Uungwana: Kimbe akabidhi ofisi ya umeya Iringa, Mkurugenzi wa manispaa ampongeza na kusema ni kiongozi makini aliyewajali wananchi

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,879
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa leo amekabidhi ofisi na gari mbele ya mkurugenzi wa manispaa hiyo na watumishi wote wa manispaa.

Kimbe amesema ameachia madaraka ya umeya kwa moyo mweupe ili vikao vya baraza la madiwani viendelee kufanyika na wananchi kupatiwa maendeleo. Kimbe amewataka watumishi wa Manispaa kutosikitika kwa yaliyotokea na badala yake waendelee kuchapa kazi kwa bidii.

Mkurugenzi wa Manispaa amesema wamesikitika sana kumpoteza Meya mwenye maono na aliyekuwa mchapa kazi haswa. Mkurugenzi amesema wataendelea kuifanyia kazi na kuikamilisha mipango yote makini iliyoachwa na Kimbe.

Source Eatv habari!

My take; Kama Kimbe ni mchapa kazi kwanini mmemtumbua?!!
 
Wakati mwingine ukitizama yanayotokea hapa duniani, unashindwa kuutetea uwepo wa Mungu.
 
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa leo amekabidhi ofisi na gari mbele ya mkurugenzi wa manispaa hiyo na watumishi wote wa manispaa.

Kimbe amesema ameachia madaraka ya umeya kwa moyo mweupe ili vikao vya baraza la madiwani viendelee kufanyika na wananchi kupatiwa maendeleo. Kimbe amewataka watumishi wa Manispaa kutosikitika kwa yaliyotokea na badala yake waendelee kuchapa kazi kwa bidii.

Mkurugenzi wa Manispaa amesema wamesikitika sana kumpoteza Meya mwenye maono na aliyekuwa mchapa kazi haswa. Mkurugenzi amesema wataendelea kuifanyia kazi na kuikamilisha mipango yote makini iliyoachwa na Kimbe.

Source Eatv habari!

My take; Kama Kimbe ni mchapa kazi kwanini mmemtumbua?!!

Katika Tunu zote zilizopo Tanzania kuna hii Moja ya Unafiki Uliotukuka ndani ya Mioyo ya Watanzania huwa inasahaulika sana tu.
 
..Meya amesema hajaondolewa kwa kufuata sheria.

..amebainisha kuwa wajumbe wa mkutano walikuwa 26 na walihitajika wajumbe 17 au zaidi kumuondoa, lakini waliopiga kura kumuondoa walikuwa 14.

..Meya ameendelea kusisitiza kuwa serikali haikupenda kuona Manispaa ya Iringa inaongozwa na CDM hivyo imetumia mabavu kumuondoa.

Cc shungurui
 
nchi ya inafanya mambo ya aibu na kushangaza sana,tutamkumbuka jaji warioba pale alipotaka mtawala apunguziwe madaraka kwenye katiba mpya,pengine watanzania wanapaswa kudai katiba mpya kwa nguvu vingenevo mtaumizwa kila kukicha na watawala wababe,mambo kama haya yanavunja moyo watu kuwa wazalendo kuchangia maendeleo,hakuna mwekezaji ambaye yuko tayari kumwaga pesa kwenye nchi yenye vituko kama hivi,kama wamefikia kuteka wafanyabiashara na kuvuruga biashara za watu ,tumeumia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Iringa leo amekabidhi ofisi na gari mbele ya mkurugenzi wa manispaa hiyo na watumishi wote wa manispaa.

Kimbe amesema ameachia madaraka ya umeya kwa moyo mweupe ili vikao vya baraza la madiwani viendelee kufanyika na wananchi kupatiwa maendeleo. Kimbe amewataka watumishi wa Manispaa kutosikitika kwa yaliyotokea na badala yake waendelee kuchapa kazi kwa bidii.

Mkurugenzi wa Manispaa amesema wamesikitika sana kumpoteza Meya mwenye maono na aliyekuwa mchapa kazi haswa. Mkurugenzi amesema wataendelea kuifanyia kazi na kuikamilisha mipango yote makini iliyoachwa na Kimbe.

Source Eatv habari!

My take; Kama Kimbe ni mchapa kazi kwanini mmemtumbua?!!
Huyu dogo juzi alitoa povu huku akijitapa hatokabidhi ofisi imekuwaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom