UVCCM Kufanya Mandamano August 31

UVCCM Kufanya Mandamano August 31

Hii ni janja ya nyani. Hapo Polisi watakachofanya ni kuzuia maandamano ya UVCCM ili wapate kisingizio cha kuzuia UKUTA.
 
Ndokusema Maandamano YANARUHUSIWA

Inawezekana kabisa serikali haitaki kusema openly maandamano kwa UKAWA yameruhusiwa, ili ku- cushion hii hali, wamewatanguliza vijana wao kuonesha kwamba hawana tatizo na maandamano ya amani, ila kwa UKAWA kama watafanya fujo watathibitiwa vikali
 
Si maandamano ya vyama vya kisiasa yamezuiliwa...au wanaenda kuandamana kenya.
 
Hawa madogo wafanye kazi maandamano marufuku hadi boss mkuu ayaruhusu. Police vunja ngongoti hizo barabarani tuone uthubutu wenu.
 
Pagumu kutofautisha umuhimu ,uharaka wa maandamano ya upande mmoja,na kuwakebehi,kuwatishia mkongoto mzito kwa wale damu ya kunguni tena walitoa notice ya mwezi mzima kufanya maadamano.

Serikali iache visingizio kwanini isitangaze kuwa wanafuta mfumo wa vyama vingi tunarudia kule chama kimmoja kushika hatamu ya uongozi period?
 
haya wale waliokuwa wanapinga maandamano wajitokeze sasa kuwapinga hao madogo...
 
UVCCM ni mapoyoyo kabisa hamna kitu, yaani bure kabisa, halafu wanapata wapi Legal authority ya kutangaza kitu ambacho kimeshapigiwa marufuku niliwaona hata kipindi kile kule Dodoma, na nyinyi wakuu sijui walezi wa UVCCM hebu tengenezeni watu wenye weledi bana, hivi JPM anyetutembeza kifua mbele sasa hivi akiondoka itakuwaje, mbona mnafuga mapoyoyo na mazombi.
 
Yaani ni mambo ya kitoto tena ya kizamani! Nafikiiri hata watoto wa siku hizi hawawezi kucheza michezo kama inayochezwa na CCM na serikali yake
 
Wana haki kikatiba, ili mradi tu wasituvurugie haki yetu ya kikatiba ya tar.Mosi Septemba! Polisi tafadhali kuwe na FAIR PLAY kwa siku zote mbili (31/08 na 01/09/2016)
 
Hapa inatafutwa sababu ya kupiga marufuku UKUTA au wanataka kuharalisha kichapo!!? Maana maandalizi yanayoendelea siyo bure!!
 
Wakuu uvccm wametangaza kufanya maandamano august 31 ili kuwaeleza wananchi kuridhishwa kwao na utendaji kazi wa raisi magufuli.jeshi la polisi lilipiga marufuku maandamano ya kisiasa hata mbowe alipotangaza maandamano ya CHADEMA kuanzia sept 1 nchi nzima aliitwa kwa mohojiano.nategemea jeshi letu tukufu la polisi litawaita UVCCM kwa mohojiano maana wanataka kuharibu amani na utulivu wa nchi yetu

Jeshi la polisi ni kitengo ndani ya ccm hivyo hawana wanaloweza kufanya dhidi ya ccm. Kumbuka wote wanafanya kazi kuhakikisha matumbo yao yanajaa hivyo hakuna hata mmoja anayeweza kuhoji tamko lolote la ccm. Wao hawafuati katiba na sheria zinasemaje wanasubiri waambiwe nini wafanye na ccm. Kwa hiyo kutarajia jeshi la polisi kuhoji chochote kinachofanywa na ccm ni kupoteza muda wako. Huko kwenye jeshi la polisi unapanda cheo ama kupata nafasi ya ulaji kwa kuwa ndio mzee na si vinginevyo. Katika mazingira kama haya unategemea nini?
 
Nionavyo mimi, huenda kuna hidden agenda katika hili na hasa hasa kama CHADEMA hawajawasilisha barua yao ya kuomba kibali cha maandamo.

Hapa jibu litakalotoka kwa polisi litakuwa na madhara kwa CHADEMA. Hata hivyo, mpango huu utakuwa umeshafeli na utawanufaisha zaidi CHADEMA kama wameshawasilisha maombi kimaandishi kwani itawabidi polisi watoe kibali kwa wa kwanza huyu wa pili asubiri. Government works on paper!
 
Ndugu zangu fungukeni bongo zenu, hii ni tracking, Magufulu akae chonjo sana na hii kitu UVCCM.

Lowasa si mdogo kma mnavomdhania, km kweli wanataka kumpongeza wafanye october 1.
 
Back
Top Bottom