el_magnefico
JF-Expert Member
- Nov 6, 2015
- 488
- 570
Ukiwa na swali lolote au ukihitaji msaada katika kiswahili kuanzia kidato cha kwanza hadi cha sita unaweza ukasaidiwa hapa kadri itakavyowezekana.Ningependelea sarufi kwa mrejesho wa haraka.
Kwa ufupi maudhui ni jumla ya mawazo yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo.Katika maudhui tunaangalia dhamira,migogoro,falsafa ya msanii,ujumbe n.k.Katika tamthilia ya Ngoswe-Penzi kitovu cha uzembe,msanii amejitahidi kuonesha dhamira mbalimbali ambazo zina uhalisia katika jamii zetu kama vile imani za kishirikina vijijini (rejea zaidi dhamira) pia vile vile katika ujumbe msanii ameiahasa jamii kama vile kuchanganya mapenzi na kazi sio jambo zuri (rejea zaidi ujumbe) na hata migogoro pia msanii ameizungumzia kama migogoro ya nafsi au mtu na mtu.Kuhusu kutokukubalika kwa hayo maudhui kwa hadhira itatokea ikiwa msanii atazungumzia jamii asiyoijua hivyo wewe kama hadhira katika jamii ya watanzania hayo mambo yaliyozungumzwa katika tamthiliya hayapo kama ni hivyo nina imani inabidi ifanyike tafiti zaidi na sidhani kama ni kwa ngazi ya kidato cha 1-6.Naomba uniandikie kwa kifupi maudhui ya Tamthilia ya Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe kwa kuzingatia mafanikio ya maudhui na kutokukubalika hayo maudhui kwa hadhira ukilinganisha na wakati wa sasa.
1.Kucheza kunachangamsha kuliko kukaa.(kitenzi jina)tunga sentensi zinazohusu ngeli KU
yeah aisei safi1.Kucheza kunachangamsha kuliko kukaa.(kitenzi jina)
2.Kule kunavutia wakati wa usiku.(ngeli ya mahali pa-mu-ku)