Uteuzi wa Makonda na hatma yake ndani ya Chama

Kelele ni nyingi na shahuku ni kubwa lakini maneno yangu ni machache;

[emoji419]Makonda hatakuwa na wakati mzuri wakati huu ambapo kundi la Msoga lina nguvu ndani ya CCM na Serikali. Kundi la Msoga ni kundi la Wazee wakongwe, wenye nguvu ndani ya CCM, na pia wenye majeraha waliyopatiwa wakati wa Magufuli.

Pia ni kundi lenye vijana wenye ndoto za kushika madaraka makubwa kuliko waliyonayo sasa, kupata/kupora fedha nyingi zaidi ya walizonazo sasa, na zaidi wanadharau kubwa kwa watu wanaowaona si wa kundi lao. Makonda atapaswa kurudia enzi zake za kulamba viatu vya kina Ridhiwani Kikwete, au awe mpole na kutojihusisha sana na mambo ya watu.

Ubabe, Kiburi na Jeuri zake hataweza kuziishi kwa sasa kwa kuwa yeye si kijana wa kundi hilo. Na zaidi hana mahusiano mazuri na kundi hilo lenye nguvu.

[emoji419]Rekodi yake ya kupora mali kwa wafanyabiashra, kuwadharau na kuwakandamiza watu wa chini yake - ambao hawakuwa na nguvu hata ya kulalamika enzi za Magufuli, inamuweka kwenye nafasi ya kuwa mtu wa kujitafakari sana kwa kila atua anayopiga.

Makonda aliwahi kumuonesha dharau hadharani Bw. Daniel Chongolo wakati yeye Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam na Chongolo akiwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni.

[emoji419]Makonda ni mtoto wa kundi lililotengwa kisiasa wakati huu. Amerudishwa ili kupunguza uwezekano wa uasi ndani ya CCM lakini je, tasaidia kitu? Kundi maarufu la Wendazao, ambalo nguvu yake kubwa ni wingi wa kura za Mkutano Mkuu wa CCM, limekosa nguvu za kisiasa ndani ya CCM baada ya kundi la Msoga kushika hatamu.

Mabadiliko ya mara kwa mara kwenye baraza la Mawaziri yamezingatia makundi haya mawili; Msoga na Wendazao. Mara nyingi kundi la Msoga limeibuka kidedea, kwa kupewa wizara nyingi na nyeti.

Kwahiyo Makonda atakuwa akifanya kazi kama mwakilishi wa kundi la Wendazao, wakiongozwa na kundi hasimu la Msoga.

Hatatakiwa kwenda kinyume na Msoga ili aendelee kubaki kwenye hiyo nafasi, na hapo itampasa kufanya kazi kwa upole na adabu - kinyume na haiba yake ya kiburi na dharau.

Sisi kazi yetu ni kuchambua!
Nawasilisha
Dr. Chris Cyrilo.

Mkuu umefanya uchambuzi mzuri sana, nakuunga mkono. Na kuongezea kuwa kiburi na dharau za Makonda hutokana na anayemtuma.
 
Nadhani uteuzi huu ni dalili nyingine ya kuwepo mpasuko baina ya Samia na msoga
gang. Time will tell. Kuna kundi la tatu

Mkuu hakuna mpasuko, ila ni mkakati maalum wa kufuta kundi la Mwendazake ifikapo na baada 2025!
 
Originally Bashite ni MSOGA GANG, alilewa tuu madaraka. Ametubu na ndo maana karudishwa kundini

Mkuu Msamaha bado, pale alipo anatembea na kitanzi cha usaliti na maovu/ukatili aliowafanyia wenye rimoti ya sasa na watu mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwenye siasa. Akijifanya mjanja tu wanaondoa stuli miguuni!
 
Kwa kweli inashangaza sana mtu ambaye ametumikia madaraka yake mabaya akiwa kiongozi unamteua wa nini? Kwanini tu-recycle watu kama hawa ambao watakuwa liability katika chama chako?

Mama ana tatizo katika uteuzi wa watu wake.
 
Kelele ni nyingi na shahuku ni kubwa lakini maneno yangu ni machache;

[emoji419]Makonda hatakuwa na wakati mzuri wakati huu ambapo kundi la Msoga lina nguvu ndani ya CCM na Serikali. Kundi la Msoga ni kundi la Wazee wakongwe, wenye nguvu ndani ya CCM, na pia wenye majeraha waliyopatiwa wakati wa Magufuli.

Pia ni kundi lenye vijana wenye ndoto za kushika madaraka makubwa kuliko waliyonayo sasa, kupata/kupora fedha nyingi zaidi ya walizonazo sasa, na zaidi wanadharau kubwa kwa watu wanaowaona si wa kundi lao. Makonda atapaswa kurudia enzi zake za kulamba viatu vya kina Ridhiwani Kikwete, au awe mpole na kutojihusisha sana na mambo ya watu.

Ubabe, Kiburi na Jeuri zake hataweza kuziishi kwa sasa kwa kuwa yeye si kijana wa kundi hilo. Na zaidi hana mahusiano mazuri na kundi hilo lenye nguvu.

[emoji419]Rekodi yake ya kupora mali kwa wafanyabiashra, kuwadharau na kuwakandamiza watu wa chini yake - ambao hawakuwa na nguvu hata ya kulalamika enzi za Magufuli, inamuweka kwenye nafasi ya kuwa mtu wa kujitafakari sana kwa kila atua anayopiga.

Makonda aliwahi kumuonesha dharau hadharani Bw. Daniel Chongolo wakati yeye Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam na Chongolo akiwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni.

[emoji419]Makonda ni mtoto wa kundi lililotengwa kisiasa wakati huu. Amerudishwa ili kupunguza uwezekano wa uasi ndani ya CCM lakini je, tasaidia kitu? Kundi maarufu la Wendazao, ambalo nguvu yake kubwa ni wingi wa kura za Mkutano Mkuu wa CCM, limekosa nguvu za kisiasa ndani ya CCM baada ya kundi la Msoga kushika hatamu.

Mabadiliko ya mara kwa mara kwenye baraza la Mawaziri yamezingatia makundi haya mawili; Msoga na Wendazao. Mara nyingi kundi la Msoga limeibuka kidedea, kwa kupewa wizara nyingi na nyeti.

Kwahiyo Makonda atakuwa akifanya kazi kama mwakilishi wa kundi la Wendazao, wakiongozwa na kundi hasimu la Msoga.

Hatatakiwa kwenda kinyume na Msoga ili aendelee kubaki kwenye hiyo nafasi, na hapo itampasa kufanya kazi kwa upole na adabu - kinyume na haiba yake ya kiburi na dharau.

Sisi kazi yetu ni kuchambua!
Nawasilisha
Dr. Chris Cyrilo.
Huyu watakuja kumkolimba tu na kiherehere chake
 
Enyi team Mbowe na Chadema!

Muacheni Makonda atimize wajibu wake.

Mlikwisha jaribu kumuangamiza sana!

Mmemuombea mabaya mara nyingi sana ila mkasahau Mungu ndie Muweza wa yooote!
Chadema wanayo kazi ya kufanya wala hawana time na huyo zero brain, ila ***** ***** zote ziko huku huko CCM,uteuzi huu umeleta tifu kubwa tu. Ni suala la muda tu.
 
Nadhani uteuzi huu ni dalili nyingine ya kuwepo mpasuko baina ya Samia na msoga
gang. Time will tell. Kuna kundi la tatu
Nakumbuka sana ile kauli ya JK kwenye mkutano mkuu wa CCM kuwa mgombea wa CCM 2025 ni Samia 'labda kama mambo yakiharibika sana'.
 
Makonda alikuwa kiongozi wa kundi la wasiojulikana.

Enzi za mwenda kuzimu makonda aliuwa watu wengi sana
Handwork yake hii
1679652251550.jpg
 
Mkuu Msamaha bado, pale alipo anatembea na kitanzi cha usaliti na maovu/ukatili aliowafanyia wenye rimoti ya sasa na watu mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwenye siasa. Akijifanya mjanja tu wanaondoa stuli miguuni!
Unamaanisha wamemuweka kwenye kilengeo
 
Rais Samia amechanganyikiwa kwenye hili. Repercussions zake ni mbaya sana. Kuna methali inasema "adui mwombee njaa"

Hapa naona maadui wa Samia wamefanikiwa kumuombea NJAA. Makonda hakufaa kurudi kwenye utumishi wa chama wala Serikali bali alipaswa kuwa gerezani tu. Hii ni DHIHAKA kubwa kwa Watanzania

Ila iko siku Paul Makonda ataingia tu gerezani na kutumikia kifungo kwa maovu yake
Gerezani kwa kosa gani?
 
Gerezani kwa kosa gani?
Makosa ya Mokonda mengi sana; uvamizi wa clouds media, kumteka Roma, kumteka Mo Dewji, kumshmbulia Tundu Lissu na kumpoteza Ben Saanane
 
Kelele ni nyingi na shahuku ni kubwa lakini maneno yangu ni machache;

[emoji419]Makonda hatakuwa na wakati mzuri wakati huu ambapo kundi la Msoga lina nguvu ndani ya CCM na Serikali. Kundi la Msoga ni kundi la Wazee wakongwe, wenye nguvu ndani ya CCM, na pia wenye majeraha waliyopatiwa wakati wa Magufuli.

Pia ni kundi lenye vijana wenye ndoto za kushika madaraka makubwa kuliko waliyonayo sasa, kupata/kupora fedha nyingi zaidi ya walizonazo sasa, na zaidi wanadharau kubwa kwa watu wanaowaona si wa kundi lao. Makonda atapaswa kurudia enzi zake za kulamba viatu vya kina Ridhiwani Kikwete, au awe mpole na kutojihusisha sana na mambo ya watu.

Ubabe, Kiburi na Jeuri zake hataweza kuziishi kwa sasa kwa kuwa yeye si kijana wa kundi hilo. Na zaidi hana mahusiano mazuri na kundi hilo lenye nguvu.

[emoji419]Rekodi yake ya kupora mali kwa wafanyabiashra, kuwadharau na kuwakandamiza watu wa chini yake - ambao hawakuwa na nguvu hata ya kulalamika enzi za Magufuli, inamuweka kwenye nafasi ya kuwa mtu wa kujitafakari sana kwa kila atua anayopiga.

Makonda aliwahi kumuonesha dharau hadharani Bw. Daniel Chongolo wakati yeye Makonda akiwa RC wa Dar es Salaam na Chongolo akiwa Mkuu wa Wilaya wa Kinondoni.

[emoji419]Makonda ni mtoto wa kundi lililotengwa kisiasa wakati huu. Amerudishwa ili kupunguza uwezekano wa uasi ndani ya CCM lakini je, tasaidia kitu? Kundi maarufu la Wendazao, ambalo nguvu yake kubwa ni wingi wa kura za Mkutano Mkuu wa CCM, limekosa nguvu za kisiasa ndani ya CCM baada ya kundi la Msoga kushika hatamu.

Mabadiliko ya mara kwa mara kwenye baraza la Mawaziri yamezingatia makundi haya mawili; Msoga na Wendazao. Mara nyingi kundi la Msoga limeibuka kidedea, kwa kupewa wizara nyingi na nyeti.

Kwahiyo Makonda atakuwa akifanya kazi kama mwakilishi wa kundi la Wendazao, wakiongozwa na kundi hasimu la Msoga.

Hatatakiwa kwenda kinyume na Msoga ili aendelee kubaki kwenye hiyo nafasi, na hapo itampasa kufanya kazi kwa upole na adabu - kinyume na haiba yake ya kiburi na dharau.

Sisi kazi yetu ni kuchambua!
Nawasilisha
Dr. Chris Cyrilo.
Msoga wana nguvu ndani ya CCM wameshindwa kuzuia uteuzi wake, pathetic

Haya yanabaki kuwa ni maoni yako tu na wala sio uhalisia wenyewe
 
Makosa ya Mokonda mengi sana; uvamizi wa clouds media, kumteka Roma, kumteka Mo Dewji, kumshmbulia Tundu Lissu na kumpoteza Ben Saanane
Una ushahidi? Kwa akili yako ya kwandumbe unadhani mo anaweza tekwa na makonda? Mrudishieni makonda nyumba yake mliyomdhulumu kabla jasho halijatiririka
 
Back
Top Bottom