Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Aisehh nchi imekuwa ya kamata kamata !! Haya mambo niliyasikia mataifa mengine mengine nikawa nawadharau kumbe eh ni rahisi rahisi tu hata sisi yametukuta.

Wakimaliza na wenye mawazo tofauti watarudi humo humo.
Sioni mpya. Msitu wa mabwepande ulisika kwa utakaji vipindi si virefu vilivyopita. Dr. Ulimboka kutekwa na kung'olewa kucha na macho, JPM hakuwa raisi. Dr. Mvungi kuuawa kikatili nyumbani kwake, JPM hakuwa raisi. Mkemia mkuu wa serikali kupotezwa maisha miaka ya mwanzoni mwa 90 JPM hakuwa hata ni mbunge. Kamanda kombe kuuawa kinyama JPM hakuwa hata mbunge. So mi ioni jambo jipya, hadi mnamsema JPM ambaye hata hatujasikia aliyepotezwa uhai wake.
Acheni kumuonea JPM. eti hatujaona viwanda, waulize Nchi zilizoendelea kiviwanda leo walichukua muda gani kufika hapa tangu walipopata wazo la kujenga uchumi wa viwanda. mapinduzi ya viwanda hata hayakuwa ya mwaka mmoja, ni karne nyingi zilipita kabla hawajafikia mapinduzi ya viwanda. Angalau JPM analo hata wazo la kuwa na viwanda kuliko viongozi wengine wanawaza kuuza mihadarati na viroba watanzania waangamie.
 
MAZOMBIE YA KISONGE YAMEHAMIA BARA
TULIZOEA HAYA MAMBO KUFANYIWA CUF..TUKACHEKA TUKASEMA HAYATUHUSU HAUO YA WAPEMBA , TULISAHAU MAZOMBIE HAYA NI KAMA NYOKA ALIKUWEPO NA BADO WAPO ZANZIBAR KWA SABABU WAMEKATALIWA.
SASA WAMEANZA BARA KWANI WAMEANZA KUKATALIWA
ZANZIBAR WASHAZOEA HAYA
KUVAMIWA RADIO HUKO ZNZ NI MAMBO YA KAWAIDA NA KUZICHOMA MOTO RADIO...SASA NYOKA KATAMBAA YUPO TANGANYIKA
 
Sioni mpya. Msitu wa mabwepande ulisika kwa utakaji vipindi si virefu vilivyopita. Dr. Ulimboka kutekwa na kung'olewa kucha na macho, JPM hakuwa raisi. Dr. Mvungi kuuawa kikatili nyumbani kwake, JPM hakuwa raisi. Mkemia mkuu wa serikali kupotezwa maisha miaka ya mwanzoni mwa 90 JPM hakuwa hata ni mbunge. Kamanda kombe kuuawa kinyama JPM hakuwa hata mbunge. So mi ioni jambo jipya, hadi mnamsema JPM ambaye hata hatujasikia aliyepotezwa uhai wake.
Acheni kumuonea JPM. eti hatujaona viwanda, waulize Nchi zilizoendelea kiviwanda leo walichukua muda gani kufika hapa tangu walipopata wazo la kujenga uchumi wa viwanda. mapinduzi ya viwanda hata hayakuwa ya mwaka mmoja, ni karne nyingi zilipita kabla hawajafikia mapinduzi ya viwanda. Angalau JPM analo hata wazo la kuwa na viwanda kuliko viongozi wengine wanawaza kuuza mihadarati na viroba watanzania waangamie.
Kwa hiyo huyu mkulu tumuache atawale kwa kuvunja sheria kisa vijiwonder?
 
Kuna mambo hayajakaa sawa ktk hii habari:
  1. Roma hajatoa wimbo wowote wenye kukashfu serikali au viongozi wake hivi karibuni. Nyimbo zilizopo ni za wakati wa Kikwete na hakuchukuliwa hatua zozote.
  2. Waliomkamata wameenda na Noah nyeusi. Polisi hawana magari dizain ya Noah. Watu waliokuwa hapo walipaswa kuwatilia shaka kama kweli hao ni polisi.
  3. Polisi wamechukua kompyuta na TV. Hapo ndipo penye utata zaidi. Kwanin polisi wachukue TV? Kwa ajili ya upelelezi, polisi hahitaji hata monitor (screen) ya PC. Anahitaji System Unit tu. Hili jambo lilipaswa liwashtue wanaokamatwa na kuwahoji askari vitambulisho vyao na kituo wanachotaka kuwapeleka. Pia watu waliokuwa karibu wangeweza kustuka kutokana na hili.
Kwa maoni yangu, suala la kukamatwa kwa Roma halijakaa kipolisi kabisa. Inawezekana ni vyombo vingine vya dola au ni kiki inatengenezwa. Hoja ya kiki hata mimi sijapenda kuiibua, lakini kama Ney kasamehewa ambaye wimbo wake uliilenga serikali moja kwa moja, kwanini serikali itake kushughulika na Roma? Kama management ya Roma inatengeneza kiki, basi wanafanya makosa makubwa sana maana kuna watu kama Ben Saanane ambaye hajulikani aliko na pia Ulimboka ambaye alipotezwa halafu akapatikana akiwa na hali mbaya sana. Hatutakiwi kujenga dhana kwamba 'kupotea na kutopatikana hata ktk vyombo vya dola ni kawaida'.
 
sooth kiki inajulikana tu sema hii ya roma imejaa maswali mengi sana
inawezekana hata maadui wake wa zamani wametake advantage due to current situation in tz
 
baada ya kuona inshu ya bashite na vyeti inafifia, chadema wanapika tukio jingine jipya la kupotea kwa roma ...utafikiria roma ni mtoto mdogo.
 
Mkuu,

Hapo kwenye "bold", tuwaachie mpaka lini?

Kaka ...
Tukio lolote la kiusalama kwa mwanainchi likitokea kuna mamlaka husika za kutoa taarifa kwa utaratibu wa Serikali.

Sasa ukiniuliza mpaka lini hilo Mimi sio msemaji wao.

Lakini hujazuiwa kupiga kelele
 
kweli kabisa, kama juhudi iliyopo ya kumtafuta Ben Saanane.
Ben saanane siwezi kulisemea sana maana hata huyo boss wake anatuchanga kama wanainchi kwa taarifa alizozitoa za awali kuhusu kuwa huyo bwana amepotea.

Hizi syndicate za siasa za nchi masikini ni tabu sana.
 
Naona issue ya Roma macho yote ni Serikali tu wakati hakuna mwenye chembe ya ushahidi hata mmoja ktk comments zote.

Kwanza kilichowafanya Roma na kundi lake kutii amri za kupanda Noah nyeusi toka kwa watu waliovaa kiraia na kubeba vifaa vyenu vya kazi nini??

Hawakutakiwa kutii amri toka kwa raia usiowajua kupakia vifaa na kuondoka nao gari za kiraia kama umechukiliwa na Serikali kweli!!

Walikuwa zaidi ya watu 4 studio walikuwa na uwezo wa kupiga kelele kuwa wamevamiwa na kila mmoja kukimbia upande tofauti kwa Mara moja na naimani hiyo gari isingeondoka hapo.

Watu wange iblock tu,sasa wote sijui wa 4 sijui 5 mnakubali tu kirahisi kubeba vifaa kweli kirahisi tu kienyeji tu hivyo.

Mimi haiingii akilini sana Hapa kuna michezo tu ya kihuni inaendelea kwa kuchezea akili za watu. Ili tuamini kuwa Serikali unafanya harassment kwa watu wake.Hii syndicate haitakubalika.

Kazi ya msingi Serikali ni kulinda RAIA wake na si kuangamiza raia wake.
 
Back
Top Bottom