Utata, upotoshaji na maoni yangu kuhusu mchoro wa Monalisa na Da Vinci Code

Habibu B. Anga

JF-Expert Member
May 7, 2013
6,557
25,671
83fc7d7f47454445e010ae6a9debda39.jpg




Sasa, unaweza kupata nakala za Kitabu changu cha "NYUMA YA ULIMWENGU WA SIRI NA UJASUSI".
kitabu kina kurasa 442 na ndani yake kuna makala 17.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 50,000/-

Pia waweza kupata kitabu changu cha "OPARESHENI ZA KIJASUSI ZILIZOFANIKIWA ZAIDI"
Kitabu hiki kina kurasa 214 na ndani yake nimechambua Oparesheni 6 tofauti.
Bei ya kitabu hiki ni Tsh 15,000/-

Wasiliana nami kwa namba 0759 181 457

Kuna uzi mwanana kabisa nimeona unajadiliwa sana wikii huu kuhusu Mchoro wa Monalisa na mchoraji wake Leonardo Da Vinci. Nimeona si mbaya na mimi nikitia maneno machache kuhusu mada hii na kujaribu kufafanua mambo kadhaa ambayo nahisi kama yanapotoshwa au hayaelezwi sawa sawa kwa mtazamo wangu na naomba nichangie katika maeneo matatu. i) ujumbe wa siri katika mchoro wa Monalisa ii) sababu za Mchoro huu kuwa maarufu sana iii) utata wa 'The Da Vinci Code'

KUHUSU 'ujumbe wa siri' KATIKA MCHORO WA MONALISA...

Kwanza kabisa kabla sijaeleza maoni yangu kuhusu ujumbe wa siri kwenye mchoro wa Monalisa, nieleze kidogo kuhusu kitabu cha Dan Brown. Kitabu hiki (The Da Vinci Code) ndicho hasa kilichosababisha kuibuka upya mijadala kuhusu mafumbo na usiri juu ya mchoro wa Monalisa.

Binafsi kwa mara ya kwanza nilikisoma mwaka 2006. Kipindi hiki nilikuwa niko sekondari bado. Nilikuwa nasoma masomo ya Sayansi lakini pia niliongezea masomo ya dini (Divinity) kama ziada. Niliposikia kuhusu kitabu hiki 'kuchallenge' uhalali/usahihi wa mambo kadhaa ya kihistoria kuhusu Biblia nikapata hamu kubwa sana ya kukisoma. Nilihangaika sana kukitafuta lakini hatimaye nikakipata na kukisoma.

Nieleze kwa ufupi sana; kitabu kinamuhusu Bwana mmoja ambaye ni Profesa wa chuo kikuu ambao pamoja na binti Fulani wanagundua kisanduku/kiboksi kidogo chenye kuelezea siri kadhaa kuhusu imani ya kikristo na historia yake iliyofichwa. Hii ni baada ya Bwana mmoja mfanya kazi wa jumba la makumbusho ya Louvre Ufaransa kuuwawa usiku na mtawa wa kikatoliki katika jumba hilo la makumbusho na maiti yake ikawekwa katika mkao sawa sawa kabisa na moja ya picha ya Leonardo inayoitwa Vitruivan Man. Pia kabla hajakata roho akatumia damu yake kujichora kifuani nyota ya pembe tano (pentagram) pamoja na herufi za kimafumbo.

Kwahiyo Profosea huyu akaitwa kusaidia upelelezi hasa kuwasaidia polisi kuelewa nini maana ya mafumbo hayo. Katika uchunguzi wake huyo profesa na huyo binti wanagundua hicho kiboksi na vitu vingine. Lakini kinachowasaidia kufanya gunduzi zote hizi ni jumbe za siri zilizofichwa katika michoro mbali mbali ya Leonardo, kama vile Monalisa, The last super, Vitruvian Man n.k.

Sasa hoja anayoijenga Dan Brown katika kitabu chake ni kwamba Leonardo Da Vinci aligundua 'The Holy Grail' na jinsi ya kuitambua mahali ilipo.
Holy Grail ni kitu/kifaa maalum cha kiungu ambacho kina uwezo wa kukleta furaha, kuponya magonjwa na kumpa mtu ufunuo kuhusu siri kuu za dunia zilizo fichwa vizazi na vizazi. Sasa hapa ndio utata mzima unapozuka..

Kwanza kabisa nisema watu wamejisahau mno kwamba hiki kitabu ni fiction (hadithi ya kutunga) na Dan Brown ni mwandishi nguli wa fiction. Kabla ya kitabu hiki alishaandika kitabu ambacho kilijipatia umaarufu kiasi kiliitwa Angels & Demons. Pia baada ya kitabu hiki alitoa kitabu kingine kilichoitwa The Lost Symbol ambacho hakikufanya vizuri sana kama The Da Vinci Code.

Kitabu hiki kilichompatia umaarufu Dan Brow ni sehemu ya pili ya kitabu chake cha Fiction kuhusu Robert Langdon ambacho sehemu ya kwanza iliitwa Angels & Demon kama nilivyoeleza na vyote hivi viwili vilimuhusu huyu huyu character anayeitwa Robert Langdon. Ingawa baada ya kitabu cha The Da Vinci Code kutoka na kujipatia umaarufu kupindukia Dan Brown mwenyewe alisisitiza kuwa kitabu chake ni fiction lakini Facts ni za kweli. Hasa hasa alisistiza kuwa kuna sehemu kubwa ya historia ya agano jipya imekuwa edited hasa hasa kuhusu ndoa ya Yesu na Mary Magdalena.

(Mary Magdalena ni yuke mwanamke aliyelia miguuni kwa Yesu na akamlowanisha miguu kwa machozi kisha akatumia nywele zake kufuta miguu. Kuna nadharia kuwa uhusianobwa kimapenzi ulianzia pale, wakafunga ndoa na kuwa a watoto. Kuna madai kuwa kizazi chao kipo mpaka leo hii. Wanaoamini nadharia hii wanadai kanisa liliachwa chini ya Mary Magdalena, lakini Petro akatumia mabavu kuhodhi kanisa na akahakikisha historia hii ya ndoa ya Yesu na Mary Magdakena inafichwa)

KUHUSU UMAARUFU WA MCHORO WA MONA LISA

Mchoro huu ulianza kujipatia umaarufu hasa hasa karne ya 19 zaidi ya miaka 300 baada ya kifo cha Leonardo. Sababu kubwa ya kwanza ya kujipatia umaarufu wake ilikuwa ni kwamba mchoro huu umechorwa na Leonardo Da Vinci.

Kumbuka kuwa Leonardo anahesabika kama moja wa binadamu wenye akili zaidi kuwahi kuishi. Yupo katika daraja moja na akina Issac Newton, Albert Einstein, Galileo, Socrates n.k.

Leonardo hakuwa mchoraji tu bali pia alikuwa mchongaji/mfinyanzi, Mwanahisabati, Mwanasayansi, Muhandisi, Mnajimu, mwanamuziki, Daktari, Mbunifu wa majengo n.k. n.k. n.k.

Moja ya kazi zake muhimu zilizoleta mchango mkubwa ukiacha uchoraji ni kwamba yeye ndiye binadamu wa kwanza kugundua nadharia na hesabu za kisayansi kufanya kitu kipae angani (Helikopta/Parashuti), pia ndiye binadamu wa kwanza kuanzisha nadharia ya kutengeneza vifaru. Pia anamchango mkubwa sana katika baiolojia (hasa hasa tawi la Anatomy).

Pili, kilichoupatia umaarufu mkubwa mchoro huu katika karne ya 20 ni tukio la kuibiwa kwake mwaka 1911. Habari hii ilikuwa gumzo ulimwengu mzima. Iliandikwa kila siku kwenye magazeti na upepelezi wake ulikuwa na wa gumzo vile vile.

Baada ya kupatikana tena mchoro huu na kurudishwa kwenye makumbusho ya Louvre nchini ufaransa. Rais wa Marekani J.F Kennedy aliuomba mchoro utembelee nchini kwake mwaka 1963.

Mchoro huu ukitembelea miji ya New York na Washington na watu walipanga mistari mirefu ya foleni na ilikuwa ikifika zamu yako unapewa sekunde 20 tu kuutazama. Inakadiriwa takribani wakazi Milioni 1.4 wa miji ya New York walijitokeza kuutazama kati ya Desemba 1962 na Machi 1963.
Baada ya hapo serikali za Japan na Russia nazo zikaomba kutembelewa na mchoro huu.

Jambo la mwisho linaloupa umaarufu huu mchoro ni utata na mabishano.
Mfano kuna utata mkubwa ile ni Picha ya nani, kuna utata kuhusu ile 'background' ni wapi, kuna utata kuhusu facial expression, kuna utata kwanini copy za zamani za mchoro huo zote zinaonyesha nyuma kwenye background kuna nguzo lakini mchoro huu wa sasa hauna nguzo, kuna utata kwanini huyo aliyechorwa hana nyusi wala kope, kuna utata kuhusu mikono ilivyowekwa kwenye picha kwasababu hana pete ya ndoa na ilhali uchunguzi wa kina wa nywele zake unaonyesha zimebanwa kwa nyuma hii ikimaanisha alikuwa ameolewa wa tamaduni za kipindi hicho, n.k. n.k. n.k.

Utata na mabishano kuhusu mchoro wa Mona Lisa hautaisha leo, kesho wala baada ya miaka 20.

Mwisho..

Kuhusu Ujumbe wa siri unaodaiwa kufichwa kwenye mchoro huu ni kwamba kwa taarifa rasmi na ambazo zimethibitishwa ni kwamba. Katika jicho la kulia eneo la retina kwenye mchoro wa Mona Lisa kuna Herufi zilizofichwa kwa ustadi mkubwa na Leonardo ambazo huwezi kuziona kwa macho kawaida. Herufi hizo ni 'LV' ambazo watu wametafsiri kana 'signature' ya Leonardo Da Vinci.
Kwenye jicho la kushoto kuna herufi pia zimefichwa na hazionekani sawa sawa kutokana na mchoro kuwa wa muda mrefu lakini zinaonekana kama ni herufi 'B' au 'C3'. Mpaka sasa hakuna anayejua maana yake.

Pia nyuma kwenye background karibu na daraja kuna herufi pia zimefichwa ambazo nazo pia hazionekani sawia, herufi hizo ni namba '72' au 'L2'. Na hizi pia hakuna anayejua maana yake.

Mchoro huu kipindi unaombwa ukatembelee nchi mbali mbali kwa maonyesho ulikatiwa bima ya Dola Millioni 100 kwa kipindi hicho. Kiwango hicho kwa fedha kinaufanya mchoro huu kuwa na thamani ya Dola Milioni 782 kwa sasa.

Limewahi kutolewa pendekezo kuwa mchoro huu uuzwe ili kuwaidia kulipa deni la serikali la Ufaransa lakini wazo hili lilipingwa vikali na serikali ikatunga sheria maalumu ya kuzuia kuuza mchoro wa Mona lisa na michoro mingine ya kihistoria ya nchi hiyo.

Kwasasa mchoro wa Mona Lisa unahifadhiwa kwenye Jumba la Makumbusho la Louvre, jijini Paris nchini Ufaransa.



Jiunge na Group langu la WhatsApp kusoma simulizi mpya kila siku. Kuna malipo ya 5,000/- kwa mwezi. Wasiliana nami 0759 181 457



The Bold.
 
Back
Top Bottom