kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 12,318
- 12,622
Mgongo ni kiungo muhimu sana kwa afya ya kiumbe akiwemo binadamu kilichotengenezwa kwa pingili za mifupa yenye tundu katikati zilizounganishwa kwa misuli maalumu inayonesa iitwayo ligament.
Mgongo una kazi muhimu sana kama vile kushikilia viungo vingine kama manya, mbavu, fuvu la kichwa, mafigo. mifupa ya uti wa mgongo hulinda uti wa mgongo, maji (CSF) ya uti wa mgongo, na kupitisha mishipa ya fahamu (nerves) kwenda kwenye viungo vingine vya mwili. Uti wa mgongo unaunganika na ubongo moja kwa moja na waji ya uti wa mgongo yanazunguuka kutoka kwenye uti wa mgongo hadi kwenye ubongo kichwani. Uti wa mgongo unaupatia mwili balance wakati wa kutembea, kuinama na kubeba mizigo.
Uti wa mgongo hua unaathiriwa sana na kubeba mizigo mizito zaidi ya 20Kg, kuinama kila wakati, ajali na magonjwa kama ya kifua kikuu (TB ya mifupa), homa ya uti wa mgongo na magongwa ya fungus na virusi.
Lakini, mizigo ndiyo inayoongoza kwa shida za migongo. Kuna vijana wengi wanazunguunga na mizigo mikubwa ya biashara mitaani kutwa nzima hasa biashara za maji ya chupa, na matunda vichwani; na madeli ya ice-cream migongoni mwao. Nimefanya kautafiti kadogo ka watu hawa, nikagundua kuwa wengi wao wanaugua shida za migongo. Kati ya watu hawa wenye shida ya migongo wengi wao ni wale wanaobeba mabegi ya ice-cream migongoni na kifuani.
Elimu itolewe kuhusu aina hii hatari ya biashara kwa vijana wetu ambao bado wana kesho nyingi sana. Na ikiwezekana wawe na bima na wasibebe mizingo inayozidi 5Kg mgongoni.