Mzee23
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 1,696
- 3,472
Habari Wakuu,
Madam President anasema pamoja na liukuta likuubwa na ulinzi wa mabunduki wa JWTZ (na makamera) "MADINI YANATOROSHWA KAMA KAWAIDA CHINI KWA CHINI"
Hili limenikumbusha maneno ya mchimbaji mdogo wa madini hayo alipokuwa anatupa visa vya utoroshwaji madini machimboni.
Ilikuwa ni siku chache baada ya kuzinduliwa Ukuta wa Mirerani, mimi nikamwambia umejengwa ukuta sasa utoroshwaji umefika mwisho.
Cha kunishangaza jamaa alicheka sana!
Akaniambia kuwa kwenye machimbo huwa kila mtu ana njia yake anayopita akichimba huko chini hivyo ukuta ule ni kituko tu kwani hizo njia zinatoka nje ya ukuta kupitia chini kwa chini bila walinzi kuwa na habari.
Naona ndio wanaligundua hili leo.
Ushauri wangu: Kwenye ulinzi wa rasilimali zetu kama madini Serikali isijikite tu kwenye bunduki za wanausalama, ijenge urafiki na ushirikiano na wachimbaji hasa wadogo itajua siri nyingi za utoroshwaji madini.