UTETEZI: Namuunga Mkono JK katika miaka mitano ijayo (2010-2015)

Gembe

JF-Expert Member
Sep 25, 2007
2,483
159
Ndugu wana Jamii wenzangu,

Ni muda mrefu toka nimeandika maada katika jukwaa hili la siasa na hii imetokana na kutigwa na shughuli za hapa na pale ila kila mara nimekuwa nikipita humu na kusoma michango ya wanajamii wanaochipukia. Nimekuwa nikiguswa sana na watu ambao wamekuwa wakiendelea kuchangia hapa toka kipindi kile bila kuchoka akiwamo Mzee Mwanakijiji na mkuu Invisible.

Uchaguzi wa mwaka huu umekuwa uchaguzi wenye fundisho kubwa hasa kwa chama tawala,sababu imeleta changamoto kwa viongozi wote kuwa kama wasipotekeleza mambo ambayo wananchi wanayataka basi wananchi wameamua kuwaadhibu katika sanduku la kupigia Kura.Tumefuatilia majimbo mengi hasa ya mjini na kuona jinsi wananchi walivyokuwa na shahuku ya mabadiliko kuliko kipindi chochote toka taifa hili lipate Uhuru. Kupungua kwa ushindi wa kikwete toka asilimia zaidi ya 80 mpaka 61 inaonesha wanachi wanataka maendeleo zaidi na hawana mchezo katika hili.

Wakati ningali mdogo siku nikifeli somo ambalo nalimudu nilikuwa Napata mshtuko na kuweka mkakati wa kuweza kupata alama za juu zaidi. Mfano huu na baraza jipya ambalo limeteuliwa na Kikwete linaonesha kuwa ameamua kurudisha Imani kwa wananchi ambayo ndiyo wasahishaji (walimu).Hoja zangu nitazijenga bila kuangalia ukubwa wa baraza .

Barabara
Kitendo cha Mkuu kumteua Magufuli na kumpa wizara ambayo inagusa watanzania wengi huku kumenigusa kwa kuwa naamini kwa usimamizi wa magufuli kutaleta mabadiliko katika ujenzi wa barabara.Mtakumbuka wakati akiwa waziri wa Ujenzi aliweza kusimamia ujenzi wa barabara nyingi Tanzania.

Barabara ya kutoka Mwanza mpaka dar esa salaam sasa hivi ina rasmi na imebaki ya kutoka Mtwara mpaka dare s salaam ambayo nina uhakika Magufuli ataishughulikia na kuisha kabal ya mwaka ujao wa fedha. Kitendo cha kumteua Mwakyembe ambaye ni tite mark kutasaidia ufanisi katika wizara hiyo sababu mwakyembe ni aina ya watu ambo usipofanya vyema au kusikiliza ushauri wake ambayo una manufaa basi atakushtaki kwa wananchi. Hii ni mbinu nzuri na nina uhakika Mtwara-dar-Mwanza-Kigoma-Mbeya-Mtwara kutakuwa na barabara za rami.
TANROADS ambao wanasimia ujenzi wa barabara za mkoa ,sasa kazi imeanza rasmi na nina uhakika Yule Mrema mwisho wake umefikia kikomo kama asipoweza kubadilika.Hataweza kuhimili vishindo vya Magufuli na Mwakyembe.

Afya
Hapa napo rais amechagua watu ambao wanweza kufanya kazi bila kuchoka. Dr. Hadji anafamika waiz kwa kupenda kufganya kazi ambazo zinaonekana. Ni kiongozi mzuri na ninategemea kupitia malengo ya Millenia basi tutaona hospitali na zahanati nyingi zikijengwa na kupatiwa huduma bora. Wananchi wanahitaji hospitali na zahanati zenye madakatari na wauguzi ambao watawahudumia wanchi kwa bei nafuu. Hapa ningeshauri serikali kupitia mfuko wa bima ya afya waanze kujenga zahanati kila mkoa sababu wanapata pesa nyingi kutoka kwa wanachama ambao ni wafanyakazi wa serikali. Kutumia mfuko huu kutasaidia sana katika kuimarisha huduma za afya.

Uchumi
Kurudisha tume ya mipango kama mpangaji wa mipango ya serikali kutaongeza tija katika kulete amaendeleo ya haraka. Awamu iliyopita hakukuwa na sera ambazo unaweza kuzipiama na ndiyo maana ilikuwa ni vigumu kwa Jk kusema amefanya nini katika miaka mine iliyopita ukiachilia shule za kata. Suala la kilimo kwanza haikuwa sera rasmi bali kauli mbiu tu na hii ilisababisha kutokuwepo kwa mafaniko katika hili. Tume ya mipango itafanya akzi kubwa sababu itapanga nini kinatakiwa kufanywa katika wizara na ni matumaini yangu watakuwa wakifuatilia kama miradi imekamilika na kutoa ripoti. Ili kufanikisha hili ningemuomba rais aongeze wachapakazina wataaluma hodari toka katika vyuo mbalimbali nchini ili wafanye kazi kwa ukaribu na watendaji wa tume hii. Tume ina watu wengi ambao walikuwamo kwenye wizara ya mipango kipindi cha Mkapa ila kunahitajika damu mpya ambayo italeta Mabadiliko.

Elimu
Utaratibu mpya wa serikali wa kurudshia uendeshaji wa shule TAMISEMI ni mkakati sahihi katika kuhakikisha unapunguz amlolongo katika maendeleo ya Elimu. Zamani kila jambo lilikuwa linap[angwa na wizara alafu ndiyo wanapelekewa Halamshauri kwa utekelezaji. Kurudisha suala hili katika halamashauri litasaidia kutatua matatizo ya walimu na hata ujenziwa shule nyingi za serikali. Sitegemei kusikia halmashauri inashindwa kughalimikia chakula katika shule za “boding”. Suala linguine ambalo naliona litaleta mafanikio ni kuipitia upya bpdi ya mkopo na kuunda bodi yenye watu wenye sifa stahili ambao watasaidia katika kuleta Maendeleo.

Siasa
Katika kuhakikisha wanachi wanarudisha Imani rais ameweza kukata watu wasiofaa au waliokuwa wanatumia magazeti ili wapate madaraka. Kitendo cha kutowateua watu kama January, EL, Serukamba, Makala na wengine wengi waliotumia magazeti ni kuonesha wana ushawishi na nguvu ni cha kinungwana na ninafaa kuungwa mkono. Hii inonesga yupo tayari kujengea taifa la watu waadilifu ambao wako tayari kuleta mabadiliko. Na hapa naomba kumsisitizia mkuu aiswape watu ubunge kwa kuwa ni makada tu!

Naomba kutuimia fursa hii kumsihi sana na kumsisitiza kwa nguvu nyingu; asiwape madaraka wale wote ambao walikataliwa na wanchi katika uchaguzi kwa kuwa siyo viongozi wanaokubalika na wananchi. Itakuwa ni chukizo kuwapa madaraka ya aina yeyote ile sababu mtu ambaye hakubaliki,ana sifa mbaya mbele ya wanachi akipewa madaraka ya kuteuliwa ni dharau kwa wananchi.

Kwa msisitizo naomba asiwateue wafuatao kabisa ili kuonesha anakubaliana na mawazo ya wananchi Lau, Batilda, G. Mongella na Wengine wengi ambao hawajashinda katika Majimbo yao kutokana na kushindwa kutekeleza matakwa ya wananchi. Muda wa kuwapa vyeo ili kuwafuta machozi usiwe katika kipindi hiki ambacho wananchi wanataka mabadiliko.Nimewataja hao wachahce sababu wamekuwa wakisemwa semwa watapewa nafasi.. Mkuu do the needful!

Kwa miaka hii mitano nina uhakika kabisa kama Rais akiwa mkali kwa mawaziri wote, wakurugenzi na makatibu wakuu, akawa msikivu kwa wanchi, akasimamia maendelea basi miaka hii mitano mabadiliko yatatokea. Sisi kama wanachi tuna kazi kubwa ya kupiga kelele ili hawa wachezaji wacheze mpira mzuri. Tusikae kimya tukiona wanakosea bali tuwapigie kelele ili wafanye kile mnacho kitaka.

Hakuna mtu anyepingana na mimi miaka hii mitano inayokuja ni miaka ya mabadiliko na Mhe. Rais lazima asimamie mabadiliko na asisite kumuondoa yeyote Yule ambayo hatatoa ushirikiano!

Naomba kuwasilisha utetezi wangu na tujadili kwa hoja Nini kifanyike?

 

.........................................
Siasa
Katika kuhakikisha wanachi wanarudisha Imani rais ameweza kukata watu wasiofaa au waliokuwa wanatumia magazeti ili wapate madaraka .Kitendo cha kutowateua watu kama January,EL,Serukamba,Makala na wengine wengi waliotumia magazeti ni kuonesha wana ushawishi na nguvu ni cha kinungwana na ninafaa kuungwa mkono.Hii inonesga yupo tayari kujengea taifa la watu waadilifu ambao wako tayari kuleta mabadiliko.Na hapa naomba kumsisitizia mkuu aiswape watu ubunge kwa kuwa ni makada tu!................................................


Binafsi naamin kuna mambo aliyofanya kikwete ambayo asiporekebisha yanapoteza kabisa imani ya kwake na pili yanatia shaka umakini wake.?


  1. JK CCM chairman ana tatizo la kuuma na kupuliza. Hana msimamo.
Jk Ni mwenyekiti wa CCM. Mwenyekiti wa chama na watu wake wa karibu wamepewa mdaraka na nguvu kikatiba(ya chama) kufanya baadhi ya maauzi kwa maslahi ya chama.

CRITIC:Kwa nini CCM ilimtoa Bashe na mwakalebela kugombea ubunge bila vyombo husika kuthibitisha wana kosa lakini wakashindwa kufanya hivyo kwa watu wenye tuhuma nzito zaidi kama Chenge na Mramba?

Serikali iliyowapeleka mahakamani Chenge na Mramba ni ya JK. ina maana mpaka serikali ya JK imewashataki imejiridhisha kuwa wana hatia. sasa kwa nini Chama kistumie rungu na uwezo wake kuonyesha JK na chama chake sio COMEDIAN
2. JK kama Baba wa familia ya rais . Hawezi kucontrol
Kama baba wa familia na rais JK aanatikiwa kuja familia yake inapata stahiki mbali mbali halali nyingi tu. Lakini alitakiwa ajue kuna baadhi ya faida zinakwenda na hasara.JK alitakiwa kutumia busara kuweka control kwa familia yake wasiibuke ghafla kisiasa ikiwezekana kuwaminya kisiasa akiwa madarakani. Binafsi naona ameshindwa ku control familia yake. Kwa nini asiwaambie washughulike na faida zilizopo mbele yao za mambo nyuma ya pazia i.e nje ya siasa. Huku kwenye siasa waje baadae???
3. Jk kama rais wa watanzania.kashindwa kutekeleza ahadi
Matumaini makubwa waliyokuwa nayo watanzaia wengi juu yake miaka mitano iliypita yamepotea kama mvuke. naamini ile kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtannzania hata yeye mwenyewe anaogpa na anaona aibu kuitamka.

Uchumi: Nina hakika yale madeni yote iliyolipa serikali ya mkapa yamekuwa negated. Wananchi juzi juzi kwenye bajeti walidanganywa kuwa bajeti yetu inajitegema kwa 40% lakini ukweli ni kuwa wahisani waligoma kutoa misaada Serikali ikakimbilia Kukopa. Iweje Norway agome kukupa msaada sababu ya ufisadi uende kukpa kwa libya useme umejitegemea????

Mgao wa umeme
: kwa miaka mitatu mfululizo kwenye hotuba zake anasema ni Changamoto. Changamoto gani inashindwa kukabiliwa miaka mitatu mfululizo.Mgao wa umeme Sio mafuriko, au tetemeko la ardhi.linalokuja ghafla.Wasomi wa kitengo cha Sera na mipango wanafanya kazi gani?

4.JK kama rafiki wa watu-
hawa ndo wanaomchimbia kaburi

Binafsi naona JK alikuwa ceremonial leader. Alitakiwa kutafuta wachapa kazi hasa ili nyota yake izidi kupanda lakini marafiki na washkaji aliwaweka karibu yake kumsaidia hawafanyi kazi yao

Sikatai lazima uchague watu unaowajua lakini lazima kuwe na clear line between kazi na urafiki sijui kama JK na Lowasa walikuwa wakikutana ofisini wanatofautisha mazungumzo ya Kikazi na kirafiki. His/ Her friend and close allies wameshindwa ku cover hata zile weakness zake.Hawafai

Akibadilika kwenye hayo atakuwa rais bora 2010-2015
 
I just don't buy any word that comes out of Kikwete's mouth! While falling into a temporal vegetative state at Jangwani, the same mouth kept pumping out an endless list of unplanned promises.
 
Watanzania sijui kama huwa tunatafakali na kufikiri. Tunapenda na kuenzi bla bla na kuremba ujinga ujinga! kinachonikera zaidi hata wale wenye uelewa mdogo hutumia jitihada kupumbaza wale wajinga. Pato la taifa linazidi kushuka kila kukicha, thamani ya shillingi inaporomoka. Mwingine anakurupuka toka kwenye nyumba ya tende na kuamua kudanganya kadamnasi eti we are on the right direction subiri flyovers Dar es Salaam kupunguza foleni, viwanja vya ndege kila mkoa wakati ATC ina ndege 3!!!! Meli kila kwenye mto ama ziwa, Bajaj kila zahanati, Kigoma kuwa DUbai, Mwanza kuwa California! na bla bla kama hizo lol. Kikwete ameshindwa tayari baraza lake la mawaziri ni kubwa mno utendaji utakuwa diluted na wale bora waziri ili kulipa fadhila.

Nchimbi, Mahanga Makongoro, Nagu, Lukuvi, Wasira, wana kipya kipi? Sawa Dr Mponda, Dr Magufuli, Prof Tibaijuka watafanya kazi nyanja zingine unapenda yawepo mazingaombwe tu?

Umasikini unaongezeka kila siku, tofauti ya matajiri na maskini inazidi kupanuka. Ufisadi na rushwa inazidi kuongezeka na kubarikiwa na uongozi wa kikwete, utawala wa sheria unakufa.

Hebu acheni ujinga hapa ebo! Gembe to hadithi zako za Abunuwas
 
Mkuu Gembe,

Ninakubaliana na mada yako pamoja na maoni yako. Lakini kuna baadhi ya maeneo nina mashaka nayo. Ni rahisi sana kuona kwa nje kwamba Baraza la Mawaziri kwenye baadhi ya Wizara Mkwere amefanya uteuzi unaofaa. Lakini swali la msingi ni hili, je, wameteuliwa ili watekeleze Ilani ya CCM na kutimiza ahadi za JK au kuna la ziada?

Moja, Wizara ya Ujenzi: Mkuu ameahidi barabara nyingi sana: Ninazokumbuka ni pamoja na Manyoni - Tabora - Kigoma; Tunduma - Sumbawanga - Mpanda; Mtwara - Tunduru - Songea; hizo ni zile kubwa, bado viporo vya kumalizia barabara ya Lindi - Mtwara na barabara ndogo ndogo alizoahidi kule Moshi na ile barabara ya kukatisha Hifadhi ya Ngorongoro, Serengeti mpaka Musoma. Barabara zote hizo ni kwa kiwango cha lami. Kwa miaka 5, hizo ni barabara nyingi sana. Bado kwenye wizara hiyo kuna viwanja vinne vya ndege. Je, Ilani na Ahadi za JK zitatimizwa chini ya Magufuli?

Mbili, Tume ya Mipango: Hii ilirudishwa nadhani miaka 2 iliyopita pale Dr. Mpango alipoteuliwa kuwa Katibu Mtendaji, lakini bado sijaona mafanikio/mabadiliko yoyote mpaka sasa. Siku zote kumekuwa na mgongano kati ya Tume ya Mipango na Wizara ya Fedha. Ndio maana kumekuwa na mara kuunganisha, mara kutenganisha. Ni rahisi sana kuandaa mipango, lakini kama Hazina haina nia ya kutekeleza mipango hiyo kwa kuwa siyo kipaumbele, then bado kuna tatizo na inaweza kuongeza msuguano na mwisho wa siku Tume ya Mipango wanakuwa frustrated maana kila wanachoandaa hakitekelezwi.

Tatu, Siasa: Mkuu wangu kama JK ana nia ya dhati ya kurudisha hadhi ya chama chake wananchi wamekuwa wakipiga sana kelele lakini sikio la kufa huwa halisikii dawa. How many times wananchi wamepiga kelele miaka 5 iliyopita? Kelele zilianza na uteuzi wa EL, zikaendelea na uswahiba wa RA, EL na JK, zikaja kwenye Richmond, zikaenda kwenye madini na mikataba yake mibovu. Magazeti yaliandika/pigia kelele mambo mengi sana, lakini ni JK huyu huyu aliyekuja na kauli kwamba kelele za mlango hazimnyimi usingizi, na wapambe wake ndio wa kwanza kufafanua kila anapotoa kauli za kejeri.

Nne, Wizara ya Maji; Hapa kuna deni kubwa sana kuanzia mijini mpaka vijijini na amesema ndani ya miaka 5, tatizo la maji litakuwa ni historia kila alikopita na kuambiwa maji ni tatizo. Ninasubiri kwa hamu hiyo miaka 5 ili tumkumbushe ahadi ya maji. Nina hakika maji litaendelea kuwa tatizo na waziri aliyetwishwa huo mzigo, ajiandae kubebeshwa lawama kwamba alishindwa ku-perform.

Tano, matatizo ya Ardhi; hapa ndipo kuna tatizo kubwa sana na tena la msingi maana linagusa wakulima ambao ndio wazalishaji wetu tunaowategemea. Akiwa Misenyi aliambiwa tatizo la ardhi, pia akiwa Mbalali, Kilosa, Mvomero, Korogwe na Handeni, kote huko aliambiwa matatizo ya Ardhi na hakutoa majibu ya kueleweka. Tatizo lililopo ni kwamba waliotangulia wameishafanya madudu sasa hawa wanaokuja wanabebeshwa mzigo wa kutatua madudu ambayo hayatatuliki. Mfano, kama ardhi imeishauzwa, unategemea waziri aliyepewa uwaziri, atafanya nini ili kurejesha ardhi hiyo? Je, hao wawekezaji wakisema watarudisha ardhi lakini kwa kuiuzia serikali kwa bei kubwa, si tutakuwa tunarudi kwenye mgogoro wa uuzaji wa nyumba za serikali?

Mwisho, Teuzi za watendaji wengine [RCs na DCs] na wakurugenzi wa halmashauri: Ninakubaliana na wewe kwamba wale wote waliokataliwa na wananchi hawatakiwi kupewa nafasi hizo. Lakini swali ni kwamba je hao ma-RC na ma-DC walio madarakani sasa hivi wana kidhi viwango vya kupewa hizo nafasi? Tatizo siyo kukataliwa na wananchi, tatizo ni namna hizo nafasi watu wanavyopewa kama zawadi na wengi wao wameshindwa kusimamia maendeleo kwenye mikoa na wilaya, na sometimes kumekuwa na conflict of interest kwa kuwa sioni mpaka wa majukumu ya Mkuu wa Wilaya na Mbunge. Kukishakuwa na mgongano kati ya hao wawili, wilaya lazima itazorota kimaendeleo na mwisho wa siku mtashindwa kujua ni nani hasa anastahili kubebeshwa lawama ya kuzorotesha maendeleo ya wilaya au jimbo husika.

NOTE: Tunapoelekea 2015, tukae mkao wa kula maana game ndio inaanza. Waliokuwa wanatarajia kuponywa majeraha yao, naona wametoneshwa majeraha yao na mtu akamwagia chumvi juu yake. Uchungu wake tutauona kwenye magazeti naona akina Balile na Muhingo Rweyemamu wameishaweka kalamu zao kwa mkao wa kueleweka ili kuanza mashambulizi rasmi.
 
Gembe,

Kuna msemo sisi Wanyamwezi wa Sikonge tunasema (nukonga vagosya) kwamba "Kununua paka kwenye gunia".

Mkuu, jitahidi uwe na subira ya kuangalia ndani kuna nini maana ukiondoka dukani.....

Miaka 5 ikiisha ndiyo ufungue gunia, utamkuta Paka wako na hapo tutaongea sasa.

Sasa hivi kusifia Paka wako mzuri sana na umenunua kwa sababu Muuzaji kamsifia au alikuwa kavaa vizuri na yuko ndani ya gari nadhifu, subiri ugonjwa wa moyo siku ukifungua gunia.
 
Kwanza wanaomtaja magufuli wanakosea sana . Wanamtandao wa JK wenyewe walishamchafua. Magufuli will not be the same again.He will try but we should not expect more than 50% of what he did in Mkapa's era.
 
Oh! mkuu Gembe ni baraza la mawaziri 2 ndio unaona jk ameshafanya kazi ya kukuridhisha? Aisee mitazamo yetu binadamu ipo tofauti kwa kweli.. Baada ya uchafu wote walioufanya ccm miaka yote leo unaona amefanya lililo la mbolea labda mimi mwenzenu napitwa na mengi naomba kujulishwa. Mabadiliko Tz. ni njozi za mchana kwa mtindo huu.
 
Bado kabisa hujafanikiwa kuniuzia mbuzi kwenye gunia.
Hata hivyo maelezo yako yana mpangilio mzuri lakini ndani yake yana harufu za ahadi za CCM
 
Gembe
Ulichosahau tu ni kuwa serikali inapatika baada ya chama kimoja cha siasa kupata ushindi, therefore chama kina nguvu kubwa na mafisadi wote ni wajumbe wa vikao muhimu vya chama vyenye maamuzi makubwa sana katika kuamua hatima ya taifa.

To me kilichoharibika Bongo ni mfumo na sio mtu mmoja mmoja, so njia pekee ya restoration ni kukipiga chini chama ili kiingie kingine na mfumo mwingine, Kama msingi ukiharibika mwenye haki afanye nini?
 
Bado kabisa hujafanikiwa kuniuzia mbuzi kwenye gunia.
Hata hivyo maelezo yako yana mpangilio mzuri lakini ndani yake yana harufu za ahadi za CCM

Mkuu Madela,

Katika mtilriko wangu hakuna sehemu ambayo nimeandika CCM,upeo wangu umeangalia nini taifa linahitaji kwa sasa bila kufuata ahadi nyingi alizozitoa Mwenyekiti.Kwa kuwa alishakuwa rais mie nanona ni bora tuanze kumshauri nini anatakiwa kufanya na kuwapa Muongozo sahihi kwa kuwa mkuli mwenyewe anapita jamvi hili na kusoma michango yetu.Nina uhakika hii miaka mitano atatusikiliza!
Oh! mkuu Gembe ni baraza la mawaziri 2 ndio unaona jk ameshafanya kazi ya kukuridhisha? Aisee mitazamo yetu binadamu ipo tofauti kwa kweli.. Baada ya uchafu wote walioufanya ccm miaka yote leo unaona amefanya lililo la mbolea labda mimi mwenzenu napitwa na mengi naomba kujulishwa. Mabadiliko Tz. ni njozi za mchana kwa mtindo huu.


Mkuu Pakawa heshima sana,Mawaziri vichwa wapo wengi sana kama Prof. Mbarara Mnyaa na kitwanga ambao wapo kwenye wizara ya sayansi na Teknoklojia.Hawa ni watendaji wa kisasa ambao wanajua dunia inahitaji nini hivyo natagemea mabadiliko makubwa sana katika nyanja za demokrasia.wapo wengi ila nitaandika zaidi katika makala yangu ambayo itakuwa ikionesha wasifu wa kila waziri ninayemfahamu ila kipindi hiki ambacho hatuna jinsi na rais wetu ndiye huyu basi tutoe ushirikiano.

NOTE: Tunapoelekea 2015, tukae mkao wa kula maana game ndio inaanza. Waliokuwa wanatarajia kuponywa majeraha yao, naona wametoneshwa majeraha yao na mtu akamwagia chumvi juu yake. Uchungu wake tutauona kwenye magazeti naona akina Balile na Muhingo Rweyemamu wameishaweka kalamu zao kwa mkao wa kueleweka ili kuanza mashambulizi rasmi.
Mkuu Keil,Malelezo yako yamekuwa msaada mkubwa tena..asante kwa angali na ushauri katika point zako tano uliziweka juu.Hawa kina muhingo na wenzake wanatakiwa waprint hizi na kuwapelekea mawaziri ili wafanya kazi.Nakuapia kwa siasa zilizo hivi sasa hawa hawana nafasi ya kuwapumbaza watanzania.

Nimeamua sasa hivi kusiammia na kuweka utaifa Mbele,Nitapaza sauti na kupiga kelele mpaka maendeleo yatokee..

BTW the line:Kitendo cha kuwarudisha klina Nchi ili kuwa ni lazima kidogo,hauwezi kuwa na baraza lenye watu wote wapya bila ya kuwa na watu wanaofaham,u siasa za ndani kidogo kama Nchi.Kuna mambo mengine ndani ya uongozi yanahitaji watu wa aina ya nchi.LA mahanga kwa kweli hata mie nina shaka na kauli anazotoa ila profile ya utendaji wake siijui kwa kweli.
 
Gembe
Ulichosahau tu ni kuwa serikali inapatika baada ya chama kimoja cha siasa kupata ushindi, therefore chama kina nguvu kubwa na mafisadi wote ni wajumbe wa vikao muhimu vya chama vyenye maamuzi makubwa sana katika kuamua hatima ya taifa.

To me kilichoharibika Bongo ni mfumo na sio mtu mmoja mmoja, so njia pekee ya restoration ni kukipiga chini chama ili kiingie kingine na mfumo mwingine, Kama msingi ukiharibika mwenye haki afanye nini?

Hapa unaangalia mfumo wa utendaji au mfumo upi?Haoni wewe unaweza kuwa mtu mzuri katika kupendkeza mfumo unaoona ni sahihi?Nilichokiona katika siasa za bongo na kwa muda mrefu kumekuwa na mlolongo katika kutoa uhuduma ila kama serikali ikiweza kurudisha mamlaka kwenye serikali za mitaa basi tutegemee mabadiliko.Yaani mafungu yawe yanakwenda moja kwa moja.

Ningekuwa mimi ndiyo Jk ningefuta vyeo vya wakuu wa wilaya na kubakisha wakurugenzi wa Halmashauri tu sababu hii itawap nguvu hawa watendaji na watakuwa na shauku ya kutekeleza matatizo ya wananchi.Hii haitoshi bali kuweka watu wenye elimu na vigezo katika kila halmashauri ili kuleta chachu ya mabadiliko..
 
Back
Top Bottom