UTEUZI: Rais Samia ateua Katibu wa Rais, Mnikulu na wasaidizi wake wa Uchumi, Sheria, Siasa, Diplomasia n.k

Poleni wale wa zamani, utamu wa kazi kupokezana....sio waliokuwa wanafikiri kuongezeana muda!
 
Ilipigwa chini
Hapana, alikuwa msemaji wa Familia.
tapatalk_1618642813282.jpg
 
Kweli kiswahili kimepanuka 'mnikulu' ndiye mtu gani hapo Ikulu
Anaenunua mashuka,mapazia,vikombe na sahani na vitunguu vya ikulu ndio mnikulu

Yaani kila kitu mle ndani yenye ndio mnunuzi yaani kwakifupi yeye ndio watchdog mkuu wa samani za madikodiko ya ikulu
 
With all due respect madame President, Mbona wasaidizi wengi?mi nirifikiri wasaidizi/washauri wako ni mawaziri?mbona unatengeneza mavyeo Mengi?
Hivi vyeo viliuwepo awamu zilizopita?
Mfano unawaziri wa mambo ya nje,anayesimamia diplomasia,harafu unateua Mshauri/msaidizi wa mambo ya kidiplomasia,sasa hapa ushauri wa nani utazingatiwa?
With all due respect Mkuu, jiongeze! Ofisi binafsi ya Rais sio Baraza la mawaziri. Inahitaji wasaidizi katika Maeneo anayoona yanafaa. Rais anafanyakazi zake ikulu
 
Bado sijaona mantiki ya kuambiwa hizi teuzi hadharani. Ni upuuzi mtupu.
Hivi kuna haja ya kuutangazia umma uteuzi wa wasaidizi wako binafsi wa ofisini ukiwa kama Rais?
Hivi watangulizi wake walifanya hivi?

Maana ukianza kufanya haya, itabidi kila msaidizi wa Rais awekwe wazi.
Kwa mfano; msaidizi wa mambo ya afya, michezo, biashara, kilimo, uvuvi, walemavu, Daktari wa Rais, Dereva wa Rais, Dressing designer wa rais, Mpishi wa rais nk.

Na pia siku ukimbadilisha msaidizi itabidi uutangazie umma.

Yoyote kwa yote hao wasaidizi unawaweka katika mazingira ya kufuatwa fuatwa na watu ili wawasaidie kufikisha ujumbe kwa rais au kufanya lobbying. Na wakipata kashfa itahusishwa na ofisi ya rais.

Binafsi naona hili ni kama jambo la kishamba, kutokujiamini na udhaifu wa rais Samia ambao ameuweka hadharani. Sio kila kitu kinapaswa kuletwa hadharani.

Watu hamna jema
 
Ngusa Samike ni mtoto wa Mzee Samike,aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Singida miaka ya 90,Mkuu wa mkoa akiwa Mwita Marwa enzi hizo.Dada yake na Ngusa anaitwa Leah Samike,ambaye sasa ni mwandishi wa habari.Sina uhakika kama Mzee Samike ana uswahiba na Jiwe!
Unamjua mama yake Ngusa?
 
With all due respect Mkuu, jiongeze! Ofisi binafsi ya Rais sio Baraza la mawaziri. Inahitaji wasaidizi katika Maeneo anayoona yanafaa. Rais anafanyakazi zake ikulu
Kilaza huyo achana nae. Yani mtu mzima hadi leo hajui kama Ikulu kunakuwa na hiyo Team. Hao tena wachache!

JF siku hizi sijui ina watu wa aina gani.
 
Bado sijaona mantiki ya kuambiwa hizi teuzi hadharani. Ni upuuzi mtupu.
Hivi kuna haja ya kuutangazia umma uteuzi wa wasaidizi wako binafsi wa ofisini ukiwa kama Rais?
Hivi watangulizi wake walifanya hivi?

Maana ukianza kufanya haya, itabidi kila msaidizi wa Rais awekwe wazi.
Kwa mfano; msaidizi wa mambo ya afya, michezo, biashara, kilimo, uvuvi, walemavu, Daktari wa Rais, Dereva wa Rais, Dressing designer wa rais, Mpishi wa rais nk.

Na pia siku ukimbadilisha msaidizi itabidi uutangazie umma.

Yoyote kwa yote hao wasaidizi unawaweka katika mazingira ya kufuatwa fuatwa na watu ili wawasaidie kufikisha ujumbe kwa rais au kufanya lobbying. Na wakipata kashfa itahusishwa na ofisi ya rais.

Binafsi naona hili ni kama jambo la kishamba, kutokujiamini na udhaifu wa rais Samia ambao ameuweka hadharani. Sio kila kitu kinapaswa kuletwa hadharani.
Wewe utakuwa Mtu wa Chato inakuuma sana, Mzilankende alikuwa anateuwa miaka mitano mfululizo sasa Mama anapiga dekio
 
kwani mnikulu anatakiwa kuwa na cv gani? maana hiyo ni tittle kama ya kimila hivi
Sidhani hiyo nafasi kama inahitaji Professionalism anaweza kupewa hata muuza kahawa muhimu atambuwe majukumu yake ni yapi.
 
Sikuwahi kuzisikia kabla hizi teuzi kwa marais waliopita au labda nilipitwa.

1. Katibu wa Rais.
2. Msaidizi wa Rais, diplomasia.
3. Msaidizi wa Rais, nyaraka na ukalimani.
4. Msaidizi wa Rais, siasa.
5. Msaidizi wa Rais, maendeleo ya jamii.
6. Msaidizi wa Rais, uchumi.
7. Msaidizi wa Rais, sheria.

Je nafasi hizi zilikuwepo huko nyuma kabla na kwa majina tafadhali. Nawakilisha.
 
Back
Top Bottom