Hiv ni kweli siku ya ufufuo ipo au ni tricky tu ya kutufariji pindi tunapofiwa na ndugu na jamaa ili tuamini ipo siku tutaonana nao paradiso na kama kweli ipo? Maana watu wamefariki miaka zaidi ya Ma elfu iliyopita ila hatujawahi kusikia habari za ufufuo wao au inakuaje? Maana kila siku watu wanazidi kuzaliana na kufa.
''Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.”
Ufu. 22:12. “Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko,…
nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza… na hivyo tutakuwa na Bwana milele.”
1 Thes. 4:16,17. “Sote tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua,… na wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu… Maana sharti huu uharibikao uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa uvae kutokufa. Basi huu uharibikao utakapovaa kutokuharibika…”
1 Kor. 15:51-53.
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti hitakuwapo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita.”
Ufu. 21:4. “Huo ndio ufufuo wa kwanza. Heri, na mtakatifu, ni yeye aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu.”
Ufu. 20:6
Kwenye huu ufufuo unaoongelewa kwenye hayo mafungu ya biblia ni wale tu waliokufa wakiwa ndani ya Yesu.