Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,848
- 15,252
Kumekuwa na ongezeko kubwa mtaani la uuzwaji wa dawa za mitishamba, dawa hizo hazina vipimo maalumu na wala haijulikani ni aina gani ya miti.
Mfano mzuri unakuta mmasai ameweka dawa kwenye galoni moja huku amebeba karatasi maalumu yenye aina za magonjwa karibu 200 ambayo yanatibika na dawa iliyopo kwenye galoni.
Dawa moja tu utaambiwa inatibu magonjwa kama vile presha, kusafisha damu,Kichwa, UTI. Uvimbe, malaria. Homa ya matumbo fungus, kisukari, tambazi. Ini nk
Ongezeka la dawa hizo zimekuwa kila mahala hadi kufikia wengine kufungua maduka ya dawa za asili lakini ukifuatilia wengi wa waliotibiwa kupitia dawa zao hawakupona wala kupata nafuu.
Serikali nayo imekuwa kimya ikiwaacha wananchi kufanya chochote bila uthibiti maalumu wa kuwaokoa raia wake. Badala ya dawa hizo kwenda kutibu tatizo inaenda kuanzisha tatizo lingine.
Huko instagram nako kumegeuka serikali nyingine maana wasomi na wasio wasomi wanatafuta namna ya kuishi kwa kuuza dawa za kila aina ambazo hawana hata ujuzi nazo wao ni ilimradi pesa imeingia mfukoni wewe mgonjwa utajijua mwenyewe mbele ya safari.