Uuzaji na unywaji ''viroba'' marufuku Arusha

Kuongea ni rahisi sana kuliko utekezaji
 
Kwani kiroba kina shida gani,mbona kinywaji hichohicho kikiwa kwenye chupa hao hao wakubwa wakinywa?Acheni hizo bana!
 
Sasa
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.

Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.

Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe.

Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa makini suala hili.”

Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na ofisi za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za vikao.

Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.
katumia mamlaka yapi kikatiba?????... Hao wenye biashara yao wakimshtaki itakuwaje??... I guess wanalipa kodi kihalali na hawana mipaka ya maeneo,muda au mikoa ya kufanya biashara zao..... Naomba maelekezo tafadhali
 
AMECHANGANYIKIWA HUYO.! UNAPOTOA AMRI AMBAYO HUNA MAMLAKA NAYO HATA MAMLAKA YA BAHATI MBAYA TU NI UWENDAWAZIMU.!
 
nenda shule wewe hata hamlingani, hebu na wewe toa amri uone kama itajadiliwa humu
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.

Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.

Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe.

Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa makini suala hili.”

Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na ofisi za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za vikao.

Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.

Nauliza:
1.Viroba ni Biashara haramu au halali?
2.Kama halali,je kuna mamlaka yeyote anapewa RC kupiga marufuku biashara halali katika mkoa wake?
3.Je wenye biashara hawawezi kumfungulia mashitaka ya kuwahujumu ktk biashara yao?
4.Hizi kampuni zinalipa kodi au lah?
5.Kama zinalipa kodi na MaRC wote wakapiga marufuku ktk mikoa yao itakuwaje?
6.Je ni hatua gani kali za kisheria atachukuliwa yule ambaye atakiuka agizo hilo?
7.Je akishinda kesi na kudai fidia,nani atalipa?
8.Je hii ni sera nzuri kwa wawekezaji?
 
bora amesema mpate cha kuandika
 
Huu ni ukurupukaji wa hali ya juu, kama viroba vina hitilafu kiafya kuna mamlaka zenye nguvu ya kufunga uzalishaji na usambazaji na sio mkuu wa mkoa.

Kazi ya mkuu wa mkoa na kuhakikisha sheria za nchi zinafuatwa hasa ile inayokataza uuzaji na utumiaji wa vilevi muda wa kazi. Kama ameshindwa hilo asifungie biashara halali za watu. Kama ni issue ya mazingira weka strict measures kwa yeyote atakayekutwa anachafua kwa karatasi za viroba.

Hao jamaa wakiamua kumfungulia mashitaka kwa kuharibu biashara yao halali.serikali isiwajibike kumlipia fine hiyo maana sio kazi aliyetumwa.
 
RC wa Arusha apigane na madawa ya kulevya, apigane na mirungi, bangi, gongo etc. Muda kufungua na kufunga bar unajulikana pambana na wamiliki wake wazingatie muda.

Pambana na makahaba na mashoga wanaoeneza ukimwi mbaya kuliko viroba.

Kubwa zaidi toa elimu juu ya ujasiriamali kwa vijana na toa elimu ya athari za ulevi hilo litakuwa soluhisho na sio marufuku. Ukitaka kuona marufuku yako haitatekelezwa fuatilia suala la madawa ya kulevya. Kitu kikiharamishwa inakuwa lucrative busiiness
 
Hii itasaidia kuokoa kizazi cha Kazi cha vijana. Najua bado watakunywa ila itakuwa kwa kujificha ficha angalau spidi itapungua. Ile kitu ni gongo live kabisa
 
Napinga amri ya mkuu wa mkoa.Haya ni maamuzi ya kisiasa ambaya hayajafanyiwa utafiti wowote.Upigaji marufuku wa biashara ya ukahaba na unywaji wa madawa ya kulevya haujasaidia chochote katika kupunguza haya matatizo bali kuyachochea tu.Kabla ya mwaka 1933 Marekani ilikuwa ina sheria inayopiga marufuku unywaji wa pombe ila ikafutwa baada ya kuoneka kuwa inazidi kuchochea ulevi na uhalifu.

Madhara ya kupiga marufuku viroba yanaweza kuwa yafuatayo
1.Kushamiri kwa biashara ya magendo ya viroba
2.Kushamiri kwa uhalifu unahohusiana na biashara ya magendo ya vilevi
3.Kuingizwa sokoni kwa pombe haramu zisizo na viwango
4.Kushamiri kwa dawa za kulevya.
5.Kuongezeka kwa unyaji wa viroba.
6.Watu kuvunja sheria ili kupata viroba.
7.Kupoteza chanzo cha kodi na ajira kwa watu

Kwa kifupi upigaji marufuku wa viroba unaweza kuzua matatizo mengine na bila kuongeza nguvu kazi yoyote iliyotarajiwa.Tunahaja ya kufanya utafiti kabla ya kukurupuka.Ni vema watu wangeelimishwa madhara ya viroba na wakaaachwa wafanye maamuzi ya kunywa ama kuacha wenyewe ili maradi tu hawavunji sheria zingine za nchi.

Kuna baadhi ya nchi zinafikiria kuruhusu biashara ya ukahaba na ata uvutaji bange ili kupunguza haya masuala.
 
Hawa watu wanatusumbua mpaka kwenye 'distribution channel'
Watu wa biashara ya jumla wamewekeza kwenye maviroba, na inashuka chini mpaka katika Retail.
Pombe haipaswi kuuzwa kupitia channel hii ya biashara, lakini Mabwana biashara wamelala wanasubiriki kukatia watu leseni ...basss ! fankuroo !
Counter- Rombo.JPG
 
Napinga amri ya mkuu wa mkoa.Haya ni maamuzi ya kisiasa ambaya hayajafanyiwa utafiti wowote.Upigaji marufuku wa biashara ya ukahaba na unywaji wa madawa ya kulevya haujasaidia chochote katika kupunguza haya matatizo bali kuyachochea tu.Kabla ya mwaka 1933 Marekani ilikuwa ina sheria inayopiga marufuku unywaji wa pombe ila ikafutwa baada ya kuoneka kuwa inazidi kuchochea ulevi na uhalifu.

Madhara ya kupiga marufuku viroba yanaweza kuwa yafuatayo
1.Kushamiri kwa biashara ya magendo ya viroba
2.Kushamiri kwa uhalifu unahohusiana na biashara ya magendo ya vilevi
3.Kuingizwa sokoni kwa pombe haramu zisizo na viwango
4.Kushamiri kwa dawa za kulevya.
5.Kuongezeka kwa unyaji wa viroba.
6.Watu kuvunja sheria ili kupata viroba.
7.Kupoteza chanzo cha kodi na ajira kwa watu

Kwa kifupi upigaji marufuku wa viroba unaweza kuzua matatizo mengine na bila kuongeza nguvu kazi yoyote iliyotarajiwa.Tunahaja ya kufanya utafiti kabla ya kukurupuka.Ni vema watu wangeelimishwa madhara ya viroba na wakaaachwa wafanye maamuzi ya kunywa ama kuacha wenyewe ili maradi tu hawavunji sheria zingine za nchi.

Kuna baadhi ya nchi zinafikiria kuruhusu biashara ya ukahaba na ata uvutaji bange ili kupunguza haya masuala.
....hicho kinachopigwa marufuku na chenyewe kimeshamiri, sasa sijui unaandika upumbavu gani !? mzee74
People !.png
 
Hujanisoma.Ndio kimeshamiri.Ila usidhani kitapungua kwa sababu kimepigwa "ban".Haya ni maamuzi ya kisiasa tu kutafuta kick binafsi.
....kwahiyo ulitaka wapewe chachandu na malapu lapu ili wa-enjoy vizuri !?, kitu kilichopigwa marufuku kinazidi vipi wakati viwanda vinajulikana ?
Hii biashara ya kijinga imevuruga mpaka channel ya distribution, Wauza jumla badala kuweka stock ya unga na bidhaa za maana wao wanajaza makatoni ya viroba .... ujinga kabisaa
 
Back
Top Bottom