Utawala TRA, uhakiki huu ni unyanyasaji

Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
16,111
26,002
Toka wiki hii nzima nimejaribu kuanza utaratibu wa kuhakiki TIN namba yangu lakini ni balaa!

Najua zoezi hili limeanza muda mrefu lakini kuhakiki kwa kipindi kifupi hata cha nusu mwaka hakitoshi kabisa.

Picha hapo juu ni Millenium Tower Makumbusho.
Foleni inatoka ndani na ina nyoka nyoka hadi barabarani kwenye maegesho.
Huko ndani usiseme, viti karibu 150 hadi 200 huko ndani vimejaa na uvundo wa miili na hewa iliyotumika ni discomfort kubwa.

Sijui kwa nini utawala TRA wasingebuni utaratibu endelevu ambao aidha mtu anajihakiki kwa mtandao au muda wa uhakiki usiwe na mwisho, na ufanywe na mtu pale unapohitajika, kama quartely tax payment.

Ni ushauri tu, lakini tunachokiona sasa ni unyanyasaji
 
Pamoja na ukweli kwamba watanzania tunapenda sana kujitokeza wakati wa deadline lakini kiukweli kwenye hili TRA wangebuni utaratibu rafiki zaidi.

Zoezi hili limekuwa gumu sana kwa kweli.
 
hivi TRA mbona wanazidi kufanya maisha kuwa magumu, kwa mtindo huu wa kuwawekea vikwazo walipa kodi hiyo kodi wataikusanyaje? pia information wanazozitaka, 1. TRA wenyewe, nyingi wanazo (wakati wa kuchukua leseni ya udereva/TIN ya zamani)
2. NIDA wanazo,
3. RITA wanazo
4. Tume ya Uchaguzi wanazo.
5. Uhamiaji wanazo (kwa wenye passport),
** Kwa maoni yangu ni kupoteza muda wa watu badala ya kufanya kazi kutwa wakashinde hapo TRA.
 
Mkuu TRA walipoongeza muda watu waliacha kwenda,kwa mfano mwezi wa 12 mzima na mwanzoni mwa jan 2017 kulikuwa na watu wachache sana ,ila ilipofika tarehe 20 jan 2017 watu wakakumbuka kuwa muda umeisha na ndio yanayotokea sasa .
Ukipita kijitonyama saa 12 asubuhi utashangaa hayo magari na watu waliokwisha fika hapo.

Tuache tabia ya kufanya kitu wakati muda ukiwa umebaki mdogo.
 
View attachment 464242 View attachment 464243
Toka wiki hii nzima nimejaribu kuanza utaratibu wa kuhakiki TIN namba yangu lakini ni balaa!

Najua zoezi hili limeanza muda mrefu lakini kuhakiki kwa kipindi kifupi hata cha nusu mwaka hakitoshi kabisa.

Picha hapo juu ni Millenium Tower Makumbusho.
Foleni inatoka ndani na ina nyoka nyoka hadi barabarani kwenye maegesho.
Huko ndani usiseme, viti karibu 150 hadi 200 huko ndani vimejaa na uvundo wa miili na hewa iliyotumika ni discomfort kubwa.

Sijui kwa nini utawala TRA wasingebuni utaratibu endelevu ambao aidha mtu anajihakiki kwa mtandao au muda wa uhakiki usiwe na mwisho, na ufanywe na mtu pale unapohitajika, kama quartely tax payment.

Ni ushauri tu, lakini tunachokiona sasa ni unyanyasaji
Pamoja na malalamiko yako lakini kikubwa hapo ulicho kosea na ni makosa makubwa ni kupost picha mtandaoni bila ridhaa yetu ndugu hayo si matumizi sahihi ya mtandao mambo yanaweza kukugeukia hata kama lengo lako lilikuwa konesha umma hiyo foleni hapo , usidhan wote watashudhulika na foleni hiyo, na kwa hiyo location ya hiyo picha ilivyo pigwa nimesha fahamu ni nani wewe,
 
Na mimi kwa maelezo yako haya, nimeshajua wewe ni nani.
 
Ni usumbufu kweli aisee, halafu kwa Dar sehemu ni chache sana. Mimi nilienda TRA Mwenge wakaniambia niende Millenium Tower, aisee nilichoka foleni niliyoikuta. Mpaka sasa nina miezi mitatu sijarudi tena.
 
Huu utaratibu kwa kweli sio rafiki na sidhani kama hilo lango wanataka wanaweza fikia! Nadhani wangejaribu kubuni namna nzuri ya kumfanya pia mteja asiboreke! Taarifa za Mlipa kodi zingeweza fanywa kwa mfumo kama daftari wa wapiga kura na kusogeza huduma ofisi za Serikali za Mtaa!
 
hivi TRA mbona wanazidi kufanya maisha kuwa magumu, kwa mtindo huu wa kuwawekea vikwazo walipa kodi hiyo kodi wataikusanyaje? pia information wanazozitaka, 1. TRA wenyewe, nyingi wanazo (wakati wa kuchukua leseni ya udereva/TIN ya zamani)
2. NIDA wanazo,
3. RITA wanazo
4. Tume ya Uchaguzi wanazo.
5. Uhamiaji wanazo (kwa wenye passport),
** Kwa maoni yangu ni kupoteza muda wa watu badala ya kufanya kazi kutwa wakashinde hapo TRA.
Mkuu hili ni tatizo la watu waliomo TRA na sehemu nyingine ndani ya serikali.
They think in one dimension only.
 
Pamoja na malalamiko yako lakini kikubwa hapo ulicho kosea na ni makosa makubwa ni kupost picha mtandaoni bila ridhaa yetu ndugu hayo si matumizi sahihi ya mtandao mambo yanaweza kukugeukia hata kama lengo lako lilikuwa konesha umma hiyo foleni hapo , usidhan wote watashudhulika na foleni hiyo, na kwa hiyo location ya hiyo picha ilivyo pigwa nimesha fahamu ni nani wewe,
Karibu tuondoe kero!
 
Mkuu TRA walipoongeza muda watu waliacha kwenda,kwa mfano mwezi wa 12 mzima na mwanzoni mwa jan 2017 kulikuwa na watu wachache sana ,ila ilipofika tarehe 20 jan 2017 watu wakakumbuka kuwa muda umeisha na ndio yanayotokea sasa .
Ukipita kijitonyama saa 12 asubuhi utashangaa hayo magari na watu waliokwisha fika hapo.

Tuache tabia ya kufanya kitu wakati muda ukiwa umebaki mdogo.
Mwezi wa 12 ni likizo na watu wanafunga biashara mashule na kwenda kupumzika makwao.
 
Mpaka leo sijaelewa nia na madhumuni ya uhakiki wa tin na umuhimu wake kiasi watu tuache kazi hapa tuu na kwenda kupanga foleni siku 3 mfululizo.
 
Ila akili ni kuongeza muda ili watu wasiende holidays?....sie miswahili tuna tabu shida na kero mpaka trump anatamani tungeondolewa duniani ..... mijitu hatujui hata umuhimu wa holidays season.
 
Pamoja na malalamiko yako lakini kikubwa hapo ulicho kosea na ni makosa makubwa ni kupost picha mtandaoni bila ridhaa yetu ndugu hayo si matumizi sahihi ya mtandao mambo yanaweza kukugeukia hata kama lengo lako lilikuwa konesha umma hiyo foleni hapo , usidhan wote watashudhulika na foleni hiyo, na kwa hiyo location ya hiyo picha ilivyo pigwa nimesha fahamu ni nani wewe,
Tehehehe , mkuu umepigwa picha nini, maana sio kwa maneno hayo.?
Ila katika hali ya kawaida hakuna picha mbaya hapo wala iliyomuhaibisha mtu, au hajawahi kupanga foleni maishani mwako?
Ni vizuri katupa taarifa na picha kabisa, ila na sisi tuliokuwa tunajiandaa kwenda tuvute subra Kwanza mpungue.
 
Mkuu hili ni tatizo la watu waliomo TRA na sehemu nyingine ndani ya serikali.
They think in one dimension only.
Husitegemee ule chips yai na wale kuku wa miezi 6, huku ukipulizwa na kiyoyozi kuanzia chumba unacholala hadi ofisini, then upate uwezo wa kufikiria umbali zaidi ya pua, katu haiwezekani na haito kaa itokee. Hatuna budi kukubaliana na matokeo.
 
Dar ndiyo shida, mikoani ukienda ni muda mfupi sana unahudumiwa na kuondoka,
dar walitakiwa waongeze vituo vya uhakiki.
 
View attachment 464242 View attachment 464243
Toka wiki hii nzima nimejaribu kuanza utaratibu wa kuhakiki TIN namba yangu lakini ni balaa!

Najua zoezi hili limeanza muda mrefu lakini kuhakiki kwa kipindi kifupi hata cha nusu mwaka hakitoshi kabisa.

Picha hapo juu ni Millenium Tower Makumbusho.
Foleni inatoka ndani na ina nyoka nyoka hadi barabarani kwenye maegesho.
Huko ndani usiseme, viti karibu 150 hadi 200 huko ndani vimejaa na uvundo wa miili na hewa iliyotumika ni discomfort kubwa.

Sijui kwa nini utawala TRA wasingebuni utaratibu endelevu ambao aidha mtu anajihakiki kwa mtandao au muda wa uhakiki usiwe na mwisho, na ufanywe na mtu pale unapohitajika, kama quartely tax payment.

Ni ushauri tu, lakini tunachokiona sasa ni unyanyasaji
Tatizo la waswahili bwana !!nyie zoezi lina miezi kama mitatu nyuma mmeshindwa kwenda mapema hadi msubiri tarehe za lala salama ndio mjitokeze!!mwezi dec wote kulikuwa hakuna watu kivile,leo imebaki siku nne mnaanza kulalamika eti muda hautoshi???na hata huu mwezi mmoja c wameuongeza tu badaye,tujifunze kwenda na muda sio kila kitu kulala mika tu wakati makosa ni yetu.
 
Back
Top Bottom