Utolewaji wa Vitambulisho vya Taifa Usioridhisha

Waziri Simbachawene alivishusha thamani hivyo vitambulisho...
Sidhani kama vina umuhimu ukiachilia mbali kwenye usjili wa line ya simu... Kwingineko unapewa options ya vitambulisho vya kutumia!
 
Tangu lilipoanza zoezi la utolewaji wa vitambulisho vya Taifa mwaka 2012/13, ni wananchi 5,621,350 tu ndio waliopata vitambulisho vya Taifa sawa na asilimia 26 ya wananchi 21,692,122 walioandikishwa NIDA hadi kufikia Juni, 2020.

Zoezi la usajili na utoaji wa vitambulisho vya Taifa kwa wananchi, linaathiriwa na sababu zifuatazo:
a) Mwaka 2016/17 Serikali iliagiza vitambulisho vya taifa viwe na saini ya mwenye kitambulisho, hatua ambayo ilipelekea uwezo wa mashine katika uzalishaji vitambulisho kushuka kutoka vitambulisho 3,168,000 hadi vitambulisho 1,584,000 kwa mwaka.

Kutokana na kuweka saini katika vitambulisho pamoja na kutokuwepo kwa matengenezo ya mashine za kuzalisha vitambulisho imepelekea NIDA kuzalisha idadi ndogo ya vitambulisho kulinganisha na uwezo wa mashine zilizopo.

b) Ufinyu wa idadi ya watumishi katika ofisi za Wilaya: CAG alibaini, asilimia 38 ya Wilaya 150 zilikuwa na watumishi watatu wakati asilimia 62 zilikuwa na watumishi 2. Kwa kila Wilaya kunatakiwa kuwe na watumishi kuanzia watatu wanaofanya utambuzi, usajili na ugawaji wa vitambulisho lakini imekuwa kinyume na utaratibu wa NIDA.

Mfano, Halmashauri ya Wilaya za Mbarali, Malinyi, Sumbawanga, Namtumbo, Itilima na Momba kila Halmashauri ina mtumishi mmoja tu anayefanya zoezi la usajili na utoaji wa vitambulisho.

c) Kutokutumika kwa Mashine mbili zenye thamani ya TZS 10.05 bilioni zilizokuwa na uwezo wa kutoa vitambulisho 19,008,000 kwa mwaka ingawa watumishi wanne walipewa mafunzo ya kutumia mashine hizo. d) Uchapaji mdogo wa vitambulisho ikilinganishwa na wingi wa wananchi walioandikishwa
Binafsi naamini kuna ufisadi. Kuna interest group hawataki watanzania wawe na vitambulisho vya taifa kwa hivyo tunapigwa vita. Bila juhudi ziada zoezi litashindikana na huku tumepoteza fedha nyingi. Hebu fikiri tangu tumeanza miaka zaidi ya kumi watu 5m tu katika idadi ya watu wazima kama millioni 25 ndio wamepewa vitambulisho. Mtu anaomba kitambulisho anasubiri toka kijana hadi anazeeka hapati. Hapo kuna hujuma.
 
Back
Top Bottom