Bw. Miundombinu,
Huu ni uamuzi wa busara sana. Nchi hii haiwezi kuendelea ikiwa watumishi wa umma wana mashaka na hali zao za maisha na uchumi. Ni bahati mbaya tu kuwa kwa desturi, umasikini una kawaida ya kupandikiza hisia za chuki na wivu. Busara ndogo tu inatufundisha kuwa huwezi kuwa na ng'ombe ambaye humpatii malisho mazuri na madawa halafu utegemee atoe maziwa mazuri, ngozi nzuri na nyama laini. Kukosekana kwa uhakika wa hali nzuri ya maisha kwa watumishi wa umma kunaathiri sana maendeleo kwa kuwalazimu kwanza kutumia muda mwingi kujitafutia unafuu wa maisha yao; na pili kufikiria kuibaiba na ubadhirifu. Katika mazingira hayo, mahitaji ya wananchi yanapewa kipaumbele kidogo sana. Mikopo hii yaweza kuwa suluhisho zaidi kuliko posho ambazo zinafanya watumishi wa umma kuwehuka kuzitafuta na kuacha kazi za majalada na uchambuzi mezani kwenda kwenye warsha na safari.
Ni vyema kufahamu kuwa pamoja na mambo mengine, maboresho ya utumishi wa umma katika nchi za kusini mashariki mwa asia (tiger economies) yalichangiwa sana na maboresho ya utumishi wa umma yaliyotoa neema kwa wafanyakazi. Neema ile ilivutia wataalamu na vijana kutoka katika sekta binafsi kujiunga na sekta ya umma. Tija na morali viliongezeka na heshima ya utumishi wa umma ikapanda. Punde mabadiliko katika uchimi yakaanza kuonekana. Na ni kweli kuwa katika mchakato ule, wananchi walilalama na hawakufurahishwa na kitendo cha wafanyakazi wa sekta ya umma kuboreshewa hali zao. Wengi waliona ni unyonyaji na ubadhirifu kuwaongezea watumishi wa umma kipato na fursa za mikopo ilihali wananchi ni maskini. Kilichasaidia ni kuwa serikali zile zilikuwa za kidikteta si kidemokrasia hivyo, sauti za wananchi zilififishwa na matokeo mazuri yalionekana baadae.
Na hapa kwetu tusitarajie ongezeko hili litapokelewa kwa mikono miwili na wananchi. Wakp watakaopinga. Ukweli unabaki kuwa Sekta ya Umma iliyo fukara haiwezi kuondoa umaskini, itazidisha ufukara tu. Ni wakati sasa tuondokane na dhana tuliyobeba vichwani mwetu kuwa mtumishi wa umma, padri, mwalimu lazima awe masikini masikini hivi au fukara fukara hivi.
Leo kijana aliyetoka Chuo Kikuu anaingia kwenye sekta binafsi na ndani ya mwezi mmoja anakopeshwa mara kumi ya mshahara wake ananunua gari yake au anapanga nyumba na kuanza kujitegemea. Aidha, amekatiwa bima ya afya AAR inayomruhusu kutibiwa kwenye hospitali yenye uhakika yeye na dependants 3-4. Kwa upande wa utumishi wa umma, kijana huyo anaanza na mshahara wa TGS D ambao kimantiki unamruhusu kupanga chumba kimoja tu na si nyumba, kutokuwa na simu ya mkononi ambayo ni muhimu kwa mawasiliano na haumruhusu kununua gari wakati standing order inamtaka awe amefika ofisini saa 1 na dk 30 asubuhi. Katika mazingira hayo unategemea nini? Hataacha file mezani akimbizie workshop au safari itakayomlipa mara mbili au tatu ya mshahara wake? Je ukimkopesha akanunua samani na gari ukawa unamkata kidogo kidogo hutamjengea loyalty na hali ya kuthamini kazi yake kwa kuwa akizembea atafukuzwa na ili hali ana deni? je hatufahamu kuwa wako wengi katika sekta binafsi ambao wanafanya kazi kwa bidii na hawahami kwa kuwa wana mikopo au wanahama tu pale ambapo wamemaliza mikopo yao? Leo hii, the best brains zinakimbilia sekta binafsi zaidi kuliko sekta ya umma. Uzalendo hauliwi mkavu mkavu.
Ifike mahala tukubaliane kuwa ni kweli nchi yetu ni maskini wa kipato na kwamba suluhisho si kwa wote kubaki kuwa maskini na wote tuondokane na umasikini kwa wakati mmoja. Tunaweza kulazimika kuwa na awamu, tunaweza kuamua kuwaweka watumishi wa sekta ya umma katika hali nzuri kwanza, kisha tukajikuta tumechochea maendeleo katika sekta nyingine.
Hapa inabidi nikubaliane kwa shingo upande kwa wabunge kukopeshwa mikopo kwa mtindo huu.
Wabunge kwa kweli wanakazi ya kuzunguka jimboni kote na mara nyingi magari haya wananchi wajimboni wanayaona kama wana haki nayo, kwa hiyo lifti, kubeba watu nk ni common mno, hivyo kwa upande mdogo magari haya yanasaidia jamii.
Hii ni the most cost effective way ya kuprovide usafiri kwa Hon Mps kuliko taratibu serikali inazotumia kwa mfano mawaziri, PS kuwa na magari ya serikali yanayolipiwa mafuta, dereva, utengenezaji, insurance blah blah.
Mimi ningependekeza mfuko huo uongezwe ufike hata 100 billion ili mawaziri, PS nao wapewe mikopo tuachane na kumaintain hayo MAVX ambayo nina uhakika cost baada ya miaka mitano ni zaidi mara kumi ya hiyo mikopo.
Hapa inabidi nikubaliane kwa shingo upande kwa wabunge kukopeshwa mikopo kwa mtindo huu.
Wabunge kwa kweli wanakazi ya kuzunguka jimboni kote na mara nyingi magari haya wananchi wajimboni wanayaona kama wana haki nayo, kwa hiyo lifti, kubeba watu nk ni common mno, hivyo kwa upande mdogo magari haya yanasaidia jamii.
Hii ni the most cost effective way ya kuprovide usafiri kwa Hon Mps kuliko taratibu serikali inazotumia kwa mfano mawaziri, PS kuwa na magari ya serikali yanayolipiwa mafuta, dereva, utengenezaji, insurance blah blah.
Mimi ningependekeza mfuko huo uongezwe ufike hata 100 billion ili mawaziri, PS nao wapewe mikopo tuachane na kumaintain hayo MAVX ambayo nina uhakika cost baada ya miaka mitano ni zaidi mara kumi ya hiyo mikopo.
Si wanalipa kodi kutoka kwenye hayo malipo kama walala hoi wengine?