Lakini kingine mara nyingi wadhamini ndiyo huwa wanaweka sharti la uwepo wa Consultant kwa ajili ya kudhibiti baadhi ya mambo fulani. Haya tumeona sana.Kuna tetesi nimesikia wizara ya maji inataka kusaini mikataba na makampuni ya consultants kwa ajili ya usanifu wa miradi ya maji na usimamizi wake.
Je inakuaje serikali itumie hizi kampuni wakati inaweza tumia wataalam wa ndani?
Inakuaje serikali iwe tayari kulipa kampuni ya consultants mabilioni ya pesa wakati kazi hiyo inaweza fanyika kwa gharama ndogo kwa kutumia wataalam wa ndani?
Yani mradi wa kijiji kimoja unaajiri kampuni isanifu kweli?
NB: Nashauri hiyo mikataba ya consultants mnayotaka kusaini mwaka huu msisaini kama kweli mnajali fedha za umma wa watanzania!!