Utawala TRA, uhakiki huu ni unyanyasaji

Utawala TRA, uhakiki huu ni unyanyasaji

View attachment 464242 View attachment 464243
Toka wiki hii nzima nimejaribu kuanza utaratibu wa kuhakiki TIN namba yangu lakini ni balaa!

Najua zoezi hili limeanza muda mrefu lakini kuhakiki kwa kipindi kifupi hata cha nusu mwaka hakitoshi kabisa.

Picha hapo juu ni Millenium Tower Makumbusho.
Foleni inatoka ndani na ina nyoka nyoka hadi barabarani kwenye maegesho.
Huko ndani usiseme, viti karibu 150 hadi 200 huko ndani vimejaa na uvundo wa miili na hewa iliyotumika ni discomfort kubwa.

Sijui kwa nini utawala TRA wasingebuni utaratibu endelevu ambao aidha mtu anajihakiki kwa mtandao au muda wa uhakiki usiwe na mwisho, na ufanywe na mtu pale unapohitajika, kama quartely tax payment.

Ni ushauri tu, lakini tunachokiona sasa ni unyanyasaji
hivi hawawezi wakafanya digital confermation
mm sielewi sijui egov inaanza lini
 
Na mimi kwa maelezo yako haya, nimeshajua wewe ni nani.
Ujinga wenu watanzania utawaisha lini??? Niambie kosa gani kisheria MTU kupiga picha na kifungu namba ngapi???
Kutishana nyau tuuu.,kila kitu simu hizi ni kosa . ,ukivaa TISHETI ni kosa,ukisema ukame ni kosa.,ukimwita MTU mtukufu ni kosa......blaaa blaaa blaaaaa
Jinga sana ninyi
 
Tatizo jingine kwenye huu uhakiki ni kituo ulichosajilia TIN kwa mara ya kwanza. Mimi nilienda kituo cha karibu nikaambiwa taarifa zangu hazipo hapo niende nilikosajili TIN kwa mara ya kwanza. Sasa kwanini wasifanye taarofa ziwe kituo chochote cha TRA. Maana TRA ni moja sasa kwanini kama nimesajilia mbeya taarifa zangu ziwe tawi lolote la TRA, nmehamia dar nataka kuhakiki naambiwa niende mbeya. Lakini kodi yangu ya biashara TRA ya dar wanapokea vizur tu hata hawakatai wakakwambia ukalipia mbeya.
HUU NI USUMBUFU.....
 
Tatizo la waswahili bwana !!nyie zoezi lina miezi kama mitatu nyuma mmeshindwa kwenda mapema hadi msubiri tarehe za lala salama ndio mjitokeze!!mwezi dec wote kulikuwa hakuna watu kivile,leo imebaki siku nne mnaanza kulalamika eti muda hautoshi???na hata huu mwezi mmoja c wameuongeza tu badaye,tujifunze kwenda na muda sio kila kitu kulala mika tu wakati makosa ni yetu.
Mkuu jaribu kufikiri kisasa.
Mimi nimejiunga hadi na mitandao kama ya Paypal ambayo ni secure, na kuna mitandao mingi sana ambayo ina security clearances, imachukua dakika chache tu ku process.

Tatizo kubwa la wasomi wetu ni kutokuwa wabunifu.
They are still attached to pen and paper.
Nchi jirani tu ya Rwanda haifanyi mambo kizamani kama sisi.
People should learn to think forward na hii digital technology.
 
View attachment 464242 View attachment 464243
Toka wiki hii nzima nimejaribu kuanza utaratibu wa kuhakiki TIN namba yangu lakini ni balaa!

Najua zoezi hili limeanza muda mrefu lakini kuhakiki kwa kipindi kifupi hata cha nusu mwaka hakitoshi kabisa.

Picha hapo juu ni Millenium Tower Makumbusho.
Foleni inatoka ndani na ina nyoka nyoka hadi barabarani kwenye maegesho.
Huko ndani usiseme, viti karibu 150 hadi 200 huko ndani vimejaa na uvundo wa miili na hewa iliyotumika ni discomfort kubwa.

Sijui kwa nini utawala TRA wasingebuni utaratibu endelevu ambao aidha mtu anajihakiki kwa mtandao au muda wa uhakiki usiwe na mwisho, na ufanywe na mtu pale unapohitajika, kama quartely tax payment.

Ni ushauri tu, lakini tunachokiona sasa ni unyanyasaji

Hivi wamekosa kabisa ubunifu wa kufanya hilo zoezi electronically ili kuokoa muda wa kazi kwa hao wanaohakikiwa?
 
Dar ndiyo shida, mikoani ukienda ni muda mfupi sana unahudumiwa na kuondoka,
dar walitakiwa waongeze vituo vya uhakiki.
acha uongo mikoani hawajaanza kuhakiki ,nilipita ofisi za kahama shinyanga wakasema mikoani bado zoezi halijaanza
 
wazee wa Deadliest Line, siku zote ulikuwa wapi kufanya uhakiki. Punguza kuzima moto mkuu
 
ndugu zangu m nakubaliana kabisa na mawazo kwamba kama kuna uwezekano...waongeze muda wa kuhakiki TIN. lakin na ss pia tumefanya uzembe mwez wa 12 na huu wa kwanza mwanzoni vituo vilikuwa vitupu....watu wanasubiri mwisho tu....zima moto ndo madhara yake.kusema watu walikuwa likizo labda kama ulikuwa likizo kuanzia mwez wa nane kama ni wa 12 hatukuwa sawa.
 
Pamoja na malalamiko yako lakini kikubwa hapo ulicho kosea na ni makosa makubwa ni kupost picha mtandaoni bila ridhaa yetu ndugu hayo si matumizi sahihi ya mtandao mambo yanaweza kukugeukia hata kama lengo lako lilikuwa konesha umma hiyo foleni hapo , usidhan wote watashudhulika na foleni hiyo, na kwa hiyo location ya hiyo picha ilivyo pigwa nimesha fahamu ni nani wewe,
Kwani kafanya kosa gani? Acha kutisha watu.
 
Huu utaratibu kwa kweli sio rafiki na sidhani kama hilo lango wanataka wanaweza fikia! Nadhani wangejaribu kubuni namna nzuri ya kumfanya pia mteja asiboreke! Taarifa za Mlipa kodi zingeweza fanywa kwa mfumo kama daftari wa wapiga kura na kusogeza huduma ofisi za Serikali za Mtaa!

Mimii nilianza ijumaa iliyopita leo ndio nimeipata hiyo TiN acha kabisa ni shidaaa

Natarajia kuona muda kuongezwa leo jion naawaambia au ni zoezi endelevu
 
Huu utaratibu kwa kweli sio rafiki na sidhani kama hilo lango wanataka wanaweza fikia! Nadhani wangejaribu kubuni namna nzuri ya kumfanya pia mteja asiboreke! Taarifa za Mlipa kodi zingeweza fanywa kwa mfumo kama daftari wa wapiga kura na kusogeza huduma ofisi za Serikali za Mtaa!
Hallow wanachemka kweli kweli, ulisikia nchi gani kuna mwisho wa kuhakiki walipa kodi? Na je ukifika huo mwisho waliopo chuoni hawatakiwi kuwa na biashata tena, au hata wawekezaji hawatakiwi tena? Sijui nani anatoaga huo muongozo. Utafili nchi ya Wazuvendi kule kwenye visiwa vya watu wasioona, napita tu.
 
Wanafikilia kwenye DOA jeupe tu, huku kwenye rangi nyeusi hawataki kabisa kupeleka akili zao.
 
Tehehehe [emoji23] [emoji23] [emoji23] , mkuu umepigwa picha nini, maana sio kwa maneno hayo.?
Ila katika hali ya kawaida hakuna picha mbaya hapo wala iliyomuhaibisha mtu, au hajawahi kupanga foleni maishani mwako?
Ni vizuri katupa taarifa na picha kabisa, ila na sisi tuliokuwa tunajiandaa kwenda tuvute subra Kwanza mpungue.
Watanzania tumezoea kuishi kwa kuvunja sheria na tumesha zoea kiasi kwamba tumefanya kama halali kuvunja sheria kifupi kopost picha ya mtu mwingine bila ridhaa ni kosa tambua hilo kwanza lakin pia kuipiga picha miundo mbinu ya serikali bila kibali maalumu pia ni kosa na hilo ulitambue pia.
 
Kwani kafanya kosa gani? Acha kutisha watu.
Kama unazijua vizuri sheria na sio mbabaishaji ni rahisi kuliona kosa lakini kama ni walewale wasio elewa kitu ila wanajifanya wajuaji kweli huwezi ona kosa lakin tambua hapo ni ndani ya ofisi za serikali na mpigaji picha sidhan kama anakibali maalum cha kufanya hivyo achilia mbali hao walio tokea kwenye picha na kupostiwa bila ridhaa yao ambalo nalo ni kosa lingine.
 
Back
Top Bottom