"Utumbuaji Majipu" na Haki ya Kusikilizwa!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,192
1,971
Tumeona "Majipu" yakitumbuliwa lakini hatukuona Wahanga wakipewa hata nafasi ya kusikilizwa ambayo huwa ni ya msingi sana katika utendaji haki! Hata Adam na Hawa walipotenda dhambi Mungu aliwauliza kwa nini walifanya hivyo na wakajitetea ndipo Mungu "akatumbua majipu!" Mungu aliwapa wenye "majipu" haki ya kusikilizwa na hata kujitetea japokuwa yeye anajua yote!

Kwa Magufuli hali ni tofauti, yeye sio kwamba anajua yote ila tu anapewa taarifa na watu ambao wengine wana chuki binafsi! Na wengine wenye "majipu" huenda walikuwa under coercion ndio maana wakafanya/wakashindwa kufanya yale waliyofanya/waliyoshindwa kufanya!

Tuliona hata Magufuli mwenyewe alitaka kubomoa jengo la TANESCO Ubungo ambalo limejengwa kwenye reserve ya barabara wakati akiwa Waziri wa Ujenzi lakini mabosi wake walimshika mkono akashindwa kufanya hivyo! So, there must be a reason, however wrong it is!

Ushauri:
Magufuli, wape hao wenye "majipu" angalau dk moja kujieleza inaweza kuleta "mitigation" katika adhabu utoazo!
Nawasilisha kwa mjadala zaidi!
 
Hao jamaa washasikilizwa sana na Mkwere!
Ukiwasikiliza utaambiwa maneno mazuri sana na ripoti tamu tamu!
Hao jamaa nikuwatumbua tu!
 
Nafikiri turudi kwenye kuunda tume za uchunguzi. Huko ndio watanzania tumezoea.
 
kwa mtazamo wangu nashauri magufuli aendelee tu na 'style' yake kwasababu ukisema awape mda wa kujieleza wataanza kuleta nyimbo nzuri ambazo tumeshazizoea na ndo zilizo kwamisha maendeleo ya nchi yetu kwa miaka mingi.
 
Assumption ni kwamba Magufuli huwa hakosei, haonei mtu, right? Kama Mungu Mwenyezi alitoa hiyo nafasi ya kujieleza sembuse mwanadamu?
 
Nafikiri turudi kwenye kuunda tume za uchunguzi. Huko ndio watanzania tumezoea.

Sishauri aunde Tume ila tu awaandikie hata barua awape siku kadhaa kujieleza kisha aendelee na kazi yake! What's wrong with that?
 
Suala la msingi utumbuaji uko kwenye mamlaka yake na wakati mwingine naamini wanaotenguliwa!Si kwamba wana makosa wengine anaona kasi yake ya utendaji hawataiweza.
 
Tumeona "Majipu" yakitumbuliwa lakini hatukuona Wahanga wakipewa hata nafasi ya kusikilizwa ambayo huwa ni ya msingi sana katika utendaji haki! Hata Adam na Hawa walipotenda dhambi Mungu aliwauliza kwa nini walifanya hivyo na wakajitetea ndipo Mungu "akatumbua majipu!" Mungu aliwapa wenye "majipu" haki ya kusikilizwa na hata kujitetea japokuwa yeye anajua yote!

Kwa Magufuli hali ni tofauti, yeye sio kwamba anajua yote ila tu anapewa taarifa na watu ambao wengine wana chuki binafsi! Na wengine wenye "majipu" huenda walikuwa under coercion ndio maana wakafanya/wakashindwa kufanya yale waliyofanya/waliyoshindwa kufanya!

Tuliona hata Magufuli mwenyewe alitaka kubomoa jengo la TANESCO Ubungo ambalo limejengwa kwenye reserve ya barabara wakati akiwa Waziri wa Ujenzi lakini mabosi wake walimshika mkono akashindwa kufanya hivyo! So, there must be a reason, however wrong it is!

Ushauri:
Magufuli, wape hao wenye "majipu" angalau dk moja kujieleza inaweza kuleta "mitigation" katika adhabu utoazo!
Nawasilisha kwa mjadala zaidi!
Ndio maana wanasimamishwa kazi kupisha uchunguzi,zamani watu mlizoea tume ambapo watuhumiwa walikuwa wanachunguzwa huku wakiendelea na madaraka yao jambo ambalo si sawa ukitakamatokeo mazuri na huu ndio utaratibu unaotumika na wenzetu walioendelea,unasimamishwa kazi unapisha uchunguzi.
 
Dr Hoseah anasubiri uchunguzi upi?
 
Suala la msingi utumbuaji uko kwenye mamlaka yake na wakati mwingine naamini wanaotenguliwa!Si kwamba wana makosa wengine anaona kasi yake ya utendaji hawataiweza.

Kwani wakipewa nafasi ya kujieleza ndio Magufuli atakuwa ameporwa mamlaka yake?
 
Tumeona "Majipu" yakitumbuliwa lakini hatukuona Wahanga wakipewa hata nafasi ya kusikilizwa ambayo huwa ni ya msingi sana katika utendaji haki! Hata Adam na Hawa walipotenda dhambi Mungu aliwauliza kwa nini walifanya hivyo na wakajitetea ndipo Mungu "akatumbua majipu!" Mungu aliwapa wenye "majipu" haki ya kusikilizwa na hata kujitetea japokuwa yeye anajua yote!

Kwa Magufuli hali ni tofauti, yeye sio kwamba anajua yote ila tu anapewa taarifa na watu ambao wengine wana chuki binafsi! Na wengine wenye "majipu" huenda walikuwa under coercion ndio maana wakafanya/wakashindwa kufanya yale waliyofanya/waliyoshindwa kufanya!

Tuliona hata Magufuli mwenyewe alitaka kubomoa jengo la TANESCO Ubungo ambalo limejengwa kwenye reserve ya barabara wakati akiwa Waziri wa Ujenzi lakini mabosi wake walimshika mkono akashindwa kufanya hivyo! So, there must be a reason, however wrong it is!

Ushauri:
Magufuli, wape hao wenye "majipu" angalau dk moja kujieleza inaweza kuleta "mitigation" katika adhabu utoazo!
Nawasilisha kwa mjadala zaidi!

Amri/Agizo la raisi wa JMTZ halipingwi na mtu au chombo chochote kile ndani ya JMTZ bali linatekelezwa TU!

...ushawahi kuwa na jipu? Hata upewe haki ya kusikilizwa litatumbuliwa tu maana huwa hakuna namna ya ziada (alternative)! So we might as well save ourselves some time na kwenda moja kwa moja kwenye utumbuaji.
 
Sishauri aunde Tume ila tu awaandikie hata barua awape siku kadhaa kujieleza kisha aendelee na kazi yake! What's wrong with that?

Kama kuna madudu yametokea chini ya mtu aendelee kuachwa ili iwe nini? Lazima uwajibike kwa nafasi yako ili tuanze upya vizuri.
 
Dr Hoseah anasubiri uchunguzi upi?

Hivi mtu kama Hosea kama kweli unataka kupambana na rushwa unataka uchunguzi gani tena. Ebu acheni maneno mengi watanzania uwezi kufanya chochote bila kufanya kazi na watu wenye discipline.
 
...ushawahi kuwa na jipu? Hata upewe haki ya kusikilizwa litatumbuliwa tu maana huwa hakuna namna ya ziada (alternative)! So we might as well save ourselves some time na kwenda moja kwa moja kwenye utumbuaji.

"Jipu" ni lugha ya picha ikiwa na maana kuwa kuna ukiukwaji wa sheria, taratibu, kanuni, etc! Haimaanishi kuwa mtu anapoonekana amefanya kosa basi anakuwa amelifanya kweli! Hata kama kalifanya kweli pia ana haki ya kusiklilizwa!
 
Back
Top Bottom