Uteuzi Hewa - Leo nimeteuliwa

Kabende Msakila

JF-Expert Member
Oct 7, 2020
554
1,000
WanaJF, Salaam!

Nawafahamisha kwamba leo tarehe 02 Desemba 2020 majira ya saa 17:50's nikiwa eneo fulani mkoani Kagera kuna simu fulani imenipigia - it seems wanafahamu details zangu za kikazi, kijamii, na kisiasa.

Mmoja kati ya wawili niolioongea nao amejitambulisha kwa jina la Kombo na kwamba yuko Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi Dar es Salaam. Mambo aliyonihoji ni haya yafuatayo:-

(a). Ameniuliza iwapo natumia kilevi au la - nimemjibu situmii kilevi chochote tangu kuzaliwa;

(ii). Ameuliza iwapo napenda kutoka na wanawake - nikamtaka ufafanuzi akasema iwapo napenda wanawake - nikamjibu nawapenda lkn si kwa kuwatumikisha kingono, kuwa na nyumba ndogo nk.

(iii). Ameuliza iwapo nilishiriki kura za maoni na kampeni za uchaguzi mkuu - nikamjibu nilishiriki, - ameuliza jimbo nikamdanganya na kumwambia Ivugo.

(iv). Akaniuliza iwapo nina familia - nikamwambia ninayo - akauliza wake wangapi nikamwambia mmoja.

Mwisho akaniuliza hobi yangu - nikamjibu briefly kuwa napenda sports and games.

Baada ya hapo akaniambia kuwa "endelea kuishi kama kiongozi ikiwa ni pamoja na kufika nyumbani mapema" na kuepuka migogoro na majirani. Pia akasema atarudi tena kunipa maelekezo kabla ya kukata simu akauliza iwapo niko tayari kufanya kazi yoyote nitakayopewa na kiongozi - nikamjibu kama ikiwa ktk taaluma yangu.

My take:
There is high possibility watu hawa wakawa wezi wa mitandaoni ambao hudanganya watu wengi kuhusu uteuzi. Kwa kuwa wamesema watarudi iwe leo au siku nyingine naendelea kusubiri maagizo watakayotaka kunipa - ntaendelea kukupeni taarifa. Lkn pia nakuwekea simu 06526697** ndiyo simu waliyotumia. Nimekuelezeni ili hili likifika kwenu msiibiwe kirahisi hivyo.

Msakila M Kabende
Bukoba - Kagera
02 Desemba 2020
 

sem2708

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,468
2,000
Tatizo kubwa watz tunaendaje kuweka details zetu nyingi sana mtandaoni. Huo ni mfano mmoja tu. Tuchukue tahadhari.
 

Mtende

JF-Expert Member
Sep 27, 2010
6,393
2,000
Matapeli wa mitandaoni wameamua kuja hadi kwenye teuzi!? Wana uthubutu sana kama ni kweli
TCRA imelala cha ajabu, ipo busy na waanaokosoa serikali badala ya kudeal na hawa wahalifu pamoja na wale wanaotuma sms za hiyo hela tuma kwa namba hii, bado kuna wale wengine wanaotuma msg za waganga maarufu, ..sijui shida iko wapi ila mamlaaka husika zimelala
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
2,375
2,000
Utakosa uteuzi kwa kuropoka kwako. Hao watu ni TISSccm wamekuona kwa jinsi unavyomsifia malaika jiwe wameamua kukupa kitengo.

Huo ndio ufanyaji kazi wa Idara kwa sasa.

Kama waliweza kumwambia mkuu kuwa Jokate anamegwa na yule dogo watashindwa kukupigia wewe kada mwenzao mpendwa???
 

jabulani

JF-Expert Member
Aug 1, 2015
4,608
2,000
Mimi waliniuliza maswali kadhaa mwishoni wakaniuliza kama nina kadi ya ccm nikawaambia sina wakakata simu.
 

Deceiver

JF-Expert Member
Apr 19, 2018
5,622
2,000
WanaJF, Salaam!
Nawafahamisha kwamba leo tarehe 02 Desemba 2020 majira ya saa 17:50's nikiwa eneo fulani mkoani Kagera kuna simu fulani imenipigia - it seems wanafahamu details zangu za kikazi, kijamii, na kisiasa...
It seems wanafahamu dtls zangu za kikazi, KIJAMII.

Halafu wanauliza kitu wanacho kijua. Kaka serikali ikikufanyia vetting wewe binafsi hawatakuuliza kitu. Hao watakua Ni walevi wenzio wamekumis klabu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom