Utendaji sifuri, kiinua mgongo 46 millioni kwa kila Mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utendaji sifuri, kiinua mgongo 46 millioni kwa kila Mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 20, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Date: 2/20/2010

  Kila mbunge kuvuna Sh46 milioni za kiinua mgongo

  *Ni asilimia 40 ya mishara yate ya miaka mitano

  Exuper Kachenje
  Mwananchi  KILA Mbunge ataondoka na zaidi ya Sh46milioni kama kiinua mgongo baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Julai mwaka huu.

  Bunge hilo litavunjwa baada ya mkutano wa bajeti unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa Agosti mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

  Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo mshahara wa kila mbunge kwa sasa anafikia jumla ya Sh1,921,000 kwa mwezi.

  Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, wabunge watalipwa fedha zao mara baada ya Bunge kuvunjwa.

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina wabunge 325, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakao lipwa na Bunge ni 276. Kwa mantiki hiyo jumla ya Sh12,724,704,000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa malipo ya wabunge hao, yatatolewa kwa mujibu wa sheria ya mafao ya viongozi wa kisiasa ya mwaka 1999 ambayo ilianza kutumika 2000.

  Kwa mujibu wa sheria hiyo, iliyotokana na marekebisho ya sheria ya awali ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986, kila mbunge atalipwa asilimia 40 ya mshahara wake alioupokea kwa kipindi chote cha miaka mitano.

  Marekebisho ya mishahara ya viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa yaliyofanywa Julai mwaka jana, yameonyesha kuwa, mbunge anapokea Sh1,921,000milioni kwa mwezi.

  Hata hivyo sheria imeeleza kuwa sio wabunge wote watakaovuna kiasi hicho cha fedha, kwa kuwa muda wao wa kuwa bungeni unatofautiana.

  Afisa mmoja mwandamizi katika ofisi ya Bunge ambaye hakutaka kutajwa gazetini alilidokeza gazeti hili jana kuwa wabunge watapata mafao hayo baada ya Rais Kikwete kulivunja Bunge.

  "Mimi si msemaji wa Bunge lakini, kwa kukusaidia tu fedha hizo zitalipwa baada tu ya rais kutangaza rasmi kulivunja Bunge.

  Wabunge watazikuta fedha hizo kwenye akaunti zao kati ya Julai na Agosti," alisema na kuongeza:

  "Malipo hayo yatafanywa kwa kuzingatia Sheria ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa ya mwaka 1999 iliyopo sasa, iliyoanza kutumika mwaka 2000. Sheria hiyo ilitokana na marekebisho yaliyofanywa kwa sheria ya awali, ambayo ni Sheria ya mafao ya viongozi maalum wa kitaifa ya mwaka 1986".

  Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah alilithibitishia Mwananchi kuwa malipo hayo ya kiinua mgongo yatafanyika kwa kutumia sheria hiyo baada ya bunge kuvunjwa.

  "Sheria iliyopo ndiyo itakayotumika na ndiyo itayoongoza kufanya malipo hayo. Sheria hiyo ni ya Mafao ya Viongozi wa Kisiasa ya mwaka 1999 iliyoanza kutumika mwaka 2000," alisema Dk Kashilillah.

  Alifafanua zaidi akiasema: "Malipo yanaweza kufanyika 'at either' (wakati wowote), kabla au baada ya kuvunjwa Bunge".

  Kuhusu kiinua mgongo kwa mawaziri na manaibu wao Kashilillah alisema sheria ipo wazi kuhusu viongozi hao na kueleza kuwa hawalipwi mishahara na Bunge bali serikali kupitia wizara husika.

  "Kuna mafao ya Bunge na serikali, sisi hatulipi mishahara ya mawaziri, bali ya wabunge. Mawaziri wanalipwa mishahara na serikali, sheria ipo wazi, ukiisoma imeweka wazi hilo," alisema Dk Kashilillah.

  Sheria hiyo imeainisha pia viwango vya malipo vya viongozi wa juu serikalini ikiwamo rais, makamu wake na waziri mkuu.

  Aidha, imewajumuisha mawaziri na manaibu wao, wakuu wa mikoa, wilaya, Spika wa Bunge na Naibu wake.

  Spika wa Bunge na naibu wake watapata kiinua mgongo cha kiwango sawa na rais mstaafu, lakini, watatofautiana kwenye baadhi ya mafao.

  Kwa mahesabu ya viwango vya mishahara yao, mawaziri na manaibu wao watuchukua jumla ya Sh2,658,768,000 kama kiinua mgongo chao.

  Mwaka uliopita serikali iliwaongezea mishahara viongozi wakuu wa nchi na viongozi wa kisiasa ambapo mishahara ya wabunge ilipanda kutoka Sh1,840,000 hadi 1,921,000 na naibu Spika kutoka Sh Sh2,080,000 hadi Sh2,172,000.

  "Viwango vya mishahara kwa viongozi wa serikali vinawekwa na serikali, mimi hainihusu hivyo siwezi kuthibitisha hilo. Nimesikia tu kama mlivyosikia ninyi," Katibu wa Bunge Dk Thomas Kashilillah aliliambia gazeti hili alipotakiwa kuthibitisha ongezeko hilo la mishahara mwaka jana.

  Hata hivyo, viwango hivyo vya mishahara, havijumuishi posho za vikao, mafuta ya gari na fedha za kujikimu ambapo sasa Mbunge mmoja anapata Sh135,000 kama posho kwa kikao kimoja cha Bunge ambayo pia mawaziri na manaibu hunufaika nayo.
   
 2. M

  Msharika JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 937
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tax payers are finished. We do not accumulate to break the viscious circle of the nation but of few angels(MPs). Then, what is the future of the nation? I ma completely confused.
   
 3. M

  M-Joka JF-Expert Member

  #3
  Feb 21, 2010
  Joined: Dec 13, 2007
  Messages: 308
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mimi natengeneza kikosi changu cha walalahoi tukamvamie mbunge wa jimbo letu mstaafu tuchukuwe haki yetu, ama uhae wake tunamuachia mwenyewe, lakini haki yetu ni yetu tu. Unyama, unyama tu!!!! Jimbo lipi???? tusiulizane kwa sababu humu ndani kila mtu ana la kwake na muda uliopo mpaka Agosti ni matayarisho ya kutosha.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Feb 21, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,880
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  I cry for my beloved country!! How can this be acceptable with so much poverty!!
  Fanya 46x300+ = 13.8 billion!!!! Hahaha....kweli tunataniana! Alafu kuna wabunge wanaojifanya kutetea haki na kujiita wapiganaji?!! Kwaheri....
   
 5. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #5
  Feb 21, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,014
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  (Photo taken in January 2010)

  Hivi hakuna chombo/watu wa kupinga uamuzi huu? Nadhani kuwa posho wanayopata wabunge wakiwa kazini inatosha kuwa kama kiinuua mgongo. Hawa wabunge pesa zao hazikatwi kwenye pension fund? Watoto wengi bado wanakaa chini madarasani, hakuna dawa za kutosha, miundombinu, hospitali etc. Pesa hizo zielekezwe huko badala ya huu ufujaji wa pesa za wananchi.
   
 6. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #6
  Feb 21, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,141
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  The country is given to the selected few, the rest we must take our own dicision because your best friend is your own head, think twice before you act.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  Mkuu halafu hiyo 14.85 billioni=(46,000,000x323) ni 40% ya mishahara yao ya miaka mitano. Kwa hiyo katika miaka mitano Wabunge jumla ya mishahara yao ni shilingi 37.12 billioni ukiweka na kiinua mgongo wameondoka na shilingi 51.975 billioni (hatujaweka marupurupu yao hapa) na hakuna chochote walichokifanya ili kutetea maslahi ya nchi na hatimaye kuleta maendeleo ya kweli. 2010 kuna uwezekano idadi ya Wabunge ikaongezeka zaidi maana baadhi ya majimbo wanataka kuyagawa mara mbili. Sijui ni nani aliyewadanganya kuwa na idadi kubwa ya Wabunge kunaongeza utendaji wao!
   
 8. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #8
  Feb 21, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 16,189
  Likes Received: 2,718
  Trophy Points: 280
  Si wanalipa kodi kutoka kwenye hayo malipo kama walala hoi wengine?
   
 9. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #9
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 80,463
  Likes Received: 117,261
  Trophy Points: 280
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/26768-dk-slaa-kuanika-hadharani-nchi-nzima-posho-za-wabunge.html

  "Nchi hii wanasema ni masikini, fikiria kuna wabunge 320 walipwe posho wakiwa Dodoma 135,000 kwa siku, mwisho wa mwezi milioni saba ambazo ni kiasi kidogo tu kinakatwa kodi. Hili ni jambo la ajabu?Ebu tazama maisha ya Watanzania vijijini na wamuogope Mungu," alisema Dk Slaa.
   
 10. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #10
  Feb 21, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 2,020
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  Ni wa-Tanzania wangapi wanaona kuna mantiki katika hoja hiyo ya Dk. Slaa? Is there real support for such reasoning? Hadi tutakaopojitambua, kuwa wakweli na wajasiri kuhusu masuala ya uendeshaji wa uchumi, uongozi wetu na haki zetu, wakulu wataendelea kula bila kuumiza vichwa kuhusu haja ya kuweka UWIANO SAHIHI.
   
 11. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #11
  Feb 21, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,427
  Likes Received: 2,086
  Trophy Points: 280
  KILA Mbunge ataondoka na zaidi ya Sh46milioni kama kiinua mgongo baada ya Rais Jakaya Kikwete kulivunja Bunge Julai mwaka huu.

  Bunge hilo litavunjwa baada ya mkutano wa bajeti unaotarajiwa kumalizika mwishoni mwa Agosti mwaka huu kwa ajili ya kujiandaa uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba.

  Fedha hizo ni sawa na asilimia 40 ya mishahara ya miaka yote mitano ya utumishi bungeni ambapo mshahara wa kila mbunge kwa sasa anafikia jumla ya Sh1,921,000 kwa mwezi.

  Kwa mujibu wa Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashilillah, wabunge watalipwa fedha zao mara baada ya Bunge kuvunjwa.

  Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina wabunge 325, kati yao 49 ni mawaziri na manaibu waziri. Ukiondoa mawaziri na manaibu wao ambao kinua mgongo chao hulipwa na serikali, hivyo watakao lipwa na Bunge ni 276. Kwa mantiki hiyo jumla ya Sh12,724,704,000 zitalipwa kama kiinua mgongo kwa wabunge hao ukiondoa mawaziri.
  HABARI NDO HIYO!
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Feb 22, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Kweli habari ndio hii, ila inauma!

  Huwa napata sana shinda kuona kuna watu wana matumaini na baadhi ya wabunge, atokee mmoja akatae hizo hela!!

  hii kitu ndiyo inafanya watu wawe na hasira huko makazini na kuendeleza rushwa mtindo mmoja!!

  kazi ipo
   
 13. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #13
  Feb 22, 2010
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Mkuu, sioni mtu wa kukataa pesa katika dunia ya leo.

  Wengi wetu wangekuwa katika mgao huo wangefurahi sana.
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #14
  Feb 22, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  mwalimu anapostaafu analipwa asilimia ngapi ya mshahara wake wa mwisho?
   
 15. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #15
  Feb 22, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,482
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Ndio maana hiyo kazi wengi wanaipenda, hata humu wengi mwaka huu watajitosa......tuko hivyo...mimi kwanza, wengine baadaye. Wanataaluma wetu wa taasisi za elimu wameezamia huko baada ya kuhangaika miaka chungu zima kwa vijishara vidogo, wakagundua ulaji uko kwa bunge! haoooo....
   
 16. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #16
  Feb 22, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,641
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kama siyo wanafiki Dr.Slaa na wenzake wagome wasichukuwe hayo mafao ili yawasaifdie wananchi majimboni mwao...sababu wananchi majimboni mwao wanaishi kwenye lindi la umaskini......we! thubutu!!!
   
 17. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #17
  Apr 17, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 254
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 60
  Major boost for MPs loan fund

  By Patrick Kisembo
  17th April 2010
  National Assembly


  The parliament has passed a declaration to increase the fund for disbursing loans to MPs, to purchase vehicles and other things, from 18bn/- to 43bn/-.

  The Deputy Minister for Finance and Economic Affairs, Omari Yusuf Mzee tabling the declaration in the national Assembly yesterday said the amount stated can be regulated by the responsible minister depending on the number of members of parliament who will be given loans and changes of prices of goods in the market.

  The fund was last increased in 2005.

  Mzee said the fund is expected to be used to provide loans to MPs and civil servants for purchasing vehicles and other means of transport.

  He said it would also be used to offer loans to civil servants for purchase of domestic items such as refrigerators, cookers, furniture, radio, bicycles, fans and tailoring machines.

  The Deputy Minister said out of the 43bn/-, 14.8bn/- would be used to provide loans to MPs for the purchase of vehicles.

  He said about 9.64bn/- would be lent to civil servants to buy vehicles; 1.2bn/- as loans for purchase of motorcycles, while 3bn/- would be for loans for maintenance of vehicles and motorcycles for civil servants.

  The Deputy Minister said that 14bn/- would be used to give loans to civil servants for domestic appliances and 360m/- which is 0.84 per cent are the costs of managing the fund.

  He said income earned from the sale of dilapidated transportation facilitates would be ploughed back into the fund to boost it.

  Mzee said debt repayments from MPs salaries would be used as short term guarantees for the purpose of generating profits.

  “The profit which will be earned will help to offset the amount not recovered from MPs,” said Mzee.

  Speaking on behalf of the opposition camp, Kabwe Zitto, MP for Kigoma North said the opposition just received the document on Thursday and had no comment on it.
   
 18. M

  MtazamoWangu JF-Expert Member

  #18
  Apr 17, 2010
  Joined: Apr 25, 2009
  Messages: 313
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  do not expect the opposition parties to be against this, hapo ndipo unapojua Uzalendo wa hawa ndugu zetu, masuala ya yanayogusa mabolesho ya maslahi yao hutasikia wakisema.....
   
 19. D

  Dr Willibrod Slaa Verified User

  #19
  Apr 17, 2010
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 675
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 60
  Mtazamo Wangu,

  Hii ni hukumu isiyostahili. Nilipotangaza Mishahara ya Wabunge kuwa ni "kufuru mbele ya Mungu" ukilinganisha ni mishahara ya Watanzania, Nilizungumza na wenzangu wote walinitenga, wakanisakama. Hivyo sidhani kama hukumu yako ni sahihi. Hoja ya Zitto ni kuwa Kambi ya Upinzani imepata "Azimio" naomba ni sahihishe, kwenye thread lugha iliyotumika ni "Declaration" neno sahihi "Resolution". Hoja ya Zitto ni kuwa Kambi ya Upinzani imeshindwa kutoa "Comment" au maoni kwa vile imepata azimio hilo jioni kabla ya kuwasilishwa Mezani/Ukumbini kwa mjadala. Hivyo Kambi haikupata nafasi ya kufanya utafiti na uchunguzi. Kuna mambo ya msingi lazima uelewe:

  i) Kuhusiana na Wabunge swala la msingi ni kuwa Wabunge hawapewi fedha hizo kama hisani, ni Mkopo. Hivyo hoja inakuwa chache zaidi kwa kuwa ni mkopo, na ni mfuko unaozunguka " Revolving" . Kumbuka pia tofauti na watumishi wa Serikali Wabunge wakiisha kukopeshwa Magari Serikali haiwapatii tena magari kwa shughuli zao. Kutoka mwaka 2005 hadi leo Bei ya magari imepanda maradufu na ndio msingi wa mtaji kuongezwa.

  Miaka ya nyuma wabunge walikuwa wanapewa magari na Serikali, lakini yalikaa kwenye pool na kukawa na migogoro mingi sana. Mtindo wa sasa unaondoa mgogoro, unafanya Serikali na hivyo rasilimali ya watanzania isitumike na wabunge visivyo kwa kuwa matengeneo ya magari hayo ni juu ya mbunge mwenyewe, Asipokata comprehensive Insurance, gari likapata ajali Serikali haihusiki.

  Lakini bado kungelikuwa na maswali:

  1) Kwanini Wabunge wapate mkopo fedha nyingi kiasi hicho wakati kwa maendeleo kwa nchi nzima Serikali ilitoa awamu ya kwanza 21 Billioni kwa mkopo wa Watanzania nao pia una mlolongo mgumu sana ukilinganisha na wa Wabunge. Hivyo bado hapa kungelikuwa na hoja kuwa je nikwanini Serikali inaweza kupata njia rahisi ya kuwakopesha wabunge na wakati huo huo kwa maendeleo kuna kuwa na ubunifu mdogo sana Hii ndio hoja, siyo kwamba kambi ya Upinzani imekuwa "numb". Tatizo je Kambi imepata muda wa kutosha kufanya utafiti wa kutosha? Unaeleza nini huu mtindo wa Serikali kuleta mambo "Under certificate of Urgency" je mtindo huu unaruhusu kufanyanika kwa mjadala wa afya?

  Nadhani hii ingelikuwa hoja.

  2) Azimio lina mambo mazito sana, kwa mfano Mfuko huu ndio pia unakopesha watumishi wa Serikali magari, pikipiki, na vyombo vya nyumbani. Wakati wa Bajeti iliyopita unakumbuka nilizuiliwa na Spika baada ya Point of Order kutoka kwa Waziri Marmo na Kombani, nilipokuwa ninahoji Matumizi ,makubwa ya furniture, vifaa, n.k. Waliokuwa wanafuatilia wanakumbuka Celina Kombani alinyanyuka na kutamka kuwa matumizi hayo ni kwa "Entitled Officers". Sasa iwapo hao ni entitled officers na huwa wanapewa vifaa na magari hayo na Serikali ni yapi haya tena yanayoingia kwenye mfuko wa Mkopo?

  Lakini nadhani mtu makini asingelitegemea Kambi ya Upinzani kukurupuka na ku castigate Azimio hilo bila kufanya utafiti wa kina nakuoanisha yaliyoko kwenye bajet, yanayotolewa na Serikali kwa entitled officers na haya yanayotolewa kwenye mfuko wa mkopo. Kambi ilihitaji kufanya research ya kina kutoa Msimamo "Informed" tofauti na MtazamoWangu anavyotaka kuonyesha ambayo hatari yake ni Kambi ya Upinzani ingeliitwa inaropoka bila utafiti.

  Nadhani hoja iliyokuwepo inaeleweka, na Zitto kwa niaba ya Kambi alikuwa Honest kueleza kuwa Kambi haikupata muda wa kutimiza wajibu wake kwa kuwa Serikali imelileta Azimio hilo kwa kustukiza. Kwa watafiti wakiangalia Order Paper iliyokubaliwa awali haikuwa na Azimio hili, na limeiingia dakika ya mwisho.

  Nilidhani ni muhimu kuelewa mazingira haya, ili mtu akihukumu jambo alihukumu akiwa na Taarifa sahihi na kamili ya mchakato unaohusika.
   
 20. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #20
  Apr 17, 2010
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 8,117
  Likes Received: 2,414
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa najaribu kufuatilia ile mijadala ya pale chuo kikuu juu ya ujamaa (Nadhani wanaita kigoda cha mwalimu). Ninaposikia habari hii, inanipa taabu sana kuwaelewa serikali na wabunge wetu..... Hivi kweli hawa watu wanapita kwenye hospitali zetu kuona hali ilivyo?.......Wanajua hali za shule zilivyo? Achilia mbali maeneo mengine ya kijamii!.......Kama angalau wangalikuwa wanafikiria mabo hayo mawili tu, kwa hakika tusingesikia vitu kama hivi vikipitishwa bungeni katika style hii! Urgency!? Urgency kwenye magari wakati wakina mama wanaojifungua wanalala mzungu wa nne mahospitalini? Aaaargh....mambo mengine kweli yanasikitisha sana. Vipaumbele vyetu ni magari?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...