi alimtangaza Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM baada ya kupata kura 483.

  Sadifa alimshinda Rashid Simai Msaraka aliyepata kura 263, wakati mgombea mwingine Lulu Msham Abdallah licha ya kujitoa katika kinyang'anyiro hicho muda mfupi kabla ya kura kupigwa, alipata kura nane.

  Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mboni Muhita alishinda katika duru ya pili baada ya kupata kura 489 na kumshinda, Paul Makonda aliyepata kura 241.

  Katika duru ya kwanza, Mboni alikuwa amepata kura 361 na Makonda kura 206, huku mgombea mwingine Ally Salum Hapi akipata kura 179. Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya wagombea wote kutofikisha nusu ya kura kama kanuni zinavyotaka.

  "Sheria kushindwa kwa heshima kuliko kushinda kwa fedheha."

  Makonda aliyekuwa akizungumza kwa hisia jukwaani alisema ikiwa UVCCM wanataka kujenga taasisi yenye nguvu na inayoaminika, lazima wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaua demokrasia.

  "Uchaguzi tulioufanya hatukumchagua Sadifa wala Mboni, bali tumechagua uongozi wa aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa tutarajie jumuiya hiyo…. kama sikueleweka historia itakuja kutuambia maana ya maneno haya," alisema Makonda na kuongeza:

  "Kama kuna mtoto wa maskini, mtoto wa mkulima kama mimi amechagua au kupiga kura yake kwa sababu ya rushwa, basi ajue amepanda mbegu maishani mwake."

  Baada ya Makonda kutoa kauli hizo alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja nje ya ukumbi ambako baadhi ya wapambe wake walimfuata na kuanza kulia machozi.

  Baadhi yao walisikika wakisema kwamba UVCCM wameisaliti demokrasia kutokana na nguvu ya fedha. Hata hivyo, Makonda alikuwa akiwafariji kwa kuwaambia wasife moyo.

  Chanzo: Mwananchi
   
 2. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #2
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wangetoa macho ingependeza sana! Na hizi rushwa wanaogawa kama njugu watakuja kujutia!
   
 3. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #3
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,800
  Likes Received: 3,884
  Trophy Points: 280
  hawa wanaotoa rushwa pesa wanatoa wapi???
   
 4. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #4
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Toka lini nyoka akazaa konokono???? Mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
   
 5. Godlisten Masawe

  Godlisten Masawe Verified User

  #5
  Oct 25, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 739
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huyu Makonda alitegemea kuna demokrasia ndani ya ccm, mbona wanachama wa ccm wanafiki hivi?
   
 6. K

  Kitanga Member

  #6
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 17, 2012
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wasioridhika na matokeo haya na wanachukia rushwa kwa dhati wasilalamike wakati chama hakitachukua hatua yo yoye.

  Maovu yalianzia katika hatua ya Wilaya, Mkoa na sasa Kitaifa lakini wenye chama wako kimya. Tena la juzi kwa upande wa UWT lilikuwa kubwa zaidi lakini hata Chairman aliishia kulalamika si kuchukua hatua kama vile kutengua matokeo!

  Vyombo vya ulinzi na usalama vipo (TAKUKURU) walifanya nini, ni kama wameshikwa na mafisadi, haiwezekani muda wote huo wasithubutu hata kumtia mtu hatiani ili asafishwe na Mahakama! Hao vijana watafute mahala pa kwenda mapema kama wanaichukia rushwa na wanaipenda Tanzania. Na uamuzi wao utakuwa ni mtaji tosha kupata support ya Watanzania maskini ambao ndo wengi na wengependa kuona watu wanowatetea.

  CCM ni kama kokoro (JKN)
   
 7. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #7
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Lini palikuaga pasafi?
   
 8. i

  iseesa JF-Expert Member

  #8
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 944
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa MKUU. Na "Mwana wa Mhunzi asiposana, hufukuta"
   
 9. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #9
  Oct 25, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,743
  Likes Received: 1,804
  Trophy Points: 280
  Yetu macho. mkidhani fedha ni kila kitu basi siku ya kujuta haiko mbali.mtapigana wee mwisho chama chenu kitakwenda kule waliko UNIP,KANU,UPC etc
   
 10. a

  afwe JF-Expert Member

  #10
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 4,087
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Ndio madhara ya wanaokuwa madarakani kujilimbikizia mali. Hawana namna nyingine ya kuzitumia zaidi ya kujiongezea nguvu ya madaraka kwa gharama yoyote ile hata kama ni kwa kuua
   
 11. manuu

  manuu JF-Expert Member

  #11
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 23, 2009
  Messages: 4,063
  Likes Received: 9,673
  Trophy Points: 280
  Ndiyo kwanza movie haijaanza hii ni trailer tu.
   
 12. w

  wakupita Member

  #12
  Oct 25, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 15
  Who is Makonda???Ye haoni majina ya wenzake yanafanana fanana na wenye nchi bana!
   
 13. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  wafu wanazika wafu wenzao...raha sana..rot in hell...dunderheads
   
 14. m

  malaka JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 5, 2012
  Messages: 1,323
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Da pesa zetu za NSSF zinafanya kazi aiseee!! Inauma sana. Ila kwanini watu hawabadiliki jamani?
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mie nilijua tu kuwa haya ndio yatakuwa matokeo.
  Hawa watoto ni wajinga sana. Hivi kwani wanadhani lini sisi M iliwahi kujitenga na rushwa?
  Kwa kadri ninavyofahamu, hakuna rushwa hakuna sisi M
  Watapiga kelele weeeee mwisho hawatauona. Achana na sisi M nyie vijana kaibeni mpate pesa kisha rudini mgombee kwa rushwa kama kweli mna nia ya kupata uongozi ndani ya lichama lenu.
  La msingi mjue tu piga ua sie huku wananchi hatutawapa uongozi wa kitaifa.
   
 16. Laurence

  Laurence JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 3,106
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Hao ndio CcM,baba analia,watoto wanalia sasa hakuna wa kumbembeleza mwenzie,kazi kwenu.
   
 17. Lucy Godfrey

  Lucy Godfrey JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 45
  ehe ndo pa kushangaa hapo lini kulishawahi kuwa kusafi mpaka pachafuke leo,mana kama kuchafuka sijui nilinganishe na nini.....:nimekataa:nimekataa:nimekataa
   
 18. s

  step Senior Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 190
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Shida ubishi tuuuuuuuuuuuuu! watu wakiambiwa watoke huko waliko hawataki ccm haiokoleki nawashauri wahame mapema kama alivyofanya Alfonce Mawazo wa Ar ona sasa joto amelionja huyu mbishi Makonda kuda dada deki!!!
   
 19. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Ukiingia chooni, usishike pua vumilia harufu hadi umalize haja yako.
  Hapa kilio cha wavujajasho/walalahoi Mungu ameisikia.
   
 20. d

  detawa hoki Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kiwango cha tatizo kimeongezeka kwa kasi ya jabu...exponentially u may say

  mwanzoni ilikuwa ya kujifichaficha... sasa ni wazi kabisa...mchana kweupe....sababu kuna selective enforcement ya sheria
   
Loading...