Utawala Wa Kisultani Chini ya Kikwete Na CCM !

Umesahau Slaa kamweka Josefina Ofisini chadema kusimamia mambo ya mapato na matumizi yote, eti ni mtaalaam wa "software" za aina hiyo. Huyo ndio bado hana madaraka Serikalini ana mweka hawara ofisini tena wazi wazi na anatumia fedha za chama kusafiri nae.
Wewe ni mtaalamu wa nini? au wa Daku?
 
Kiukweli tunahitaji mabadiliko ya kiutawala,haiwezekani miaka 50 ya uhuru watu ni walewale na maendeleo ya kurudi nyuma!
Japokuwa itakuwa ngumu kuestablish mfumo kutokana na upinzani mkali kutoka kwa wale wanaonufaika na mfumo,lakini ni lazima tupitie huko ili kuepuka mapinduzi dhidi ya tawala dhalimu(misri,Algeria,Tunisia wamefikia hapo)
 
Rais Kikwete ameigeuza Tanzania kuwa nchi ya Kisultani ambayo watoto wa wenye madaraka kuzidi kupewa nafasi kubwa katika serikali na Chama. Rais Kikwete ndiye kiongozi mkuu wa nchi, ila kila mtu katika family yake ni kama Rais.

Mama Salma anapewa heshima kama Rais, na hata anakopita magari yote usimamishwa. Ridhiwani anafanya teuzi nyingi sana ndani ya serikali ambako marafiki zake upewa nafasi nyeti na kubwa.Ukimuudhi Ridhiwani utapata matatizo katika ndoa yako na hata ajira ipotee. Vile vile, kwa mara ya kwanza katiak historia ya Tanzania, Rais, Mkewe, na mwanaye wana nyadhifa za juu kwenye uongozi wa Chama

Watawala na familia zao wananeemeka chini ya Kikwete. Kwa mfano familia ya Kairuki. Mbelwa chini ya miaka mitatu ametoka kuwa mwandishi wa hotuba hadi ubalozi na ukurugenzi Mambo ya nje. ni wanagapi wako Foreign miaka zaidi ya 20 na bado hawajapata hata naibu ukurugenzi?

Mkewe Mbelwa Angela Kairuki kapewa ubunge na hatimaye kuteuliwa naibu waziri na mbunge. Mdogo wake Mbelwa ni mkurugenzi mkuu pale TIC. Ukienda BOT mambo siyo mambo. Watoto wa vigogo wako kila sehemu. Ukienda kwenye balozi zetu ni watoto wa wakubwa kwenye balozi hasa za ulaya. Huu ni mfano tu; Watoto Wa Vigogo BoT

1. 1. Salama Ali Hassan Mwinyi, 2. Filbert Tluway Sumaye, 3. Zaria Rashidi Kawawa, 4. Blasia William Mkapa,
5. Harriet Matern Lumbanga, 6. Pamela Edward Lowassa, 7. Rachel Muganda, 8. Salma Omar Mahita,
9. Justina Mungai, 10. Kenneth Nchimbi, 11. Violet Philemon Luhanjo, 12. Liku Kate Kamba, 13. Thomas Mongella na
14. Jabir Abdallah Kigoda.


Watoto wa wakulima tukilalamika tunaambiwa twende shule ili tupate nafasi kama hizo, jamani haki hiko wapi? Kama siyo usultani ni nini.
Umesahau Chadema nacho chama cha Kisultani.

Tundu Lissu na dada yake wote ni wabunge wa Chadema.

Mzee Mtei, muasisi wa Chadema kaampa Uenyekiti Mkwe wake Mbowe.

Rose Kamili kapewa ubunge alizaa na Dr Slaa.

Ndesamburo, mbunge pamoja na mtoto wake kike na mkwe wake wote wabunge wa Chadema.

Kamanda unaionaje hii.
 
Kwani hujaona kitu kama hii, Hiki ni chama ambacho bado kinatambaa kwenye ulingo wa siasa lakini tayari kinafanya undugunization with impunity.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    34.7 KB · Views: 51
  • image.jpg
    image.jpg
    46.9 KB · Views: 51
  • image.jpg
    image.jpg
    36.3 KB · Views: 41
  • image.jpg
    image.jpg
    33.5 KB · Views: 45
  • image.jpg
    image.jpg
    29.7 KB · Views: 39
  • image.jpg
    image.jpg
    32.7 KB · Views: 47
  • image.jpg
    image.jpg
    38.3 KB · Views: 43
mie nadhani kuna tofauti kubwa tu kati ya ajira za serekali na kuwa mwanasiasa hawa wa mwisho wameajiriwa na watu na hupitia michakato halali ya kichama. Mfano Nape japo ni mtoto wa aliyekua kigogo ila inajulikana wazi kwamba amepitia vetting process za kutosha mpaka akawa mwenezi. Ila suala la uozo kitika utumishi wa umma wall sio siri tena ndio maana kumefanyika reforms recently. Tunapoingiza siasa katika professionalism kuna tatizo
 
Bora hata ya jk unajua kuwa chadema wameweka mpaka hawala zao kwenye viti maalu na udiwani mfano rose kamili suku na paleso-hawala wa slaa,esther matiku -hawala wa mbowe,lisu kapeleka dada yake ambaye ni cristina lisu,ndesambulo kaweka binti yake ukipinga ntakuwekea nyumba ndogo zaidi za hawa watu wako.
We, Muongo na Mkuu wa majungu. Hebu waweke hao mahawara kama ni kweli!
 
Kwanini wajae BOT tu kwanini wasiajiriwe hata Halmashauri? Tanzania nzima hakuna mtoto wa kiongozi mwenye mamlaka ya kuanzia Katibu mkuu wa Wizara anayefanya kazi Halmashauri.
 
Kama wana sifa kwanini wasipewe? Kulalamika hakutakusaidia wewe. Nenda shule

Nina wasiwasi na uwezo wako kufikiri. Walioenda shule wote watapatiwa kazi BoT? Kwa nini watoto wetu sisi viongozi wasifanye kazi katika taasisi zingine ambazo they equally require waliosoma na sio kujazana BoT?
 
Kama wana sifa kwanini wasipewe? Kulalamika hakutakusaidia wewe. Nenda shule
lol, alafu 'wenye shibe' wana majibu mazuri hayo. Ukiwa na roho nyepesi yatakufanya unywe sumu labda kwa wenye roho ngumu basi watatoa machozi, we acha tu!
 
Hata ningekuwa mimi ningefanya hivyohivyo,kwanini mwanangu apate shida nikiondoka? angalia wa Nyerere huwezi amini ni wale watoto wa aliyekuwa kiongozi mkubwa anayeheshimiwa na wote ulimwenguni,uwalinganishe na wa Mandela wanavyochakarika we acha tu ukipata kitumie majuto mjukuu!!!
 
Wandugu, Hiyo ni hulka ya kisiasa popote pale na sio usultani tuu! Umarekani(USA) Rais BUSH (Baba) akarithisha rais G.Bush (mwana) na mwana akafadhilisha mdogo kuwa gavana wa State. Na huko CUBA Mzee Castro kamrithisha Mdogo RAUL. na huko INDIA Mama Gandhi alimrithisha Mwanae RAJIV Gandhi. Na huko GABON Mzee Omari BONGO amemrithisha Ali BONGO..... na sehemu nyingi... La kuweke maanani ni kula nao sahani moja, Kujipanga na kuenda na WAKATI.
 
Back
Top Bottom