UTEUZI: Rais Samia amemteua Rais mstaafu, Dkt. Kikwete kuwa mkuu wa chuo UDSM kwa kipindi kingine cha Miaka 6

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Uteuzi huo utaanza Januari 17, 2022.

My take
Mwenye nacho ataongezewa, naye asiyenacho hata kidogo kile alichonacho atanyang'anywa

2022- Kazi iendelee

4137609A-CC4A-448E-9DA3-4D878EC46AFB.jpeg
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Uteuzi huo utaanza Januari 17, 2022.

My take

Mwenye nacho ataongezewa, naye asiyenacho hata kidogo kile alichonacho atanyang'anywa
Safi Sana Mama kaziiendelee
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Uteuzi huo utaanza Januari 17, 2022.
 
Baba kikwete hongera saaana!! pokea zaidi ya pongezi kutoka kwenye sakafu ya Moyo wangu!!! unastahili mnooooooo!!! ongezewa hata miaka mia bwana weee!! ila tatizo bana baada ya kustaaf hatuonani kiviile!

yaani umekuja huku south hukunitafuta! au ratiba ilibana mkuu, na wewe ndo chanzo cha mimi kufika huku tutafutane bana weee!! usijali we jitahidi tu siku nyingine ukija bana!!! si unajua haturuhusiwagi kuwasogelea lkn ntakupa number yangu in box tukutane huko!!
 
Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita.

Uteuzi huo utaanza Januari 17, 2022.

My take
Mwenye nacho ataongezewa, naye asiyenacho hata kidogo kile alichonacho atanyang'anywa

2022- Kazi iendelee

View attachment 2064221
Ahakikishe sasa ndani ya miaka hii 6 mingine chuo cha Udsm muchas-Mbeya kinajengwa na hospital yake ya kufundishia.
 
Hongera mama kwa uteuzi makini. Hongera mzee jakaya kwa kuaminiwa tena!

Kazi inaendelea.
 
Arudishe Hospitali ya MLOGANZILA MUHAS nassoro tuwe na University Teaching Hospital nchini.
 
Hongera mchaguliwa hongera mchaguwaji ninawaombea kwa Allah akuhifadhini na akupeni busara na hekima ktk majukumu yenu
 
Kikwete alitakiwa atujengee chuo kikubwa Sana huku Baga moyo sijui alifeli wapi.
Hata Barabara ya kuunganisha wilaya ya kibaha na bagamoyo ameshindwa kujenga
 
Kikwete alitakiwa atujengee chuo kikubwa Sana huku Baga moyo sijui alifeli wapi.
Hata Barabara ya kuunganisha wilaya ya kibaha na bagamoyo ameshindwa kujenga
Usimlaumu sana mkuu, urais ni kazi kubwa kuliko tunavyofikir
 
Kwan inashindikana vipi kuwateuwa vijana waliograduate ambao wako mitaan badala ya kuwakumbatia hao wazee kila siku ambao akili zao zilishajichokea.

JIbu untakalopata ni kuwa wao wenye nchi wanaamini hakuna mwanachuo kijana wa kuaminika kupewa madaraka ama nguvu ktk siasa ama vyeo ktk ajira kwakuwa vijana wenyew hawa waliopo ni aina ya Wale wa mirinda nyeusi, wabetiji, waliokubuhu kwenye ulevi na ushenz wa kila aina, so acha wazee waendelee kulaa bata,.

Hayo si maneno yangu, ni maneno ya yule alieanzisha mfumo wa ukitaka ajira, onesha uzoefu wa miaka10
 
Hivi wakati wanachuo wahuni wanazidi kuongezeka hapo UDSM Jakaya amefanya nini kukabili wahuni hadi ateuliwe kwa mara nyingine kuwa mkuu wa chuo?
 
Back
Top Bottom