Gembe
JF-Expert Member
- Sep 25, 2007
- 2,483
- 159
Ndugu wana Jamii wenzangu,
Ni muda mrefu toka nimeandika maada katika jukwaa hili la siasa na hii imetokana na kutigwa na shughuli za hapa na pale ila kila mara nimekuwa nikipita humu na kusoma michango ya wanajamii wanaochipukia. Nimekuwa nikiguswa sana na watu ambao wamekuwa wakiendelea kuchangia hapa toka kipindi kile bila kuchoka akiwamo Mzee Mwanakijiji na mkuu Invisible.
Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa uchaguzi wenye fundisho kubwa hasa kwa chama tawala,sababu imeleta changamoto kwa viongozi wote kuwa kama wasipotekeleza mambo ambayo wananchi wanayataka basi wananchi wameamua kuwaadhibu katika sanduku la kupigia Kura.Tumefuatilia majimbo mengi hasa ya mjini na kuona jinsi wananchi walivyokuwa na shahuku ya mabadiliko kuliko kipindi chochote toka taifa hili lipate Uhuru. Kupungua kwa ushindi wa kikwete toka asilimia zaidi ya 80 mpaka 61 inaonesha wanachi wanataka maendeleo zaidi na hawana mchezo katika hili.
Wakati ningali mdogo siku nikifeli somo ambalo nalimudu nilikuwa Napata mshtuko na kuweka mkakati wa kuweza kupata alama za juu zaidi. Mfano huu na baraza jipya ambalo limeteuliwa na Kikwete linaonesha kuwa ameamua kurudisha Imani kwa wananchi ambayo ndiyo wasahishaji (walimu).Hoja zangu nitazijenga bila kuangalia ukubwa wa baraza .
Barabara
Kitendo cha Mkuu kumteua Magufuli na kumpa wizara ambayo inagusa watanzania wengi huku kumenigusa kwa kuwa naamini kwa usimamizi wa magufuli kutaleta mabadiliko katika ujenzi wa barabara.Mtakumbuka wakati akiwa waziri wa Ujenzi aliweza kusimamia ujenzi wa barabara nyingi Tanzania.
Barabara ya kutoka Mwanza mpaka dar esa salaam sasa hivi ina rasmi na imebaki ya kutoka Mtwara mpaka dare s salaam ambayo nina uhakika Magufuli ataishughulikia na kuisha kabal ya mwaka ujao wa fedha. Kitendo cha kumteua Mwakyembe ambaye ni tite mark kutasaidia ufanisi katika wizara hiyo sababu mwakyembe ni aina ya watu ambo usipofanya vyema au kusikiliza ushauri wake ambayo una manufaa basi atakushtaki kwa wananchi. Hii ni mbinu nzuri na nina uhakika Mtwara-dar-Mwanza-Kigoma-Mbeya-Mtwara kutakuwa na barabara za rami.
TANROADS ambao wanasimia ujenzi wa barabara za mkoa ,sasa kazi imeanza rasmi na nina uhakika Yule Mrema mwisho wake umefikia kikomo kama asipoweza kubadilika.Hataweza kuhimili vishindo vya Magufuli na Mwakyembe.
Afya
Hapa napo rais amechagua watu ambao wanweza kufanya kazi bila kuchoka. Dr. Hadji anafamika waiz kwa kupenda kufganya kazi ambazo zinaonekana. Ni kiongozi mzuri na ninategemea kupitia malengo ya Millenia basi tutaona hospitali na zahanati nyingi zikijengwa na kupatiwa huduma bora. Wananchi wanahitaji hospitali na zahanati zenye madakatari na wauguzi ambao watawahudumia wanchi kwa bei nafuu. Hapa ningeshauri serikali kupitia mfuko wa bima ya afya waanze kujenga zahanati kila mkoa sababu wanapata pesa nyingi kutoka kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa serikali. Kutumia mfuko huu kutasaidia sana katika kuimarisha huduma za afya.
Uchumi
Kurudisha tume ya mipango kama mpangaji wa mipango ya serikali kutaongeza tija katika kulete amaendeleo ya haraka. Awamu iliyopita hakukuwa na sera ambazo unaweza kuzipiama na ndiyo maana ilikuwa ni vigumu kwa Jk kusema amefanya nini katika miaka mine iliyopita ukiachilia shule za kata. Suala la kilimo kwanza haikuwa sera rasmi bali kauli mbiu tu na hii ilisababisha kutokuwepo kwa mafaniko katika hili. Tume ya mipango itafanya akzi kubwa sababu itapanga nini kinatakiwa kufanywa katika wizara na ni matumaini yangu watakuwa wakifuatilia kama miradi imekamilika na kutoa ripoti. Ili kufanikisha hili ningemuomba rais aongeze wachapakazina wataaluma hodari toka katika vyuo mbalimbali nchini ili wafanye kazi kwa ukaribu na watendaji wa tume hii. Tume ina watu wengi ambao walikuwamo kwenye wizara ya mipango kipindi cha Mkapa ila kunahitajika damu mpya ambayo italeta Mabadiliko.
Elimu
Utaratibu mpya wa serikali wa kurudshia uendeshaji wa shule TAMISEMI ni mkakati sahihi katika kuhakikisha unapunguz amlolongo katika maendeleo ya Elimu. Zamani kila jambo lilikuwa linap[angwa na wizara alafu ndiyo wanapelekewa Halamshauri kwa utekelezaji. Kurudisha suala hili katika halamashauri litasaidia kutatua matatizo ya walimu na hata ujenziwa shule nyingi za serikali. Sitegemei kusikia halmashauri inashindwa kughalimikia chakula katika shule za boding. Suala linguine ambalo naliona litaleta mafanikio ni kuipitia upya bpdi ya mkopo na kuunda bodi yenye watu wenye sifa stahili ambao watasaidia katika kuleta Maendeleo.
Siasa
Katika kuhakikisha wanachi wanarudisha Imani rais ameweza kukata watu wasiofaa au waliokuwa wanatumia magazeti ili wapate madaraka. Kitendo cha kutowateua watu kama January, EL, Serukamba, Makala na wengine wengi waliotumia magazeti ni kuonesha wana ushawishi na nguvu ni cha kinungwana na ninafaa kuungwa mkono. Hii inonesga yupo tayari kujengea taifa la watu waadilifu ambao wako tayari kuleta mabadiliko. Na hapa naomba kumsisitizia mkuu aiswape watu ubunge kwa kuwa ni makada tu!
Naomba kutuimia fursa hii kumsihi sana na kumsisitiza kwa nguvu nyingu; asiwape madaraka wale wote ambao walikataliwa na wanchi katika uchaguzi kwa kuwa siyo viongozi wanaokubalika na wananchi. Itakuwa ni chukizo kuwapa madaraka ya aina yeyote ile sababu mtu ambaye hakubaliki,ana sifa mbaya mbele ya wanachi akipewa madaraka ya kuteuliwa ni dharau kwa wananchi.
Kwa msisitizo naomba asiwateue wafuatao kabisa ili kuonesha anakubaliana na mawazo ya wananchi Lau, Batilda, G. Mongella na Wengine wengi ambao hawajashinda katika Majimbo yao kutokana na kushindwa kutekeleza matakwa ya wananchi. Muda wa kuwapa vyeo ili kuwafuta machozi usiwe katika kipindi hiki ambacho wananchi wanataka mabadiliko.Nimewataja hao wachahce sababu wamekuwa wakisemwa semwa watapewa nafasi.. Mkuu do the needful!
Kwa miaka hii mitano nina uhakika kabisa kama Rais akiwa mkali kwa mawaziri wote, wakurugenzi na makatibu wakuu, akawa msikivu kwa wanchi, akasimamia maendelea basi miaka hii mitano mabadiliko yatatokea. Sisi kama wanachi tuna kazi kubwa ya kupiga kelele ili hawa wachezaji wacheze mpira mzuri. Tusikae kimya tukiona wanakosea bali tuwapigie kelele ili wafanye kile mnacho kitaka.
Hakuna mtu anyepingana na mimi miaka hii mitano inayokuja ni miaka ya mabadiliko na Mhe. Rais lazima asimamie mabadiliko na asisite kumuondoa yeyote Yule ambayo hatatoa ushirikiano!
Naomba kuwasilisha utetezi wangu na tujadili kwa hoja Nini kifanyike?