UVCCM kwachafuka

Baba na Mama zao wanashika nafasi ndani ya CCM kwa rushwa. Unategemea uzao wao uweje?. Ukipanda bangi usitegemee kuvuna mtama. Tangu lini nyoka kazaa panya.

Kumbuka: Law of Consistency.
 
Hivi kweli bado kuna vijana wako CCM wanaotegemea kwamba rushwa ni dhambi? Kijana yeyote aliye CCM yuko huko kwa sababu ya Pesa. Hapa tatizo mshiko umezidiana.
 
wapo wapi akina RITZ, REJAO et al mawazo na michango yako inahitajika hapa!
 
hivi siku ile ya ufunguzi wa kikao chao nape alikuwa amefurahi kaonekana tbc anapiga gitaa ilkuwa anashangilia rushwa au
 
Hivi jamani watu wanahainga nini na chama ambacho hata mwenyekiti wake amekiri kuwa kimebobea kwa rushwa????

Lichama lenyewe limekufa......!!!
 
Wangetoa macho ingependeza sana! Na hizi rushwa wanaogawa kama njugu watakuja kujutia!

Wakati wanatoa rushwa hawa wanaolalama walikuwa wamefungwa vitambaa usoni? au ndio kutafuta pa kutokea! Sielewi mimi somo hilo.
 
Sioni tatizo kwa UVCCM kulalamikia rushwa na niseme kitu
kimoja.CCM ya sasa sio ile yenye maadili yaMWANA tanu,
Nimewahi kusoma barua ya Butiku ya mwaka 2005 akilalamika
kama juu ya kuvunjwa kwa katiba ili kumbeba JK. Nahiyo barua
kila mtu anaweza kuipata kutoka katika kitabu cha Mpendazoe cha
Tutashinda. kwa ufupi tu , nikwamba hakuna kitu huko kinachoweza
kuisaidia TZ zaidi ya kuiuza tu.
 
Kuna watu ni wapumbavu sana tena kupindukia. Na si wengine ni hao wanaolalamika hovyo baada ya kushindwa kwenye chaguzi za CCM. Wanajua lichama lao la kifisadi, rushwa ni "business as usual" alafu wanategemea kupita bila rushwa. Tangu lini ukalisukuma gari ukiwa ndani ya gari? Come on, get out!!!!!!!, tokeni nje acheni kulalamika. Mbona hata mahjiulizi mbona CDM kwenye chaguzi zao hawalalamiki?

Siku hizi kila mtu anayeshindwa CCM lazima alalamike, mpaka waziri mkuu mstaafu, analalamika sasa akina hohehahe, tutafanyaje? Wakiyatenda haya kwenye mti mbichi, itakuwaje kwenye mti mkavu?
 
  • MADAI YA RUSHWA YATAWALA,
  • MALISA, SHIGELLA, BASHE, NYALANDU WATUHUMIWA,
  • MAKONDA ATOA KAULI NZITO
MATOKEO ya uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) yametangazwa jana huku kukiwa na harakati za kuyapinga kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

Kati ya mambo yaliyotajwa kupindisha taratibu za uchaguzi huo uliofanyika juzi ni kile kilichoelezwa kuwa ni kutawaliwa na vitendo vya rushwa.

Baada ya Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutangaza matokeo, baadhi ya vijana waliyapinga na kuanza kukusanya saini 340 ili kuyapinga.

Katika kuonyesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, baadhi ya wajumbe walibeba mabango yenye ujumbe wa kutokubaliana na matokeo, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein baada ya kumaliza kufunga mkutano huo.

Moja ya bango hilo lilikuwa na maneno: “Jumuiya si ya Lowassa na wafuasi wake (Benno, Bashe, Zungu, Zabein…..) hivyo jumuiya itakuwa na kambi mbili ya kwanza jukwaani na kambi ya mezani.”

Bango jingine lilisomeka: “Jumuiya imara hujengwa na uchaguzi wa haki na siyo rushwa za Bashe, Benno na Zungu.”

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ni miongoni mwa makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kambi yake imekuwa ikitajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Kwa tafsiri ya mabango hayo, Benno (Malisa) alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Bashe (Hussein) naye alikuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo ambaye amemaliza muda wake
.
Maofisa usalama na walinzi wa jumuiya hiyo ambao walikuwa wakijaribu kuwanyang’anya vijana hao mabango walishindwa, hivyo kulazimika kusubiri dakika kama tano hivi hadi msafara wa Dk Shein ulipoondoka walipowatoa nje ya eneo la ukumbi wa mkutano
.
Tukio hilo lilizua tafrani baada ya walinzi hao kuwanyanyua juujuu vijana wawili kati ya sita waliokuwa na mabango, huku wengine wakionekana kutaka kuwapiga lakini polisi waliingilia kati na kuwatoa nje.

Baadaye polisi waliondoka na vijana watatu katika tukio ambalo lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu na baadhi ya wagombea ambao walishindwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa UVCCM.

Vijana walalama

Mapema jana asubuhi, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walikutana na waandishi wa habari na kulalamika kwamba rushwa ilitawala huku wakiwatuhumu viongozi wa UVCCM na baadhi ya makada wa chama hicho kwa kuhusika na vitendo hivyo.
Waliotajwa ni pamoja Malisa, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, Bashe na mtoto wa Lowassa, Fredy.

“Kama Rais Jakaya Kikwete kweli yuko makini na kauli zake ni za dhati, basi atengue matokeo ya uchaguzi huu maana kanuni zimekiukwa na kusema kweli rushwa ilitawala. Atumie nafasi yake kurejesha hadhi ya chama, huu uchaguzi ni batili,” alisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Morogoro, Augustine Matefu.

Walidai kuwa Bashe ndiye aliyekuwa mratibu wa uingizaji wa fedha katika eneo la mkutano ambazo zilitumika kugawanywa kwa wajumbe na kwamba Malisa na Shigela waligawa Sh1 milioni kwa viongozi wa mikoa kama hatua ya kumpigia kampeni mmoja wa wagombea walioshinda.

Kada mwingine, Livamba Adinan Selemani alisema: “Vijana kweli tumempuuza Rais, kweli mtu ambaye hana hela hawezi kupata uongozi UVCCM, kwa maana nyingine nchi yetu inakwenda pabaya. Watu wachache wenye fedha wanaweza kuamua kufanya wanachotaka, hivyo ndivyo uchaguzi wetu wa vijana ulivyokuwa.”

Mjumbe mwingine, Kichanta Selemani alisema malalamiko ya viongozi wa UVCCM kuwapendelea baadhi ya wagombea yalifikishwa kwa Lukuvi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Wakati makada hao wa CCM wakizungumza na waandishi wa habari, lilitokea kundi jingine la makada wa chama hicho ambao walianza kuzozana na wenzao wakisema kuwa malalamiko yao yanatokana na kushindwa na kwamba walitaka kutumia: “Viongozi wa ngazi za juu za CCM” kuwachagulia vijana viongozi.

Kundi hilo la pili lilidai kuwa katika uchaguzi huo kundi hilo la kwanza ndilo lililohonga fedha na kumtaja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwamba alikuwa akiwashawishi wajumbe kwa fedha kumchagua mmoja wa wagombea.

Akizungumzia tuhuma hizo, Nyalandu alisema kupitia ujumbe wa simu yake ya mkononi: “Mimi siyo mjumbe wala mgombea na wala sihusiki kwa lolote. Nilikwenda ukumbini na waziri mwenzangu na baadaye tukaondoka pamoja. Hao ni waongo wakubwa na wazushi wachache wanaonunua haki.”

Hakuna mtu yeyote niliyeongea naye wala kutoa hela yoyote kwa sababu zozote zile na tulikuwa ukumbini baadaye nje wote pamoja (na waziri). Shame to them who lie (aibu kwao wanaosema uongo) na wataje majina yao tuyasikie.”

Alimtaja Waziri aliyekuwa naye kuwa ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tzeba kwa lengo la kuwasalimia vijana ambao walikuwa wakiendelea na mkutano wa uchaguzi.

Watuhumiwa wanena

Kwa nyakati tofauti, wakijibu tuhuma hizo watuhumiwa wote walikanusha kuhusika kutoa rushwa na kuwataka wanaolalamika kupeleka ushahidi wao Takukuru na kufikisha malalamiko hayo katika vikao vya ulinzi na maadili vya CCM.

Shigela kwa upande wake, akizungumza na waandishi wa habari alisema kinachotokea sasa kuhusu tuhuma hizo kilitarajiwa kwani ni kawaida watu wanaposhindwa katika uchaguzi kutoa malalamiko hata kama hawana ushahidi wa tuhuma husika.

Shigela alikanusha yeye na Malisa kutoa fedha kwa viongozi wa mikoa akisema kwa nafasi yake asingeweza kupata fursa ya kufanya hivyo kwani alikuwa mratibu mkuu wa uchaguzi kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.

“Kama kuna watu hawakuridhika kuna taratibu za chama inabidi zifuatwe, kwa mujibu wa taratibu zetu kuna siku 14 za malalamiko na hizo mtu anaweza kuzitumia kuandika malalamiko yake na yapelekwe kwa viongozi wahusika ili wachuke hatua,” alisema Shigela na kuongeza:

“Vinginevyo taratibu za chama haziruhusu kutoa au kupokea rushwa kwa namna yeyote, kwa hiyo kama mtu anadhani ana uwezo aitumikie jumuiya popote pale alipo kwa sababu wote hatuwezi kuwa viongozi kwa pamoja.”

Kwa upande wake, Malisa alisema: “Nimefanya kazi yangu na kutekeleza wajibu wangu kwa ukamilifu, kama kuna jambo lolote ambalo linahusu UVCCM, basi kamuulizeni mwenyekiti wa jumuiya maana yupo.”

Bashe alikanusha kuhusika na vitendo vya rushwa na kuwataka wanaotoa madai hayo, kama wana ushahidi waupeleke Takukuru au kufikisha suala hilo katika vikao vya chama hicho.

“Waambieni kwamba wasilete siasa za shule za sekondari UVCCM, maana kama wangeshinda ni dhahiri kwamba wasingelalamika. Ninawapa ushauri wa bure, kwanza kama wana ushahidi wa madai hayo kwamba mimi Hussein nimetoa rushwa, basi wapeleke ushahidi wao Takukuru lakini pia ndani ya chama tunayo Kamati ya Maadili na Usalama wapeleke malalamiko yao huko ili yafanyiwe kazi.”

Alisema hawezi kujihusisha na rushwa kwani hata Rais Kikwete katika hotuba ya ufunguzi alikemea vitendo hivyo.

Fredy akizungumza kwa simu alisema: “Tuhuma hizo siyo za kweli kwani mimi licha ya kwamba nilipata barua ya mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo sikuenda Dodoma kutokana na kubanwa na kazi.

“Kwanza mimi si mjumbe wa mkutano mkuu japokuwa ni Katibu wa Uhamasishaji wa Mkoa wa Arusha. Nilipata mwaliko lakini sikuweza kufika huko (Dodoma) nimetingwa na kazi nyingi,” alisema.

Matokeo ya uchaguzi

Lukuvi alimtangaza Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM baada ya kupata kura 483.

Sadifa alimshinda Rashid Simai Msaraka aliyepata kura 263, wakati mgombea mwingine Lulu Msham Abdallah licha ya kujitoa katika kinyang’anyiro hicho muda mfupi kabla ya kura kupigwa, alipata kura nane.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mboni Muhita alishinda katika duru ya pili baada ya kupata kura 489 na kumshinda, Paul Makonda aliyepata kura 241.

Katika duru ya kwanza, Mboni alikuwa amepata kura 361 na Makonda kura 206, huku mgombea mwingine Ally Salum Hapi akipata kura 179. Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya wagombea wote kutofikisha nusu ya kura kama kanuni zinavyotaka.

“Sheria kushindwa kwa heshima kuliko kushinda kwa fedheha.”

Makonda aliyekuwa akizungumza kwa hisia jukwaani alisema ikiwa UVCCM wanataka kujenga taasisi yenye nguvu na inayoaminika, lazima wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaua demokrasia.

“Uchaguzi tulioufanya hatukumchagua Sadifa wala Mboni, bali tumechagua uongozi wa aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa tutarajie jumuiya hiyo…. kama sikueleweka historia itakuja kutuambia maana ya maneno haya,” alisema Makonda na kuongeza:

“Kama kuna mtoto wa maskini, mtoto wa mkulima kama mimi amechagua au kupiga kura yake kwa sababu ya rushwa, basi ajue amepanda mbegu maishani mwake.”

Baada ya Makonda kutoa kauli hizo alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja nje ya ukumbi ambako baadhi ya wapambe wake walimfuata na kuanza kulia machozi.

Baadhi yao walisikika wakisema kwamba UVCCM wameisaliti demokrasia kutokana na nguvu ya fedha. Hata hivyo, Makonda alikuwa akiwafariji kwa kuwaambia wasife moyo.

Chanzo: Mwananchi

ccm hakuna jipya, hayo ni ya kawaida, hivi mmesahau kuna kipindi cha mwanasheria chenge walipitisha sheria ya kuhalalisha rushwa iliyoitwa Takrima? je hao wanaoshangaa leo wao sio sehemu ya matokeo hayo? ccm karibu yote imechafuka, inanuka rushwa na uvunjaji wa haki za binadamu

kila apandaye huvuna alichopanda, haitarajiwi upande maovu uvune mema
 
Hivi kuna Vijana wanaojitambua kweli wapo kwenye hili lichama? Du kweli kushabikia CCM inabidi uwe na akili za maiti.
 
ccm hakuna jipya, hayo ni ya kawaida, hivi mmesahau kuna kipindi cha mwanasheria chenge walipitisha sheria ya kuhalalisha rushwa iliyoitwa Takrima? je hao wanaoshangaa leo wao sio sehemu ya matokeo hayo? ccm karibu yote imechafuka, inanuka rushwa na uvunjaji wa haki za binadamu

kila apandaye huvuna alichopanda, haitarajiwi upande maovu uvune mema
sio karibu yote ni yote!
 
Kama kuna vioja duniani basi hili la vijana wa ccm kushangaa kilichotokea ni mmoja ya vioja hivyo, kwa nini wanajifanya hawaoni kile kinachoendelea kwenye taasisi nzima yaani chama kizima hivi wanafikiri chama kinaweza kuharibika halafu wao wakapona kwa misingi gani. Kitu gani kinawafanya wafikiri hivyo. Any way inawezekana maana in tz anything can happen
 
Wote wezi tu, hakuna uchaguzi wowote unaohusisha checheme bila kugubikwa na vitendo vyo rushwa. Nawashangaa wanaUVCCM ambao wanalalamikia rushwa. Kwanza na wenyewe wametoa tu, sema dau lao limekuwa dogo.

Uzoefu unaonesha kuwa hata zile sehemu ambazo wanaCCM hugombea peke yao, bado hutoa rushwa tu!
 
  • MADAI YA RUSHWA YATAWALA,
  • MALISA, SHIGELLA, BASHE, NYALANDU WATUHUMIWA,
  • MAKONDA ATOA KAULI NZITO
MATOKEO ya uchaguzi wa Jumuiya ya Vijana ya Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) yametangazwa jana huku kukiwa na harakati za kuyapinga kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi.

Kati ya mambo yaliyotajwa kupindisha taratibu za uchaguzi huo uliofanyika juzi ni kile kilichoelezwa kuwa ni kutawaliwa na vitendo vya rushwa.

Baada ya Msimamizi wa uchaguzi huo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi kutangaza matokeo, baadhi ya vijana waliyapinga na kuanza kukusanya saini 340 ili kuyapinga.

Katika kuonyesha kutoridhishwa na mchakato mzima wa uchaguzi, baadhi ya wajumbe walibeba mabango yenye ujumbe wa kutokubaliana na matokeo, mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein baada ya kumaliza kufunga mkutano huo.

Moja ya bango hilo lilikuwa na maneno: "Jumuiya si ya Lowassa na wafuasi wake (Benno, Bashe, Zungu, Zabein…..) hivyo jumuiya itakuwa na kambi mbili ya kwanza jukwaani na kambi ya mezani."

Bango jingine lilisomeka: "Jumuiya imara hujengwa na uchaguzi wa haki na siyo rushwa za Bashe, Benno na Zungu."

Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ni miongoni mwa makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 na kambi yake imekuwa ikitajwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

Kwa tafsiri ya mabango hayo, Benno (Malisa) alikuwa Kaimu Mwenyekiti wa UVCCM aliyemaliza muda wake, Bashe (Hussein) naye alikuwa ni Mjumbe wa Baraza Kuu la jumuiya hiyo ambaye amemaliza muda wake
.
Maofisa usalama na walinzi wa jumuiya hiyo ambao walikuwa wakijaribu kuwanyang'anya vijana hao mabango walishindwa, hivyo kulazimika kusubiri dakika kama tano hivi hadi msafara wa Dk Shein ulipoondoka walipowatoa nje ya eneo la ukumbi wa mkutano
.
Tukio hilo lilizua tafrani baada ya walinzi hao kuwanyanyua juujuu vijana wawili kati ya sita waliokuwa na mabango, huku wengine wakionekana kutaka kuwapiga lakini polisi waliingilia kati na kuwatoa nje.

Baadaye polisi waliondoka na vijana watatu katika tukio ambalo lilikuwa likifuatiliwa kwa karibu na baadhi ya wagombea ambao walishindwa katika nafasi mbalimbali za uongozi wa UVCCM.

Vijana walalama

Mapema jana asubuhi, kundi la vijana kutoka mikoa mbalimbali walikutana na waandishi wa habari na kulalamika kwamba rushwa ilitawala huku wakiwatuhumu viongozi wa UVCCM na baadhi ya makada wa chama hicho kwa kuhusika na vitendo hivyo.
Waliotajwa ni pamoja Malisa, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela, Bashe na mtoto wa Lowassa, Fredy.

"Kama Rais Jakaya Kikwete kweli yuko makini na kauli zake ni za dhati, basi atengue matokeo ya uchaguzi huu maana kanuni zimekiukwa na kusema kweli rushwa ilitawala. Atumie nafasi yake kurejesha hadhi ya chama, huu uchaguzi ni batili," alisema Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM kutoka Morogoro, Augustine Matefu.

Walidai kuwa Bashe ndiye aliyekuwa mratibu wa uingizaji wa fedha katika eneo la mkutano ambazo zilitumika kugawanywa kwa wajumbe na kwamba Malisa na Shigela waligawa Sh1 milioni kwa viongozi wa mikoa kama hatua ya kumpigia kampeni mmoja wa wagombea walioshinda.

Kada mwingine, Livamba Adinan Selemani alisema: "Vijana kweli tumempuuza Rais, kweli mtu ambaye hana hela hawezi kupata uongozi UVCCM, kwa maana nyingine nchi yetu inakwenda pabaya. Watu wachache wenye fedha wanaweza kuamua kufanya wanachotaka, hivyo ndivyo uchaguzi wetu wa vijana ulivyokuwa."

Mjumbe mwingine, Kichanta Selemani alisema malalamiko ya viongozi wa UVCCM kuwapendelea baadhi ya wagombea yalifikishwa kwa Lukuvi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Wakati makada hao wa CCM wakizungumza na waandishi wa habari, lilitokea kundi jingine la makada wa chama hicho ambao walianza kuzozana na wenzao wakisema kuwa malalamiko yao yanatokana na kushindwa na kwamba walitaka kutumia: "Viongozi wa ngazi za juu za CCM" kuwachagulia vijana viongozi.

Kundi hilo la pili lilidai kuwa katika uchaguzi huo kundi hilo la kwanza ndilo lililohonga fedha na kumtaja Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu kwamba alikuwa akiwashawishi wajumbe kwa fedha kumchagua mmoja wa wagombea.

Akizungumzia tuhuma hizo, Nyalandu alisema kupitia ujumbe wa simu yake ya mkononi: "Mimi siyo mjumbe wala mgombea na wala sihusiki kwa lolote. Nilikwenda ukumbini na waziri mwenzangu na baadaye tukaondoka pamoja. Hao ni waongo wakubwa na wazushi wachache wanaonunua haki."

Hakuna mtu yeyote niliyeongea naye wala kutoa hela yoyote kwa sababu zozote zile na tulikuwa ukumbini baadaye nje wote pamoja (na waziri). Shame to them who lie (aibu kwao wanaosema uongo) na wataje majina yao tuyasikie."

Alimtaja Waziri aliyekuwa naye kuwa ni Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tzeba kwa lengo la kuwasalimia vijana ambao walikuwa wakiendelea na mkutano wa uchaguzi.

Watuhumiwa wanena

Kwa nyakati tofauti, wakijibu tuhuma hizo watuhumiwa wote walikanusha kuhusika kutoa rushwa na kuwataka wanaolalamika kupeleka ushahidi wao Takukuru na kufikisha malalamiko hayo katika vikao vya ulinzi na maadili vya CCM.

Shigela kwa upande wake, akizungumza na waandishi wa habari alisema kinachotokea sasa kuhusu tuhuma hizo kilitarajiwa kwani ni kawaida watu wanaposhindwa katika uchaguzi kutoa malalamiko hata kama hawana ushahidi wa tuhuma husika.

Shigela alikanusha yeye na Malisa kutoa fedha kwa viongozi wa mikoa akisema kwa nafasi yake asingeweza kupata fursa ya kufanya hivyo kwani alikuwa mratibu mkuu wa uchaguzi kuhakikisha kila jambo linakwenda sawa.

"Kama kuna watu hawakuridhika kuna taratibu za chama inabidi zifuatwe, kwa mujibu wa taratibu zetu kuna siku 14 za malalamiko na hizo mtu anaweza kuzitumia kuandika malalamiko yake na yapelekwe kwa viongozi wahusika ili wachuke hatua," alisema Shigela na kuongeza:

"Vinginevyo taratibu za chama haziruhusu kutoa au kupokea rushwa kwa namna yeyote, kwa hiyo kama mtu anadhani ana uwezo aitumikie jumuiya popote pale alipo kwa sababu wote hatuwezi kuwa viongozi kwa pamoja."

Kwa upande wake, Malisa alisema: "Nimefanya kazi yangu na kutekeleza wajibu wangu kwa ukamilifu, kama kuna jambo lolote ambalo linahusu UVCCM, basi kamuulizeni mwenyekiti wa jumuiya maana yupo."

Bashe alikanusha kuhusika na vitendo vya rushwa na kuwataka wanaotoa madai hayo, kama wana ushahidi waupeleke Takukuru au kufikisha suala hilo katika vikao vya chama hicho.

"Waambieni kwamba wasilete siasa za shule za sekondari UVCCM, maana kama wangeshinda ni dhahiri kwamba wasingelalamika. Ninawapa ushauri wa bure, kwanza kama wana ushahidi wa madai hayo kwamba mimi Hussein nimetoa rushwa, basi wapeleke ushahidi wao Takukuru lakini pia ndani ya chama tunayo Kamati ya Maadili na Usalama wapeleke malalamiko yao huko ili yafanyiwe kazi."

Alisema hawezi kujihusisha na rushwa kwani hata Rais Kikwete katika hotuba ya ufunguzi alikemea vitendo hivyo.

Fredy akizungumza kwa simu alisema: "Tuhuma hizo siyo za kweli kwani mimi licha ya kwamba nilipata barua ya mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo sikuenda Dodoma kutokana na kubanwa na kazi.

"Kwanza mimi si mjumbe wa mkutano mkuu japokuwa ni Katibu wa Uhamasishaji wa Mkoa wa Arusha. Nilipata mwaliko lakini sikuweza kufika huko (Dodoma) nimetingwa na kazi nyingi," alisema.

Matokeo ya uchaguzi

Lukuvi alimtangaza Mbunge wa Donge, Sadifa Juma Khamisi kuwa Mwenyekiti wa UVCCM baada ya kupata kura 483.

Sadifa alimshinda Rashid Simai Msaraka aliyepata kura 263, wakati mgombea mwingine Lulu Msham Abdallah licha ya kujitoa katika kinyang'anyiro hicho muda mfupi kabla ya kura kupigwa, alipata kura nane.

Katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti Mboni Muhita alishinda katika duru ya pili baada ya kupata kura 489 na kumshinda, Paul Makonda aliyepata kura 241.

Katika duru ya kwanza, Mboni alikuwa amepata kura 361 na Makonda kura 206, huku mgombea mwingine Ally Salum Hapi akipata kura 179. Uchaguzi huo ulirudiwa baada ya wagombea wote kutofikisha nusu ya kura kama kanuni zinavyotaka.

"Sheria kushindwa kwa heshima kuliko kushinda kwa fedheha."

Makonda aliyekuwa akizungumza kwa hisia jukwaani alisema ikiwa UVCCM wanataka kujenga taasisi yenye nguvu na inayoaminika, lazima wahakikishe wanajiepusha na vitendo vya rushwa ambavyo vinaua demokrasia.

"Uchaguzi tulioufanya hatukumchagua Sadifa wala Mboni, bali tumechagua uongozi wa aina ya jumuiya tunayoitaka, sasa tutarajie jumuiya hiyo…. kama sikueleweka historia itakuja kutuambia maana ya maneno haya," alisema Makonda na kuongeza:

"Kama kuna mtoto wa maskini, mtoto wa mkulima kama mimi amechagua au kupiga kura yake kwa sababu ya rushwa, basi ajue amepanda mbegu maishani mwake."

Baada ya Makonda kutoa kauli hizo alishuka jukwaani na kwenda moja kwa moja nje ya ukumbi ambako baadhi ya wapambe wake walimfuata na kuanza kulia machozi.

Baadhi yao walisikika wakisema kwamba UVCCM wameisaliti demokrasia kutokana na nguvu ya fedha. Hata hivyo, Makonda alikuwa akiwafariji kwa kuwaambia wasife moyo.

Chanzo: Mwananchi
Kama Chama kimefikia hatua hii, sasa kumbe si Wanawake tu wanashangaza katika nao kutumia rushwa sasa hata vijana ambao tunategemea tunawaandaa kuwa viongozi wa taifa hili wanatumia rushwa. Kwa matazamo wangu, WANAWAKE NA VIJANA wametumiwa na VIGOGO kufanya yote haya, kumbe bado rushwa hiyo imesababishwa na watu wengine. Kauli ya Mwenyekiti wa CCM kuwashangaa wanawake nao katika rushwa ina rudi tena kwa hao vigogo ambao wamesababisha haya yote. Imefikia wakati sasa kuona kuwa kama kweli CCM na Taasisi zake zinaandaa rais wa 2015 kwa kutumia chaguzi hizi, basi watakuwa na kazi sana kumpata mgombea. Ombi kwa vyma vya upinzani, tumieni hali hii ambayo imejitokeza katika chaguzi hizi za ccm kwaanda wananchi kukabiliana na hili katika uchaguzi wa 2015. Tumieni udhaifu huu uliojitokeza kama agenda kuhamasisha wananchi kufungua macho na kuona kuwa sasa pesa inaatumika kununua uongozi, wajiandae kwa hali hii na kujiandaa kuzichukua hizo pesa lakini wajiandae pia kuwapa maumivu watakaotoa pesa hizo kwa kuwanyima kra na kula. Tumeshachoka na uozo wa aina hii, unanunua uongozi ili kulifanyia nini taifa hili? Ningekuwa mimi mgombea wa urais kupitia ccm 2015, ningesubiri uchaguzi, nikishachaguliwa ningekifuta chama na kuanzisha kingine ili kuleta matumaii mapya kwa walionichagua.
 
Mmevuna mlichopanda! "Pasipo busara ushindi huenda kwa Mjinga" kulalamika tu haitoshi na uchaguzi ndio tayari umeshafanyika! "TAFAKARI CHUKUA HATUA"
 
Vijana ambao hawakuridhika wasilalamike bali wajipange kimyakimya kisha 2015 wachukuwe hatua kwani Ccm hii ya JK inalengoLA KUMFUTA JASHO LOWASA kwa kukubali kujiuzuru ili awalinde wenzake.
 
Back
Top Bottom