Analogia Malenga
Platinum Member
- Feb 24, 2012
- 5,286
- 10,833
Kumeibuka utata kufuatia taarifa za mwanamke mmoja, mama wa watoto wa wawili, kudaiwa kujinyonga katika mahabusu ya polisi jiji jijini Dar es Saalm, huku ndugu wa marehemu wakitilia shaka taarifa hiyo ya polisi.
Wakati Jeshi la Polisi likidai Stella Moses (30) amejinyonga akiwa kituo cha polisi Mburahati jijini Dar es Saalm, nduguze wametaka ufanyike uchunguzi na hawatachukua mwili hadi ukweli ufahamike.
Kamanda wa Polisi Wilaya ya Kinondoni, Ramadhan Kingai aliliambia gazeti hili kuwa mwanamke huyo alijinyonga na polisi wa kituo cha Mburahati waliupeleka mwili huo na kwenda kuuhifadhi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Kwa mujibu wa Kingai tukio hilo lilitokea Jumatatu Desemba 21 lakini ndugu wa mwanamke huyo wameliambia gazeti hili kwamba Stella alifariki Jumapili Desemba 20 jioni, siku ambayo alijisalimisha kituoni hapo baada ya kupata taarifa kwamba anatafutwa.
Walisema walipompelekea mtuhumiwa huyo chai Jumatatu saa 2 asubuhi, waliambiwa na polisi kuwa wamechelewa na hivyo wakatakiwa kurudi saa tano.
Walipokwenda tena muda walioahidiwa waliambiwa waende ndugu yao akijaribu kujinyonga na amepelekwa Muhimbili, hivyo wamfuate huko.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia, walipofika Muhimbili walielezwa kuwa ndugu yao alifikishwa akiwa amwikwishafariki dunia na mwili wake ulipelekwa na polisi saa 5:27 usiku.
Kutokana na utata wa mazingira ya kifo hicho, ndugu hao wamewenda kuonana na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kupeleka malalamiko yao kufikisha malalamiko na kudai uchunguzi wa kifo hicho.
Mambosasa alilieleza gazeti hili kuwa baada ya kupokea malalamiko hayo, atafungua jalada la uchunguzi kubaini ukweli juu ya tukio hilo.
“Mimi kazi yangu ni kuchunguza, nimepokea malalamiko yao leo (jana) na hatua inayofuata ni kufungua jalada kwa ajili ya kuchunguza,” alisema Mambosasa.
Kwa upande wake Kingai alisema Stella alijinyonga kwa kutumia nguo aliyokuwa amevaa,” inaonekana alikuwa na madeni mengi ndiyo maana amejinyonga. Tumechunguza tukio hilo haikuwa uzembe wa askari wetu kwani wakati anaingia mahabusu taratibu zote zilifanyika ikiwemo kupekuliwa.”
Soma zaidi gazeti la Mwananchi Desemba 23, 2020