Utumishi kwanini wamefanya hivi?

Utumishi kwanini wamefanya hivi?

Mwamba028

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2013
Posts
4,648
Reaction score
3,807
Kwenye tangazo la kuitwa kazini la tar 17 idadi ya watu waloitwa ni pungufu kulingana na ile walotangaza

Mfano kwa nafasi ya afisa utumishi nafasi zilikuwa 40 ila wameita watu 8 tu
nafasi ya afisa tarafa walitangaza nafasi 5 lakini wameita watu wawili

Kwa mwenye majibu au tetesi embu anijuze aisee mana binafsi nlikuwa dissapointed sana ile siku nlipoona hlo tangazo
 
hapa hata mimi sijawaelewa ila nimehisi hawana fungu la kulipa wakipata pesa wataita tena

afisa tawala nafasi 15 wameita 3
 
Kuna watu huwa wapo kwenye database ya Utumishi wanasubiri nafasi wapangiwe. Hawa ni wale ambao walifanya oral interview na hawakubahatika kuitwa kazini. Hivyo nafasi zikitoka hupelekwa.
 
yaah inawezekana fungu linasumbua mana kampen ilikula snaa
 
okonkwo tutapoa tu mkuu

na hyo database iteme bc mana uku kistreet co mchongo asee
 
Kuna watu huwa wapo kwenye database ya Utumishi wanasubiri nafasi wapangiwe. Hawa ni wale ambao walifanya oral interview na hawakubahatika kuitwa kazini. Hivyo nafasi zikitoka hupelekwa.

mkuu sawa data base ipo ila wametoa nafasi 40 wameita watu 8 ( including wa kwenye data base) ivyo kuacha ombwe la nafas kama 30+ ivi.
 
mkuu sawa data base ipo ila wametoa nafasi 40 wameita watu 8 ( including wa kwenye data base) ivyo kuacha ombwe la nafas kama 30+ ivi.

"ombwe" umetumia msamiati adimu kwel mkuu,,haha
 
Tumeipenda wenyewe,, Chaguo letu wenyewe,,
Acha waisome namba eeeeeh,,(waisome namba) sisiem mbele kwa mbeleeee
Hatuna muda wa kupoteza tena cha msingi nafasi hizo watu washaitwa wakafanye kazi
Mmezoea sana kulalamika waswahili acheni hizo, wengine mkajiajiri.

Hapa Kazi Tu.
 
Kuna watu huwa wapo kwenye database ya Utumishi wanasubiri nafasi wapangiwe. Hawa ni wale ambao walifanya oral interview na hawakubahatika kuitwa kazini. Hivyo nafasi zikitoka hupelekwa.

Hata kama ni hivo majina huwa wanayapublish kwa pamoja na hao wa sahivi
 
MUNGU ni mwema mm naamini mtairwa tu tena zaid ya hzo nafas zilizobaki,watakuwa wanaweka mambo sawa mtaitwa tuu
 
Huo mchezo wa kuita watu pungufu kwenye ajira haujaanza leo.

Wakipigiwa simu majibu yao hata hayaridhishi watu wanenda wanakata tamaa sasa hata kuhudhuria usaili wao.
 
Huo mchezo wa kuita watu pungufu kwenye ajira haujaanza leo.

Wakipigiwa simu majibu yao hata hayaridhishi watu wanenda wanakata tamaa sasa hata kuhudhuria usaili wao.

wakipigiwa huwa wanasemaje mkuu
 
hapo nikwenda utumishi kuuliza n kupata majibu ya uhakika, haiwezekani kuwaita watu waliokua kwenye database,kwenye data base huwa wanaitwa ikiwa kunanafasi haikutangazwa na tayari wanao watu wenye sifa kwa nafasi hizo kwenye database ila kwa zile zilizotangwa wanaitwa ni wale waliohudhulia kwenye interview tu
 
wakipigiwa huwa wanasemaje mkuu

''nafasi hazikuwa kama kwenye tangazo ila tulitangaza idadi hiyo tukitegemea kuwa zingeweza kuongezeka ila bahti mbaya hazikuongezeka''

au

''ukiona hivyo ujue wengine hawakufaulu usaili kwahiyo tutatangaza tena hizo nafasi zilizobaki''

hayo ni baadhi ya majibu yao.
 
Jipeni moyo na kanzu data yenu... Yaani kanzu data mtu mmoja aitwe sehemu mbili tofauti???? :crazy: Sisemi kwamba siwaamini utumishi ila sio kitu cha kutegemea kabisa na kuanza kujipa moyo.
 
Back
Top Bottom