Utumwa mpya ndani ya Kanisa

Ukiwa na namna yako ya pekee ya mtindo wa maisha hapa duniani ni ngumu sana kueleweka na walimwengu wote hata kama yana mafanikio makubwa .

Wewe IGA yule anayefuatwa na watu wengi wa ulimwengu huu hata kama ni mdhambi!! hapo sasa ndivyo utakavyo kubalika na kueleweka vizuri na walimwengu wa dunia na ulimwengu huu.
 
Teh heheheee! Kutwa kucha unahangaika na uwepo wa Mungu, kila nyuzi inayotaja Mungu upo halafu unawadanganya eti hayakusumbui. Unasumbukaje? Kwa sababu moyoni mwako ukweli unaujua na ndio unaokusumbua!
Wewe huangaiki? hebu toa hoja! Siyo kashfa na maneno machafu ambayo mnadai Mungu hapendi.
 
wajinga ndio waliwao
 
Kweli kabisa
 
You mess up..!
Hata kama hilo ni kweli, huo ni ushahidi zaidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, kusingekuwa na mess ya aina yoyote.

Kila kitu kingekuwa katika perfect order.
 
Watu wamekuwa wavivu kuisoma biblia ndiyo maana wanapigwa, na waendelee kupigwa mpaka akili iwakae sawa. Watu wanapenda miujiza ya kuombewa, mara maji mara mafuta, mara chumvi nk.

Hakunaga mambo ya kuvunja laana hakuna nabii wala mtume wala mchungaji awezaye kuvunja laana, laana zilivunjwa na Yesu akamaliza kama akuzimaliza Yesu ni mtu gani awezaye kuzivunja?
Sadaka na zani vinapaswa vitolewe mahala sahihi hambapo hakuna ufisadi, ili vifanye kazi ya Mungu, lakini kwa staili hii ya uvivu wa kuyasoma maandiko wacha waendelee kupigwa mpaka akili ziwakae sawa.
 
Hahahah..! Kiranga Kwa akili yako wewe una hisi Mungu anaupande..?

Mungu yupo katikati ya mazuri na mabaya, God has no choice, no good or bad to him..! Alichonifanya kibaya na kizuri kwa binadamu ndicho kipimo cha hukumu zake kwetu.

Kifupi iko hivi hizo maafa na mabaya yote tunayaumba sisi katika maisha yetu si Mungu. Mfano huwa mnaambiwa dhambi mwisho wake ni mauti/kifo, utambue mtenda dhambi ni binadamu si Mungu.

Ukisema Mungu angetuumba na kutunyima utashi tufanye kazi kwa settings/programmed kama computer ata wewe hapo usinge hoji haya maswali yako ya kijinga. By the way Malaika wako programmed na hawa hizo mess zote unazosema kuwepo kwake ni kuthibitisha kutokuwepo kwa Mungu, mfano Malaika hawapatwi na hizo maafa na mabalaha, Lakini usidhani Malaika wanaenjoy/kufurahia uumbwaji wao zaidi ya binadamu.


Wewe jamaa uwezo wako wa reasoning nautilia shaka sana...!
Hata kama hilo ni kweli, huo ni ushahidi zaidi kwamba Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, kusingekuwa na mess ya aina yoyote.

Kila kitu kingekuwa katika perfect order.
 
Asipo elewa na hii uyu jamaa atakuwa na pepo anapepo zito (linalompelekea upumbavu ,ujinga pia na ukichaa wakutokuamini uwepo)

Ila naamini MUNGU atakuja kumuonyesha yeye ni nani kwake ikifika wakati
 
Ni kweli kabisa mtoa mada walokole wa sikuizi wamekuwa kama wajinga au naweza sema misukule hawapo katika uwezo wao kamili au timamu wa kufanikisha au kuratibu mambo yao katika ubongo wao

Toa ubarikiwe!
Hakuna mahali kwenye biblia wameandika toa ubarikiwe lakini kuna mahali for wameandika toa kwa hiari yako na kutoa kwa hiari sio kushinikizwa na kutishwa kwamba usipotoa utalaaniwa huo ni ujanja wa wahuni tunamtolea MUNGU kwasabu ametubariki na sio kwasababu atupe vitu MUNGU sio betting umpe ili akupe vyote ni vyake ata ulivyo navyo pia ni vyake kwaiyo kwa swala la kutoa huangalia moyo wa mtu ambao unatoa shukrani kwa vichache ambavyo MUNGU amempa si kwa kutishwa au kulazimishwa kwa hiari yake mwenyew

2 Wakorintho 8:3 Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao;

Watu walitoa kwa hiari na sio kwa kutishwa

Na hili limepelekea ujinga kabisa na watu wamekuw wavivu Yesu alifanya kazi mchana kutwa na bado usiku alikuwa anaenda kuomba
Walokole ujinga uwatoke yaani kazi wanakuwa wavivu ukitegemea miujiza nasema sahau hiyo miujiza maandiko yanasema kila mtu atavuna alicho panda

Kama ulipanda haba utavuna haba afu unaanza MUNGU mbona umeniacha MUNGU hajawai muacha mtu ,mtu ndiye anamuacha MUNGU

Uvivu piga kazi sana kwa nguvu zote kwanza MUNGU huwa hashughuliki na
Wavivu hata sikumoja acha uvivu piga kazi

Wagalatia 6:7 Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi; kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna.
 
Makanisa mainstream ndio majizi orijino. Katoliki, Lutheran, Anglican na mengineyo... Tena haya ndio kichefuchefu zaidi kwani hupeleka huo mshiko wanaotuchukulia Rumi, Jeremani, Uingereza na kwingineko. Kwa kuwa wote ni wevi huwa nawaunga mkono hawa wajasiria dini wa kisasa kwani wamejiongeza na hukuza uchumi wa humu humu kwetu. Wameamua kuchukua fungu lao linalowaangukia...
Kanisa Katoliki kwa mfano, limewahi kupora, kutesa, kuua walioitwa 'wazushi', kushiriki biashara ya utumwa na zaidi kusaidia mataifa ya Ulaya ya Kikatoliki kueneza ukoloni Afrika, Asia na Amerika ya Kusini huku lenyewe likineemeka pakubwa kwenye 'uwekezaji' huo.
Sijui kama lilishawahi kuomba radhi kwa dhuluma kubwa ambazo limeifanyia ainabinadamu, na hata lijapoomba radhi, bado manufaa ya kiuchumi yaliyotokana na dhuluma hizo ndio msingi ambao kanisa limeegama kwa sasa.
Huu unaouita 'utumwa mpya' ni rasha rasha tu, mapichapicha yenyewe hasa yalikuwa na hadi sasa yako kwenye makanisa makongwe niliyoyataja hapo juu. Anza na hayo kwanza kisha ndio uje kuwashambulia wanangu wa faida walioiona fursa na kuamua kuchukua chao.
 
Chaajabu hata baadhi ya waislam wameanza mambo haya hasa kwa mbinu za nyota zilizo ibwa sijui....

all in all huu ni wizi wa wazi

Mambo ya nyota ni upuzi na ushikirikina. Wenye kuamini hayo watapata hukumu yao. Hakika ya Uislamu ni dini ya haki umejitenga mbali na machafu yote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…