Utoroshaji Tanzanite umenikumbusha maneno ya mchimbaji huyu

Inasikitisha kusikia kua hata taarifa za kutoroshwa madini tumekuja kuzipata baada ya kifo cha mwendazake
Ilikuwa ni dhambi kubwa kiasi gani kuongea ukweli kwenye utawala uliopita?
Risasi kama mvua enzi za mwendazake endapo ungesema ukweli. Bora walikaa kimya enzi hizo ili waje waseme ukweli enzi hizi!

Hili ndio funzo tunalolipata kutokana na utawala wa aina ya mwendazake
 
Unabishana na rais aliyosema hayo jana?

Siwezi kubishana na Mh Rais ila na bishana na wapambe nuksi walio mfanya asema siku za maombolezi ni 14 wakidhani ni kumkomoa marehemu kumbe Kikatiba ni siku 21 zilizoisha jana.

Wanao mdanganya Mh Rais kuwa baadhi ya wafanyabiashara walioingia kwenye mshikemshike wa kudaiwa lodi kimaguvu na kimabavu bila kutumia akili ni watakatifu kuliko malaika wa Mungu wa Mbinguni na wamedhulumiwa jasho lao. Hivi huyo Mfanyabiashara aliye kuja na private jet kutaka kuyatengeneza mambo ya kodi akazenguliwa na kuondoka ni nani? Mbona hatajwi jina jamii ikmjua huyu mfanyabiashara mtakatifu.
 
Katamka rais sisi tunaongeza nyama tuu

Sio kweli mnaongeza nyama, pilipili, limao tangawizi na mazaga zaga yote. Hatairi iko kama yenye ndiye kaenda sokoni kuwaletea hivi vitendea kazi au kaletewa na walio tengeneza mazingira ya yeye kufika hapo sasa analipa fadhila. Shughuli ndio imeanza.
 
One thing for sure.. SSH ndio rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...louder n clearer
 
One thing for sure.. SSH ndio rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...louder n clearer

Nani aliye bisha na kupinga hilo? Wasiwasi baadhi yetu kwa mwanzo huu atakuwa Rais wa aina gani? Hilo tu. Miaka 5 ya JPM nchi hii na Watu wake wamebadilika mitazamo yao kiasi kikubwa sana. Analijua hilo ama yuko zama za bunge la Katiba mpya na mitazamo ya Speed and Standard-rip
 
Kama kuna kitu cha kipuuzi na kijuha kilifanywa na utawala wa mwendazake ni huu ukuta.

Labda kama alijenga kudhibiti vibaka...eneo ambalo tulipigwa vibaya kwenye madini ni mikataba mibovu tuliyoingia na wapigaji na madalali nje ya nchi.

Kwa tech ilivyo advance haikuwa sahihi kabisa kujenga ule ukuta
Kuna mwanasiasa amesema kuwa kiongozi aliyetutoka alikuwa SHUJAA ALIYEPITWA NA WAKATI

Nia alikuwa nayo njema na rasilimali zetu lakini mbinu alizotumia kuzipambania rasilimali zetu ni za kizamani!
 
Pamoja na kuwepo kwa Underground Tunnels za kutosha lakini haijawazuia wamarekani kujenga Ukuta kati yake na Mexico...

Kitaalam tunasema risk can never be eliminated, it can only be reduced to an acceptable level...Ujenzi wa ukuta haukua intended kumaliza tatzo la utoroshaji wa Tanzanite bali kupunguza ukubwa wa tatzo.

Tunapojicheka kwa kujenga ukuta basi ni bora tuwacheke na Wamarekani pia..
ni hilo tu ndugu zangu.
 
Siwezi kubishana na Mh Rais ila na bishana na wapambe nuksi walio mfanya asema siku za maombolezi ni 14 wakidhani ni kumkomoa marehemu kumbe Kikatiba ni siku 21 zilizoisha jana.

Wanao mdanganya Mh Rais kuwa baadhi ya wafanyabiashara walioingia kwenye mshikemshike wa kudaiwa lodi kimaguvu na kimabavu bila kutumia akili ni watakatifu kuliko malaika wa Mungu wa Mbinguni na wamedhulumiwa jasho lao. Hivi huyo Mfanyabiashara aliye kuja na private jet kutaka kuyatengeneza mambo ya kodi akazenguliwa na kuondoka ni nani? Mbona hatajwi jina jamii ikmjua huyu mfanyabiashara mtakatifu.
Hapa hatuangalii watakatifu wala mashetani.., tunaangalia haki, utu na sheria, hata kama ni majambazi kuna taratibu za ku-deal nao.., sababu hata huyo mtumia mabavu na maguvu ni myanganyi tu.., Two Wrongs does not make a Right...
 
Unajua mtu kama hujui kitu ni bora unyamaze.hapo aliyekusimulia kakulisha uongo mtupu
 
Habari Wakuu,

Madam President anasema pamoja na liukuta likuubwa na ulinzi wa mabunduki wa JWTZ (na makamera) "MADINI YANATOROSHWA KAMA KAWAIDA CHINI KWA CHINI"

Hili limenikumbusha maneno ya mchimbaji mdogo wa madini hayo alipokuwa anatupa visa vya utoroshwaji madini machimboni.

Ilikuwa ni siku chache baada ya kuzinduliwa Ukuta wa Mirerani, mimi nikamwambia umejengwa ukuta sasa utoroshwaji umefika mwisho.

Cha kunishangaza jamaa alicheka sana!

Akaniambia kuwa kwenye machimbo huwa kila mtu ana njia yake anayopita akichimba huko chini hivyo ukuta ule ni kituko tu kwani hizo njia zinatoka nje ya ukuta kupitia chini kwa chini bila walinzi kuwa na habari.

Naona ndio wanaligundua hili leo.

Ushauri wangu: Kwenye ulinzi wa rasilimali zetu kama madini Serikali isijikite tu kwenye bunduki za wanausalama, ijenge urafiki na ushirikiano na wachimbaji hasa wadogo itajua siri nyingi za utoroshwaji madini.
Tangu lini Chadema wakaitakia mema ccm hadi wajipe kazi ya kumsifia rais Samia?.

Kazi ya kumsifia rais Samia ni ya MATAGA siyo ya chadema
 
Ni hivi.. umezungushwa ukuta sawa, lakini uchimbaji huhusisha utafutaji wa mali mielekeo tofauti tofauti chini kwa chini hivyo kuzaa mahandaki marefu ambayo yanavuka usawa wa ukuta umbali mrefu tu.. sasa kama unataka kutoroshea hukohuko unashindwa?
Hujui kitu ww unaropoka tu
 
Siwezi kubishana na Mh Rais ila na bishana na wapambe nuksi walio mfanya asema siku za maombolezi ni 14 wakidhani ni kumkomoa marehemu kumbe Kikatiba ni siku 21 zilizoisha jana.

Wanao mdanganya Mh Rais kuwa baadhi ya wafanyabiashara walioingia kwenye mshikemshike wa kudaiwa lodi kimaguvu na kimabavu bila kutumia akili ni watakatifu kuliko malaika wa Mungu wa Mbinguni na wamedhulumiwa jasho lao. Hivi huyo Mfanyabiashara aliye kuja na private jet kutaka kuyatengeneza mambo ya kodi akazenguliwa na kuondoka ni nani? Mbona hatajwi jina jamii ikmjua huyu mfanyabiashara mtakatifu.

dangote
 
Uweze kujenga ukuta usiweze kufuatilia njia za chini kwa chini. Nyie ni watu wa ajabu mwalidharaulisha na kulifedhehesha jeshi letu la JWTZ mbele ya jamii kwa tamaa zenu za madaraka ya kisiasa. Chagueni nini cha kuongea basi. CDF na team nzima ya ulinzi na usalama iwajibishwe kwa uzembe huu mnaotuaminisha.
Nguvu nyingi akili kisoda, ndio awajibishwe.
 
Inasikitisha kusikia kua hata taarifa za kutoroshwa madini tumekuja kuzipata baada ya kifo cha mwendazake
Ilikuwa ni dhambi kubwa kiasi gani kuongea ukweli kwenye utawala uliopita?
Hotuba ya mama ya jana unaweza kuchukulia mkopo benki. Ni hotuba ya karne!
 
Hapa hatuangalii watakatifu wala mashetani.., tunaangalia haki, utu na sheria, hata kama ni majambazi kuna taratibu za ku-deal nao.., sababu hata huyo mtumia mabavu na maguvu ni myanganyi tu.., Two Wrongs does not make a Right...

Wakati wanadhulumu kodi za Watanzania wao walitumia haki, utu na sheria ipi?
 
Huyu sijui style za deals zake ingawa najua hulka ya rushwa ya Wanigeria walio wengi. Hivyo siwezi kumzungumzia. Lakini si amini mfanyabiashara mkubwa kama huyu atendewe hivyo tunavyo taka kuaminishwa bila ya sababu ya maana. Na amini muda utatupa majibu sahihi kwa vile watuhumiwa hawatakaa kimya watataka kujisafisha.
 
Back
Top Bottom