Utatuzi na msaada

el_magnefico

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
458
1,000
Ukiwa na swali lolote au ukihitaji msaada katika kiswahili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita unaweza ukasaidiwa hapa kadri itakavyowezekana.Ningependelea sarufi kwa mrejesho wa haraka.
 

Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
36,236
2,000
Naomba uniandikie kwa kifupi maudhui ya Tamthilia ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe kwa kuzingatia mafanikio ya maudhui na kutokukubalika hayo maudhui kwa hadhira ukilinganisha na wakati wa sasa.
 

el_magnefico

JF-Expert Member
Nov 6, 2015
458
1,000
Naomba uniandikie kwa kifupi maudhui ya Tamthilia ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe kwa kuzingatia mafanikio ya maudhui na kutokukubalika hayo maudhui kwa hadhira ukilinganisha na wakati wa sasa.
Kwa ufupi maudhui ni jumla ya mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.Katika maudhui tunaangalia dhamira,migogoro,falsafa ya msanii,ujumbe n.k.Katika tamthilia ya Ngoswe-Penzi kitovu cha uzembe,msanii amejitahidi kuonesha dhamira mbalimbali ambazo zina uhalisia katika jamii zetu kama vile imani za kishirikina vijijini (rejea zaidi dhamira) pia vile vile katika ujumbe msanii ameiahasa jamii kama vile kuchanganya mapenzi na kazi sio jambo zuri (rejea zaidi ujumbe) na hata migogoro pia msanii ameizungumzia kama migogoro ya nafsi au mtu na mtu.Kuhusu kutokukubalika kwa hayo maudhui kwa hadhira itatokea ikiwa msanii atazungumzia jamii asiyoijua hivyo wewe kama hadhira katika jamii ya watanzania hayo mambo yaliyozungumzwa katika tamthiliya hayapo kama ni hivyo nina imani inabidi ifanyike tafiti zaidi na sidhani kama ni kwa ngazi ya kidato cha 1-6.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom