Utunzaji wa Magari ya Serikali

Tembomtata

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
266
426
Huwa inaniuma sana ninapo pishana na magari ya serikali, madereva wengi (sio wote) hawafuati sheria, uendeshaji wao sio wa kujali utunzaji wa haya magari.

Haya magari yangekuwa yanatunzwa vizuri both na taasisi lakini pia na madereva wenyewe yangepunguza gharama kubwa zinazotumika kwenye manunuzi ya magari mapya na utunzaji wa yaliyopo.

Unakutana na gari ya serikali ya mwaka 2010 imechoka haifai, 10 years gari imenunuliwa mpya leo haifai kweli are we serious? Taasisi zingekuwa zinapimwa kwa matumizi mazuri ya resources sio tu uzalishaji.

Siku moja niko kwenye car wash, nikawa naongea na dereva mmoja wa serikali ananiambia kuna wakati inafika yeye ndo inabidi atafute hela ili afanye service sikutaka kuamini moja kwa moja ila if that is true then we have a very long way to go.

Niiombe Serikali yangu, ifanye jambo kwenye hili kama ni trainings kwa malogistics officers na dereva ama lolote lile linalowezekana
 
Madereva wa serikali hawana huruma hata kidogo na Magari Yao.
jamaa wako Rafu Sana na sio waangalifu wanachojali ni mbio Tu na kuwasha taa muda wote
 
Wanayaburuza ili yaonekane yamechoka ili mwisho wa siku wauziwe wenyewe, kuna Hard top moja amejiuzia Ndali Changu, lilikuwa bado zuri kabisa, kaulize bei aliyolipa utachoka
 
Kuna huyu dereva wa Landcruzer ya jeshi JWTZ huku mpakani mwa Tanzania na Msumbiji (Kambi ya Sindano)MASASI hii gari sijui kama itafikisha mwaka m1...
 
Kuna huyu dereva wa Landcruzer ya jeshi JWTZ huku mpakani mwa Tanzania na Msumbiji (Kambi ya Sindano)MASASI hii gari sijui kama itafikisha mwaka m1...
Kaka umemuharibia mtanzania mwezio.
 
Pesa ya serikali haina mwenyewe ndio maana boss anabebea gari yake ya ofisi mikaa ila yake alonunua kwa jasho lake utumzaji wake 99.9%
 
Sisi kama wananchi inabidi tuwasimamishe na kuwachapa viboko, hizo ni mali zetu, kodi yetu
 
Back
Top Bottom