UVCCM Kufanya Mandamano August 31

UVCCM Kufanya Mandamano August 31

Jeshi lipo madhubuti kudhibiti ujinga wowote utakao jitokeza.
G.jpg
 
nimemsikia Shaka kupitia azam tv anasema wameshatoa taarifa polisi kuomba ulinzi na endapo polisi watayakataa maombi yao kwa sababu yoyote ile basi wao wataangalia namna ya kujilinda wenyewe
 
Naona mmesikia UVCCM na wao wanaandamana
Mmeanza kutokwa povu.

Haaa haaaaa

Ngoma inogire.

Nasikia UVCCM wanaandamana siku tatu mfululizo
Kumuunga mkono rais mzalendo magufuli.

Tulien wana UKUTA
Mlitaka muandamane peke yenu?

Badala ya kushangilia kundi jingine limepatikana la kuandamana
naona mnatokwa povu
 
Watu hawataki kufanya kazi....!!!

M/Kiti wa CCM taifa awe makini vijana watamvurugia. Mimi nilitegemea vijana wa UVCCM sasa waonyeshe njia kwa kufanya kazi kwa kuanzisha miradi mbali mbali ya kuwaletea maendeleo watanzania, kwa kutumia vitegauchumi walivyonavyo wawasaidia vijana kupata mitaji nk. Wawatembelee vijana kwenye maeneo yao wakusanye kero za vijana na kuziwasilisha kwa sekeretarieti ya chama na kisha afikishiwe mwenyekiti wa Chama taifa. ndiyo maana nasema UVCCM nayo inatikiwa kufumuliwa. Kama ni kweli wanataka kufanya hivyo eti kuandamana kumuunga mkono Rais...na sema watakuwa hawafai. Rais ninayemjua hataki kuungwa mkono kwa staili ya maandamano. Wajiangalie hao viongozi wa UVCCM.
Wewe nawe jiongeze hakuna cha maandamano hapo hiyo danganya toto hiyo trick ishapangwa wajifanye wanataka kuandamana afu police wawazuie then police wazuie na ya UKUTA kwa kisingizio kua mbona ya uvccm wamezuiwa na wametii, huo ni utoto wanachotaka kufanya uvccm
 
UVCCM waitisha maandamano Agosti 31

Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imepanga kuitisha maandamano nchini nzima Agosti 31 mwaka huu yenye lengo kumpongeza Rais John Magufuli kutokana utendaji kazi tangu aingie madarakani.

Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka alisema maandamano hayo ni ya amani tofauti na vyama vingine na tayari wameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya ulinzi.

Soma zaidi:UVCCM waitisha maandamano Agosti 31
 
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imepanga kuitisha maandamano nchini nzima Agosti 31 mwaka huu yenye lengo kumpongeza Rais John Magufuli kutokana utendaji kazi tangu aingie madarakani.

Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka alisema maandamano hayo ni ya amani tofauti na vyama vingine na tayari wameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya ulinzi.

Alisema Rais Magufuli amefanya mambo mengi katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani hivyo hawana budi kumpongeza kwa njia ya maandamo ili kufikisha ujumbe kwa wananchi waliomchagua.

My Take: Hii ni kwa ajili wakinyimwa waseme ya UKUTA nayo yasitishwe. Mchezo huu hauitaji hasira poleni

Ninaomba sana maandamano haya yaruhusiwe ili wavuliwe nguo vizuri hadhari kwenye operesheni UKUTA. Watanatoa agenda za kumalizwa, wajinga kweli.

By the way, UVCCM wako wangapi Tanzania? H ahahahahaaaaaaaaaaaaaaaa!.

Mwisho wa wenye mwili umefika!
 
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) imepanga kuitisha maandamano nchini nzima Agosti 31 mwaka huu yenye lengo kumpongeza Rais John Magufuli kutokana utendaji kazi tangu aingie madarakani.

Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka alisema maandamano hayo ni ya amani tofauti na vyama vingine na tayari wameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya ulinzi.

Alisema Rais Magufuli amefanya mambo mengi katika kipindi kifupi alichokuwa madarakani hivyo hawana budi kumpongeza kwa njia ya maandamo ili kufikisha ujumbe kwa wananchi waliomchagua.

My Take: Hii ni kwa ajili wakinyimwa waseme ya UKUTA nayo yasitishwe. Mchezo huu hauitaji hasira poleni
My take is here...UVCCM ni mtego kwa CHADEMA kwakuwa wanafahamu hawatapewa kibali au ruhusa na Jeshi la Polisi hivyo Police wataendelea na msisitizo wao kuwa hata UVCCM tumewanyima kibali hivyo na nyinyi hamna ruhusa ya kufanya hivyo!!Kwa sababu ukiangalia UVCCM hawakuwa na maandalizi yoyote ya kuwa na maandamano!
 
Naona wanajipendekeza kwa "MTUKUFU" hawa vijana wa UVCCM njaa zinawasumbua hakuna kimya hayo maandamano wakaandamane huko lumumba.
Haa haaaa
Wakiandamana CCM ni njaa
na wakaandamanie LUMUMBA.

Hahaha
Wakiandamana UKAWA
Ni uzalendo.

Ngoma inogire
 
Hapo kuna mchezo wa kijanja unafanywa ili kuwahadaa UKUTA , issue imekaa hivi hao vijana wa CCM wanaandaa maandamano Feki wataomba kibali cha polis Kisha siku ya mwisho polis watazuga kukataa , Kisha waje na sababu kuwa wameona kuna uvunjifu wa Amani sasa wanazuia maandamano ya vyama vyote yaani CCM na Ukawa ili kuwaonyesha wananchi kuwa wao hawana upendeleo , hiyo mbinu ya umoja wa vijana imeshitukiwa mapema .
 
Waandamane wasiandamane, tarehe 1 Septemba UKUTA iko pale pale. Kamwe hatutarudi nyuma. Tumegundua huyu dereva uchwara gari yetu anaipeleka Zimbabwe hivyo tunataka kuirudisha Tanzania kabla haijavuka mpaka wa Zambia.
Mbona mnaweweseka sana.
Ss na nyie mtaandamana tu ile tarehe moja.

Sasa waachin na wenzenu waandamane hio tarehe 31 agost
 
Haa haaaa
Wakiandamana CCM ni njaa
na wakaandamanie LUMUMBA.

Hahaha
Wakiandamana UKAWA
Ni uzalendo.

Ngoma inogire
Maandamano ya CCM ni feki ni mbinu ya kuwahadaa Ukawa
 
Wakuu naomba kuuliza,

Hivi wanachama wa CCM haya maneno huwa yanawachanganya kwa hawaelewi maaana ya au wanayatafsiri tofauti na maana ilivyo

1. Maandamano
2. Amani
3. Utulivu
4. Kukosoa/kupongeza/kusifia serikali
5. Chama cha siasa
6. Mikutano
7. Katiba

Ni kwamba huwa wana maana tofauti na inayojulikana na wengi au ni Hofu inayowafanya kuchukulia kinachofanywa na Vyama vya upinzani ni Vurugu.
Maandamano ya amani ya UVCCM yako palepale agost 31.
Tujitokeze kwa wingi nchi nzima
 
Kwa ufupi
  • Kaimu Katibu Mkuu wa jumuiya hiyo, Shaka Hamdu Shaka alisema maandamano hayo ni ya amani tofauti na vyama vingine na tayari wameshatoa taarifa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya ulinzi.Eti niyakumpongeza mh.Magu kwa kazi nzuri anayoifanya tangu achaguliwe.
  • Kuamkia kesho yake ni UKUTA ambapo polisi tayari wanafanya mazoezi kwa ajili yao, Vip hii imekaaje wakuu
 
Maandamano ya CCM ni feki ni mbinu ya kuwahadaa Ukawa
Hahahha.

Yapi orijino
mkuu
n umetumia kipimo gan.
?

Kuandamana ukawa wamesema n haki ya kila mtu
Waachen bhana UVCCM

hahahha
 
Back
Top Bottom