Makanisa yaliojawa na shuhuda.
Huwa sielewi nini maana ya zile shuhuda.
Mtu anatolewa pepo anawekewa mic ili wasikie pepo linaongea.
Siku nzima unashinda kanisani, huna kazi za kufanya.
Upumbavu sana.
Nakubaliana na mtoa mada kwa asilimia zote na pia waliochangia humu wengi sana nakubaliana nao sana.
Labda nianze na hii ya kuwekea watolewa pepo mic ili wasikike.
Unapoinga kwenye mifumo ya kidunia ya kutaka/kutamani faida,LAZIMA utajikuta unapitia barabara zile zile(japo hata pembeni uchochoroni,ila sambamba na hizo njia) ambazo kwa kiasi kikubwa ndizo zaaminika kuwa zaleta hiyo/hizo faida kwa haraka ama uhakika zaidi.Kwa yeyote mtafuta pesa ama faida,kujitangaza hakutakwepeka. Na tangazo litazingatia 'tukio' lenye kuvutia zaidi ama mojawapo ya namna hiyo.
Naamini wapo waongoza kondoo/waumini ambao si feki na hata hutangaza shuhuda kwa nia njema kabisa za kuongeza imani za wasikilizaji (kwani shida nyingi za wanadamu zafanana tu,tofauti ni chache) ili nao waende wakapate uponyaji ama utatuzi wa kiroho.Ila,kama jinsi shetani alivyovamia na kuiga sadaka ya kumwaga damu,leo tunao masanii wa nyumba za ibada wanaotenda haya kwa nia ya kutangaza ili wawapate wahanga(wateja) wengi zaidi.Lengo likiwa ni hela za waumini.Hawa hawana haya,huruma wala kujali.Sera zao ni 'njoo na shida yako,ila leta/uje na pesa tu(ama tuma pesa kwa njia za simu)'.
Hawa utawasikia hata wao wenyewe wakivimba vichwa wasikiapo shuhuda zikutolewa maana wanajua marketing efforts zao likely zitalipa na kuwavuta wengi zaidi.
Huwa nasikiliza mahubiri mbalimbali.Kwa kweli,hata kwa msomaji Biblia wa kawaida utagudua upotoshaji wa ajabu sana wakati mwingine.Neno linaongezewa mbwembwe kibao za kibinadamu ili kuvutia watu.Naamini,neno lenyewe tu likisomwa,lina maajabu na nguvu kwa msomaji.Halihitaji kuongezewa mbwembwe na kihisia za kibinadamu,chumvi wala uongo kamwe.
Hata hao wanaokwenda hizo nyumba za ibada,wengine si ajabu sio kuwa ni wajinga sana wa neno kivile.Ila shida ikikaba,kwa baadhi akili hufa ganzi na kutafuta suluhisho kwa namna yoyote ile,hata kujipeleka kwa wasanii wa madhabahuni kutafuta ama suluhu,ama wachawi wa shida zao au sababu/vyanzo.Na hawa wasimamia shoo,hawakosi sababu na wanajua watu lazima waje tu.na si ajabu huomba shida zisiishe.
Hawa hutumia shida za wengine kuganga shida zao na hasa wanajua watu tunapenda sana njia za mikato,kutafuta wachawi na kutamani miujiza bila ustahiki wa kuipata hiyo miujiza kwa namna sahihi,rahisi na hata mingi mingine iliyo ndani ya uwezo wetu wenyewe.
Sikumbuki kusoma mahala Yesu kudai sadaka ama kuagiza mitume wake kudai sadaka.Ila nakumbuka akielekeza wakienda mahala,watafute kwa wenyeji panapowafaa waingie kwa ,watapata huduma humo;kitu kama hicho.
Sasa hivi,hawa wasanii hawatendi haya.Labda wakati haufanani.Ila,hata wakienda mahala,si ajabu watalala mahoteli ya kifahari zaidi kuzidi hata kiwango cha muumini yeyote wanaowahubiria.Wakitoka humo,wataweka msisitizo mkubwa wa sadaka na mambo yao yanaenda safi tu.Na hapa ndipo ujanja na werevu wa kuweka mashiko kwenye imani ili kuvuta zaidi watu na kuongeza zaidi faida.Mambo ya imani ili kuyawekea faida,yanawekewa 'vitu'.Navyo ni chumvi,maji n.k. maana nadhani walishajua,ama watu walishazoea sana au vipi,kuweka tu mikono,watu hawatoi hela ya kutosha.Mpaka umkabidhi kitu,ndipo pesa ama hutoka zaidi ama ni rahisi 'kuidai' kirahisi zaidi.Upande wangu,naamini wapo wanaofanya haya kwa nia njema na uhalisia,ila wapigaji nao wamehamia humo kibao!!!
Jana tu,kuna jamaa akampigia mmojawapo wa hawa watu kwa shida yake.Akaishia kuagizwa atume 150,000/= haraka sana ili apate ukombozi.Tena ikiambatana na utisho wa ajabu kusisitiza kuhusu chanzo cha hiyo shida.Labda ili hiyo pesa itumwe haraka zaidi.Agizo lilitokea eneo la Kinondoni.Hii ni ajabu,upuuzi na kioja cha hali ya juu kabisa.Hakika manabii wa uongo wamejaa na tunao wengi mno.
Kuna siku nilisikia rais wa Rwanda (ama uongozi wa huko) waliamua kuyapunguza makanisa feki sababu hakuelewa sababu ya uwepo wa makanisa mengi mno huku mengine hata hayaeleweki.Wakati ule,nilikubaliana naye kwa theluthi mbili,ila theluthi moja nikasita kuwa labda kuna walakini.Hatimae nilikuja kuamini,hakika YUPO SAHIHI na hili twalihitaji sana hapa Tz.Tuna wasanii wasio hata na haya,huruma wala kusita na hawana hata huo woga wa Mungu.
Natamani siku moja nchi hii iwe na utaratibu wa kuchuja hizi nyumba za ibada.Najua si rahisi hasa ukizingatia serikali haiingilii mambo ya imani,na labda haitakuja kutokea.Ila,kwa urahisi na wepesi wa kufikia waumini ulivyo mkubwa sasa,hakuna haja ya utitiri wa makanisa ambayo asilimia kubwa sana ni shoo za kuvuta na kupiga hela tu kwa faida ya wasimamia hizi shoo, tena toka kwa walio na hali ya chini,wahitaji na wenye shida.Naamini na kukubali kuwa,sadaka itolewe na kila mmoja.Ila,hawa wengine wanautumia huu mwanya kinyama sana tena bila haya wala huruma.
Kwa kuwa pia nakumbuka mahala kwenye Biblia panasema,ile siku Yesu atawakataa hata wale watakaojitetea kuponya kwa jina lake,hii inaashiria wazi kuwa,kuponya,pamoja na sarakasi za namna hiyo,sio kigezo cha usahihi wa huyo atendaye hayo.
Ila,heshima kwa viongozi wote wa dini (zote) ambao wanazingatia misingi ya imani zao kwa kuweka maslahi ya dini/imani zao na kuongoza na kuelekeza waumini sawa sawa na matakwa ya mapenzi ya Mungu.Hawa waliobaki wanaoenda nje ya mstari,Mungu anawaona.