UTI sugu kwa wanawake

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
573
2,553
UTI ni ufupisho wa maneno Urinary Tract Infection, au kwa kiswahili ikiwa ni maambukizi ya mfumo wa mkojo ambao huhusisha figo, kibofu cha mkojo, mrija wa mkojo pamoja na mrija unao unganisha figo na kibofu cha mkojo.

3D77CBA1-4A1D-416A-BCEA-0257F374A3E5.jpeg


Maambukizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria jamii ya E. coli, lakini katika mazingira machache fangasi na virusi wanaweza kuwa chanzo cha maambukizi haya.

Dalili zake
  • Kupatwa na maumivu yanayochoma wakati wa haja ndogo
  • Kujisaidia haja ndogo mara kwa mara isiyotoa mkojo mwingi
  • Kujisaidia mkojo mweusi au ulio na chembechembe za damu na harufu kali
  • Maumivu ya nyonga
  • Uchovu, Homa na kutapika
  • Maumivu ya sehemu ya chini ya tumbo
Kwanini UTI hujirudia sana kwa wanawake kuliko wanaume?
Wanawake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua ugonjwa huu pamoja na kujirudia mara kwa mara kwa kuwa mrija wa mkojo huwa ni mfupi sana tofauti na wanaume, pia tundu la uke huwa karibu na sehemu ya haja kubwa hivyo ni rahisi kwa bakteria kutoka kwenye choo kuingia ukeni.

Pia, matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kemikali kali kusafishia via vya uzazi, kufikia umri wa ukomo wa hedhi pamoja na ujauzito ambao hubana kibofu cha mkojo na kupunguza ufanisi wake kwenye kutoa mkojo wote huwa ni baadhi ya sababu zinazoongeza uwezekano wa wanawake kuugua ugonjwa huu kuliko wanaume.

Kinga
Kuna baadhi ya njia zinazoweza kutumika kujikinga na tatizo la UTI ya kujirudia. Mfano wa njia hizo ni-
  • Kunywa walau lita 2 za maji kila siku
  • Kutokuvaa nguo za ndani zinazobana sana
  • Kuvaa nguo za ndani zilizotengenezwa kwa pamba asilimia 100
  • Kutumia juisi za matunda mara kwa mara
  • Kuacha mazoea ya kuvaa nguo za ndani mbichi
  • Kusafisha via vya uzazi kutoka mbele kwenda nyuma (frontal to back wiping) baada ya haja kubwa na wakati wa kuoga ili kuzuia bakteria wasiingie kwenye uke kutoka sehemu ya haja kubwa
  • Kwenda haja ndogo kila baada ya kushiriki tendo la ndoa
  • Kuacha tabia ya kutunza mkojo kwa mda mrefu baada ya kuhisi haja ndogo.
Ugonjwa huu usipotibiwa vizuri unaweza kusababisha kuharibika kwa figo, hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa unapata tiba sahihi pamoja na kuzuia maambukizi ya kujirudia kila mara.

Chanzo: CDC/ Womens Health/ Mayo Clinic
 
Back
Top Bottom