Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Jana niliwasikiliza mawaziri wakiitetea serikali ambaye ni mwajiri wao katika hili suala zima la tozo zinazotesa wananchi.
Sikutegemea kipya kusema ukweli kutoka kwa Dr Mwigulu Nchemba zaidi ya kujenga hoja nyingi za aina ya maisha aliyokulia, anajiweka mbali na dhana ya utajiri unaosemekana ameupata katika awamu ya sita baada ya kukabidhiwa dhamana ya uwaziri.
Kusema amekulia katika familia ya watoto 11 na kusema kachunga ng'ombe ni kujaribu tu kujishusha mbele ya macho na akili za wanaomsikiliza.
Utetezi ulionifanya nifikirie kwa kina ni ule uliotolewa na waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Simbachawene. Yeye angalau alikuja na hoja zenye uungwana na zisizo na chembechembe ya mtu aliyelewa madaraka.
Pale aliposema kuwa ipo tofauti ya Awamu ya kwanza na ya pili na miaka hii ya sasa, aliweza kujenga hoja ya kueleweka. Kwamba kuna ongezeko kubwa la watu kitaifa. Na hao watu peke yake ni changamoto kuweza kutimiza mahitaji yao yote kama serikali.
Enzi zile tunasoma shule ya msingi na sekondari. Kulikuwa na utaratibu wa kuwalisha chakula cha mchana wanafunzi, nakumbuka miaka ile pale forodhani wanafunzi wa sekondari walikuwa wanapata chakula pale pale shuleni. Hapo hujaongelea utaratibu wa madaftari na vitabu kugawiwa bure.
Hayo yaliwezekana kutoka na uchache wa idadi ya watu wa Tanzania nzima kwa wakati ule, rasilimali angalau zilionekana kwenda sambamba na watu waliozitumia. Mtu akimaliza chuo kikuu ajira zinamsubiri tena za uhakika.
Leo hii huwezi ukayafanya haya bila ya kuleta maneno na kutokueleweka miongoni mwa wanajamii hao hao. Tupo wengi na tunazidi kuongezeka idadi, siku zote wingi wa watu huja na faida ya taifa kuwa na uhakika wa rasilimali watu na humo ndimo wamo wataalam wa sekta mbalimbali na wateja wa biashara mbalimbali kubwa.
Lakini wingi wa watu hujaa na changamoto za rasilimali zisizotosha kutakiwa ziyaguse maisha ya kila mtu, vita ya kimawazo ndio huanzia hapo.
Hivyo sio haki kusema kuwa sisi tumekuwa maskini kulinganisha na awamu za kwanza na ya pili, hapana. Ukweli ni kwamba teknolojia zimepiga hatua na maisha yamerahisishwa sana kulinganisha na miongo iliyopita. Mtihani ni namna kila mmoja wetu anavyoweza kuguswa na huo urahisishwaji wa maisha kulingana na maendeleo ya kiteknelojia.
Serikali hata ikijitahidi kuhakikisha uwepo wa ajira mpya laki moja kila mwaka, kama kwa mwaka huo mmoja wanaoingia katika soko la ajira wakiwa wakihitajika kitaaluma ni laki tano, hapo wapo watu laki nne wanaotakiwa kuumiza vichwa ili waweze kuwa na maisha angalau yenye kufanana na yale ya binadamu wa kisasa.
Kama upo uwezekano wa kukuza sekta zisizo rasmi kupitia ujenzi na uimarishaji wa vyuo vya VETA, na hilo lifanyike kwani ndilo litakalopunguza ukosefu wa ajira angalau kati ya wale laki nne wanaobakia mtaani basi laki mbili na nusu wawe na maarifa mengine ya kupambana wenyewe mtaani.
Huwa naziangalia filamu za kinigeria, namna zinavyovutia na kuwa na ujumbe unaoishi siku zote. Nollywood wametengeza mastaa wa viwango vya kidunia, wanasifika kila mahali sinema zao zinapouzwa. Ukichunguza wale watengeneza filamu na waigizaji utagundua wengi wao ni watu waliokosa kazi rasmi za serikalini na kuamua kupambana kwa kujiajiri wenyewe.
Kwa Taifa lenye kufanya sensa ili kujua idadi ya watu wake, ambao kwa habari zisizo rasmi wanaweza kuzidi milioni 60, wasio na ajira wataendelea kuongezeka. Hivyo sekta kama filamu na zenyewe zipewe kipaumbele na wizara husika.
Kisiwe ni kipaumbele cha kisiasa, la hasha. Wenye kuweza kufaidika na sekta ya filamu ni wengi, wenye elimu za vyuo vikuu na wasio na kazi kama Nigeria kwa hapa Tanzania ni wengi pia. Serikali inajipangaje kuitumia sanaa ya uigizaji katika kupungua hii changamoto ya ajira. Hilo ni swali linaelekezwa kwa wizara yenye dhamana ya utamaduni na masuala ya sanaa.
Pia kuna suala la serikali kuutazama mpira wa miguu, una fursa nyingi sana zimejificha japokuwa baadhi yetu tunautazama tukiwa na mtazamo hasi. Samuel Eto'o amestaafu rasmi soka miaka kama kumi imepita lakini mpaka kesho ni balozi maalum ya mashirika makubwa ya UN, pamoja na Kanu na Drogba. Hawa watu wameingiza pesa nyingi kiasi gani katika mzunguko wa kiuchumi huko katika mataifa wanayotoka?.
Zipo habari za Obi Mikel nyota wa zamani wa Nigeria ambaye inadaiwa malori mengi yanayofanya biashara huko Lagos na Abuja mmiliki ni yeye, ametoa ajira kwa wanigeria wangapi?. ameingiza pesa kiasi gani katika mzunguko mzima wa Nigeria?. Nilimuelewa sana Mheshimiwa Rais SSH aliposema upo mpango wa kujenga academy pale Tanganyika Packers Kawe kuliko kupaacha pakichakaa tu. Ni sekta yenye kutengeneza mzungiko mpana sana wa pesa kama ikitiliwa maanani na kutochukuliwa poa tu.
Niliweza kumuelewa Waziri Simbachawene, kwamba maisha ya sasa yamerahisishwa sio kama yale ya simu za mezani za kuzungusha, sasa hivi unatumia vidole kwa kugusa tu kioo cha simu unakuwa umeshawasiliana na jamaa zako wa Marekani na Canada.
Nilimuelewa aliposema ipo changamoto ya mtu mmoja mmoja, ndio hivi vilio vya tozo kwa raia asiye na kipato halafu hicho hicho kidogo anachopata anapoamua kuweka benki au kumtumia rafiki yake anaona kinakatwa kodi.
Wingi wetu na ongezeko la watu huja na neema nyingi tu lakini huja pia na changamoto halisi. Niliweza kuielewa vizuri hoja ya Mheshimiwa Simbachawene.