Uuzaji na unywaji ''viroba'' marufuku Arusha

Uuzaji na unywaji ''viroba'' marufuku Arusha

dawa ya hivi viwanda sio kuvuifunga......
watoze kubwa kubwaaaaa sanaaaaaa na kuwabana sokoni wasiongeze bei,.watafilisika au kubadili biashara wenyewe..............
pamoja na kutozwa kodi kubwa pia vikaguliwe material zinazotumika kutengeneza kinywaji hicho
 
Ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe aina ya viroba mkoani Arusha.

==Chanzo: Gazeti la Nipashe.

Sijui kama hili litawezekana kwa hawa vijana wa ''people's'' nadhani watakimbilia Moshi ama wataandamana kupinga.
Huyu mkuu Wa mkoa sio Mzima .unatangaza kufungia kiwanda cha viroba .wakati kipo kisheria .tena mbaya zaidi kiwanda cha viroba kipo ARUSHA .huyu anatafuta kufunguliwa kesi ya madai na kiwanda cha viroba.tusubiri tuone
 
hawa watu wana leseni na kodi wanalipa inakuaje anakuja mtu kutoa tamko kama ilo kwa nini asifate sheria maana haya mambo si ya kukurupuka tuu.viroba vina madhara sana sema wakae wajue watamaliza vipi..
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.

Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.

Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe.

Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa makini suala hili.”

Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na ofisi za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za vikao.

Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.
 
Mkuu wa mkoa hujaona lile onyesho la ngono lililodhaminiwa na hao wenye kiwanda cha viroba hapo arusha?Njia rahisi ni kuongeza kodi iwe kubwa katika hivyo vinywaji au kufunga viwanda vyake kabisa.Tumeshindwa kupiga matufuku matumizi ya mifuko ya plastic sijui kama hilo tutaweza
 
Huyu mkuu Wa mkoa sio Mzima .unatangaza kufungia kiwanda cha viroba .wakati kipo kisheria .tena mbaya zaidi kiwanda cha viroba kipo ARUSHA .huyu anatafuta kufunguliwa kesi ya madai na kiwanda cha viroba.tusubiri tuone
andamaneni mpinge kama kawaida yenu, inawezekana hilo agizo likawa kama kuitangaza biashara hiyo. Leo nadhani mauzo yake yatapanda.
 
Wakisema hivyo wapige marufuku na uvutaji sigara, pia asisahau kodi ya walevi ndo inaendesha nchi hii ndo maana kila bajeti wanaoandisha bei ya bia
 
Hapo ndio naona viongoz w9engine hawapo ktk uongoz au hawakustahili kupewa uongoz kwanza viroba vimekuwa vikisababisha malipo hewa au ni nn...kwanza hicho kiwanda kinalipa kodi kama sio wakifungie ili uzalishaji usiwepo tena hila sidhan kama inahusisha na serikali wakat mtu ananunua serikali inapata kodi
 
Mkuu wa mkoa kavurugwa viroba ni biashara halali na kodi wanalipa aache kukurupuka kwanin aspige marufuku whisky
hata mi nashindwa kumuelewa, huyu mkuu nazani akili ya viroba inampeleka puta!

Jigo
 
Mpango huo ni wa mda mrefu au ni kwa sababu tu ya slogan ya "Hapa kazi tu"? Na kama ni wa mda mrefu ni nini hatma ya secta ya uchumi Tz ambayo pombe ni miongoni mwa bidhaa iongezayo pato kubwa kwa taifa? Pia je wanaotakiwa kupigwa marufuku ni watumiaji au watengenezaji(viwanda)? Na kwanini usiwe mpango nchi?
 
Kuber zimepotea mitaani,hata viroba inawezekana kuvipoteza mitaani
 
Nina wasiwasi na upeo wa mleta mda pamoja na source yake....
Arusha hatuwezi kutawaliwa na maneno ya makada ambao wanatafuta KIKI
 
Ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha amepiga marufuku uuzaji na unywaji wa pombe aina ya viroba mkoani Arusha.

==Chanzo: Gazeti la Nipashe.

Sijui kama hili litawezekana kwa hawa vijana wa ''people's'' nadhani watakimbilia Moshi ama wataandamana kupinga.

========

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi aina ya kiroba katika mkoa huo.

Alisema uamuzi huo unatokana na vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa kushindwa kufanya kazi na kulewa wakati wa kazi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema anafanyia kazi sakata la mkazi wa Kata ya Ngarenaro anayedaiwa kujihusisha na uuzaji na uingizaji wa dawa za kulevya ambaye baada ya kukamatwa na polisi aliachiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Ntibenda alisema hayo jana Arusha wakati akizungumza na watendaji wa serikali za mitaa 154, maofisa watendaji kata 25 pamoja na wenyeviti wa serikali za mitaa.

Alisema suala la kilevi aina ya kiroba ni kero kwa vijana kufanya kazi wakiwa wamelewa au kuwa navyo mifukoni hasa madereva wa pikipiki, daladala na wapiga debe.

Alisema kutokana na vijana kunywa kinywaji hicho nyakati za kazi, amepiga marufuku uuzwaji wa kilevi hicho, atakayekiuka agizo hilo hatua za kisheria zitachukuliwa.

“Sitaki kuona viroba vikiuzwa katika Mkoa wa Arusha na atakayekiuka nitamchukulia hatua za kisheria, lakini huyu anayeuza dawa za kulevya halafu polisi wanamwachia na wananchi hawajui kwanini anaachiwa huku akiendelea kuuza dawa, sasa nasema mwisho wake umefika, nitafuatilia kwa makini suala hili.”

Baadhi ya wenyeviti wa serikali za mitaa walihoji sababu za kutokuwa na ofisi za kufanyia kazi badala yake wanalazimika kutumia nyumba zao au kukodisha ofisi ili kufanya kazi za jamii lakini pia hawana posho za vikao.

Wenyeviti hao akiwemo Amani Mwakalinga wa mtaa wa Darajani na Hilary Mkonyi wa mtaa wa Ngarenaro, walisema awali Mkurugenzi wa Jiji, Juma Idd aliahidi kuwajengea ofisi lakini hadi sasa hakuna utekelezaji.
Tatizo la hili tamko ni kuwa kiroba ni bidhaa halali, kuna vibali na leseni zote za kiserikali kuzalisha na kuuza sokoni. Bidhaa hii pia hulipiwa kodi zote za serikali kama bidhaa halali kabisa.
Hapa mkuu wa mkoa kateleza na kavunja sheria.

Huwezi piga marufuku bidhaa halali kwa sababu alizotoa.
Kwani hata bia, whisky na wine zikinywewa kupita kiwango ni janga kubwa vile vile.
Kuna bidhaa nyingine kama sigara ni bidhaa hatari ba yenye madhara mengi duniani kote lakini haijapigwa marufuku.

Kupiga marufuku viroba kunahitaji mchakato tofauti na hilo tamko la boss. Ndo maana halisi ya utawala wa sheria unapokuja.
 
Hajapiga marufuku uuzwaji wa viroba bali uuzwaji wa viroba kwenye maduka
 
Tokea Monaban apigwe chini, sirluta amepoteza uwezo wa kujenga hoja ..
kampuni inayotengeza viroba haipo kisheria? haijasajiliwa? hailipi kodi? sasa ukipiga marufuku ghafla kwa sababu za kisiasa utawarudishia gharama za uwekezaji? utawalipa fidia? Magufuli alitoa wapi wakuu wa mikoa (tena mkoa mkubwa kama Chuga) wa aina hii??
 
weka kodi kubwa kwa kiroba ili kiuzwe kwa bei kubwa ambayo itafanya iwe ngumu kukipata vinginevyo ile ni biashara halali inakibali na inalipiwa kodi halali tena wenye kiwanda wanaweza kushitaki kwa kuvurugiwa biashara yao ,nadhani ingekusaidia kuliko kutoa katazo vipi mtu akitoka navyo Dar,Kilimanjaro,Tanga,au Pwani akaja kunywea Arusha utajuaje kama kanunua Arusha au alikotoka?
 
Back
Top Bottom