Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,081
- 62,752
MITHALI 11:6. HAKI HUOKOA WENYE HAKI. FITNA ZA KISIASA ITAWANASWA WENYE HILA. HAKI NDIO USALAMA WA NCHI NA SIO VINGINEVYO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Bado Kuna mtifuano ndani ya nchi. Mambo ni kama yanazidi kutokota.
Maoni yangu binafsi, malalamiko ya watu yafanyiwe kazi. Hasa kuhusu Haki za watu ikiwemo Haki ya kujua kina nani wanafanya UTEKAJI na MAUAJI, baadhi ya mateka wapo wapi.
Nchi itakuwa salama ikiwa wananchi wote wapo salama. Nchi huweziiita inausalama ikiwa Kuna mwananchi hata mmoja ambaye hayupo salama.
Nchi huanza na mtu mmojammoja. Kujali maisha na usalama wa mtu mmoja ni kujali maisha ya taifa na usalama wa taifa Zima.
Watibeli tunasisitiza, hakuna haja ya mafarakano. Njia ya suluhu ni kuitafuta HAKI ilipo na kuitenda. Nani kaonewa apewe Haki yake. Nani kadhulumu apewe anachostahili.
Kutumia ubavu, vitisho na ubabe sio njia sahihi katika usalama wa nchi. Hasa kama watu wanahoja ya msingi ambayo ingeweza kusikilizwa.
Yesu aliwahi kuambiwa kuwa awaamuru wanafunzi wake waache kupiga Kelele. Akajibu, hakika wanafunzi wake wakikaa kimya basi Mawe yatapiga Kelele.
Falsafa ya kauli hiyo inamaana kubwa katika utawala na uongozi. Ni akheri watu kupiga Kelele kuliko Mawe yapige Kelele. Ikifikia Mawe yakianza kupiga Kelele itakuwa ni too late katika usalama.
Ni kweli watu wanaweza kutumia HAKI pia kufanya uhalifu. Yaani mtu anaweza kutumia KISINGIZIO Fulani cha HAKI kama sehemu ya kutimiza Hila yake kupata jambo Fulani.
Njia sahihi ya serikali kutoruhusa wenye Hila kutumia HAKI kama chambo ni kuitenda HAKI husika.
Ipo hivi, wenye HAKI wakikaa kimya Haki ikakanyagwa basi waovu Fulani huweza kuinuka kuitetea HAKI hiyo kwa malengo yao binafsi.
Ikiwa viongozi wenye dhamana watakaa kimya Haki zinapokanyagwa ni wazi kuwa nature itazalisha Wahalifu na watu wabaya kuitetea HAKI ambayo imekaliwa Kimya.
Makundi mengi ya Waasi na Magaidi duniani ni matokeo ya wenye HAKI kukaa kimya. Kama wenye HAKI wangetenda wajibu wao automatically kusingekuwa na kitu kinachoitwa Waasi au Magaidi duniani kwa sababu Waasi na Magaidi duniani hutumia HAKI Fulani iliyosikanyagwa kama chambo au KISINGIZIO cha Yale wayafanyayo.
Mfano, haiwezekani mtu ndugu yake kauawa, au kapotea katika mazingira tata alafu wenye wajibu wa kumlinda, kuchunguza na kutenda haki kwa waliomuua ndugu yao hawatimizi huo wajibu.
Mtu huyu ni rahisi kushawishiwa kujiunga na makundi mabaya katika kulipa Haki ya ndiye(Kisasi).
Watibeli tunapenda Amani na utulivu. Lakini tunapenda Amani ambayo chanzo chake ni HAKI. Sio amani ya dhulma.
Amani ya dhulma ni Ile ambayo watu hujiona salama kwa vile mambo mabaya hayajawakuta ila yanawakuta wengine. Amani ya dhulma ni amani bandia ambayo huchangiwa na watu kutokuwa na UPENDO.
Mtu asiye na UPENDO huwa mwoga, hawezi kuwa JASIRI, hawezi kuwa mkweli, hawezi kuwa Huru.
Hana UPENDO ndio maana hata mwingine akiumia au kudhulumiwa atakaa kimya kwa sababu ya woga, ubinafsi, na unafiki.
Amani ya kweli ipo kwa wenye HAKI, wenye UPENDO, AKILI na wapenda UKWELI.
Kuhusu maandamano yanayoratibiwa kesho kutwa September 23.
Maandamano hayo hayatakuwa HAKI ikiwa lengo lake ni kumtoa Rasi Samia Suluhu kwa kauli ya SAMIA MUST GO.
Sisi Watibeli hatutayasapoti.
Lakini tutayasapoti endapo lengo litakuwa kupiga Kelele, kuishinikiza serikali kuwatafuta WAUAJI na watekaji wa matukio yaliyotokea kwa sababu yanahatarisha usalama wa nchi.
Yanahatarisha usalama wa nchi kwa sababu ndugu na jamaa waliofanyiwa hivyo vitendo wanaweza kuichukia nchi yao kwa Kuona haikujali uhai wa wapendwa wao na hivyo kuunda roho ya UASI ili kulipa Kisasi.
Hiyo Samia Must Go ifanyike Mwaka kesho kwenye Sanduku la Kura. Ikitokea Wizi wa kura basi walioibiwa watakuwa na HAKI ya kupigana Kufa kupona kupata HAKI yao na sisi watibeli tutawaunga Mkono wenye hiyo HAKI bila kujali uwezo wao, nguvu zao, nafasi zao, idadi yao, tabia zao n.k.
Kwa sababu kama wameshinda why not wasipewe Ushindi wao?
Lakini kama hawajashinda hawatakuwa na Haki hiyo.
Nimalize kwa kusema, tuipende nchi yetu.
Na kuipenda nchi yetu ni kupendana sisi kwa sisi.
Na kupendana sisi kwa sisi ni kutendeana kwa HAKI.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa Sasa Dar es salaam
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Mithali 11:6
Haki yao wenye haki itawaokoa; Bali wafanyao fitina watanaswa kwa hila yao wenyewe.Bado Kuna mtifuano ndani ya nchi. Mambo ni kama yanazidi kutokota.