Utoroshaji Tanzanite umenikumbusha maneno ya mchimbaji huyu

Mzee23

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
1,696
3,471
Habari Wakuu,

Madam President anasema pamoja na liukuta likuubwa na ulinzi wa mabunduki wa JWTZ (na makamera) "MADINI YANATOROSHWA KAMA KAWAIDA CHINI KWA CHINI"

Hili limenikumbusha maneno ya mchimbaji mdogo wa madini hayo alipokuwa anatupa visa vya utoroshwaji madini machimboni.

Ilikuwa ni siku chache baada ya kuzinduliwa Ukuta wa Mirerani, mimi nikamwambia umejengwa ukuta sasa utoroshwaji umefika mwisho.

Cha kunishangaza jamaa alicheka sana!

Akaniambia kuwa kwenye machimbo huwa kila mtu ana njia yake anayopita akichimba huko chini hivyo ukuta ule ni kituko tu kwani hizo njia zinatoka nje ya ukuta kupitia chini kwa chini bila walinzi kuwa na habari.

Naona ndio wanaligundua hili leo.

Ushauri wangu: Kwenye ulinzi wa rasilimali zetu kama madini Serikali isijikite tu kwenye bunduki za wanausalama, ijenge urafiki na ushirikiano na wachimbaji hasa wadogo itajua siri nyingi za utoroshwaji madini.
 
Uweze kujenga ukuta usiweze kufuatilia njia za chini kwa chini. Nyie ni watu wa ajabu mwalidharaulisha na kulifedhehesha jeshi letu la JWTZ mbele ya jamii kwa tamaa zenu za madaraka ya kisiasa. Chagueni nini cha kuongea basi. CDF na team nzima ya ulinzi na usalama iwajibishwe kwa uzembe huu mtakao kutuaminisha.
 
Tanzanite ni za Watanzania na wanaotorosha ni Watanzania wanaohatarisha maisha yao kwenye mahandaki.

Hizi rasilimali ni za kwetu sote acheni wachimbaji wajikwamue kiuchumi.
 
Uweze kujenga ukuta usiweze kufuatilia njia za chini kwa chini. Nyie ni watu wa ajabu mwalidharaulisha na kulifedhehesha jeshi letu la JWTZ mbele ya jamii kwa tamaa zenu za madaraka ya kisiasa. Chagueni nini cha kuongea basi. CDF na team nzima ya ulinzi na usalama iwajibishwe kwa uzembe huu mnaotu aminisha.
Wajitathmini,siyo hadi mama awawajibishe. Ni fedheha sana, walinzi wapo, halafu mali zinaporwa.
 
Na zinazo porwa na Majizi na Mafisadi ambao ni baadhi ya wanasiasa na washirika wao nani atajitathimini? Acheni huu upuuzi wenu.
CDF ajitathmini,aonyeshe mfano. JPM alikua anawasema wengine, huyu kampandia hadi CDF.

Kwakweli yeye na wenzake, wawajibike, ni fedheha, nadhani JPM hakua anajua kama udhaifu huo upo, angewawajibisha.
 
Inasikitisha kusikia kua hata taarifa za kutoroshwa madini tumekuja kuzipata baada ya kifo cha mwendazake
Ilikuwa ni dhambi kubwa kiasi gani kuongea ukweli kwenye utawala uliopita?
Waliokua kwenye utawala ule halafu wakakaa na JPM kinafiki hawafai kabisa, walitakiwa waache ngazi kuonyesha hawakubaliani na unafiki,badala yake eti saa hizi,ndiyo wanasema, hii si sawa. Tuishi maisha ya kweli na halisi, kama JPM alivyoishi kwa kuonyesha rangi yake halisi hadi anakufa.
 
Uweze kujenga ukuta usiweze kufuatilia njia za chini kwa chini. Nyie ni watu wa ajabu mwalidharaulisha na kulifedhehesha jeshi letu la JWTZ mbele ya jamii kwa tamaa zenu za madaraka ya kisiasa. Chagueni nini cha kuongea basi. CDF na team nzima ya ulinzi na usalama iwajibishwe kwa uzembe huu mnaotu aminisha.
Unabishana na rais aliyosema hayo jana?
 
sii kweli kwa njia za chini ni haiwezekani itakuwa ni mbinu nyingine ila ya njia za chini ni kitu hakiwezekani
Ni hivi.. umezungushwa ukuta sawa, lakini uchimbaji huhusisha utafutaji wa mali mielekeo tofauti tofauti chini kwa chini hivyo kuzaa mahandaki marefu ambayo yanavuka usawa wa ukuta umbali mrefu tu.. sasa kama unataka kutoroshea hukohuko unashindwa?
 
Kama kuna kitu cha kipuuzi na kijuha kilifanywa na utawala wa mwendazake ni huu ukuta.

Labda kama alijenga kudhibiti vibaka...eneo ambalo tulipigwa vibaya kwenye madini ni mikataba mibovu tuliyoingia na wapigaji na madalali nje ya nchi.

Kwa tech ilivyo advance haikuwa sahihi kabisa kujenga ule ukuta
 
Uweze kujenga ukuta usiweze kufuatilia njia za chini kwa chini. Nyie ni watu wa ajabu mwalidharaulisha na kulifedhehesha jeshi letu la JWTZ mbele ya jamii kwa tamaa zenu za madaraka ya kisiasa. Chagueni nini cha kuongea basi. CDF na team nzima ya ulinzi na usalama iwajibishwe kwa uzembe huu mnaotu aminisha.
Katamka rais sisi tunaongeza nyama tuu
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom