Utata: Msanii Roma Mkatoliki na wenzake wakamatwa/tekwa nyara

Habari wakuu nimekuta bandiko katika ukurasa wa Prof. Jay kuhusu kukamatwa kwa msanii ROMA na kuchukuliwa kwa baadhi ya vitu vya studio ya Tongwe record sijui ni kiki au kweli? Mwenye kujua kinachoendelea

=======

View attachment 491832
Baada ya kuzagaa kwa taarifa kuhusu kukamatwa kwa Msanii Roma Mkatoliki akiwa studio na kupelekwa kusiko julikana, Muungwana Blog imefika katika studio za Tongwe Records jijini Dar es salaam ambapo mkasa mzima ulikuwa hivi...

Kwa mujibu wa Mashuhuda (Majina yanahifadhiwa) walio ambao pia wanaishi katika nyumba ambayo inapatikana studio ya Tongwe, wameijuza Muungwana kuwa April 5, 2017 ambayo ilikuwa ni jana, katika majira ya Saa moja jioni ilionekana gari aina ya Noah nyeusi nje ya studio hizo, ambapo walishuka watu zaidi ya Watano na kuingia ndani ya studio hizo.

Watu hao bila ya kujitambulisha walitamka kuwa wanamuhitaji Roma na mwenzake ambapo walimchukua na kutoka nae nje, na baada ya muda kidogo walirejea ndani na kuwachukua wengine watano akiwemo na Prodyuza wa studio hiyo Anayeitwa Moni.

Mbali na kuwachukua watu hao pia mashuhuda hao wemeeleza baadhi ya vifaa vya studio hiyo pia vimebebwa ikiwemo TV, na Computer.

Kwa Mujibu wa Mwanasheria wa Studio hiyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Edin ameiambia Muungwana Blog kuwa nikweli tukio hilo limetokea na mpaka sasa hawajui Roma na wenzake wamepelekwa wapi na hivyo hawezi kuelezea zaidi mpaka atakapojua walipo wakina Roma, ambapo aliongeza kuwa anakwenda kuripoti katika kituo cha polisi cha Oysterbay Jijini humo.

Chanzo: Blogs
Wasanii, uzeni rekodi nzuri mujulikane badala ya kutegemea vituko kama sehemu ya kujitangaza.
Imekuwa ni uchafu tuuuu!
 
Sasa mnasema tu kakamatwa kosa alofanya ni lipi? na sidhani kama ni rahisi tena kukamata Msanii baada ya lile tukio la Nay...pia kama Polisi wana shida naye nadhani wangemuita kuliko kufanya tukio litakalovuta attention za Watu.

Ukute tu ana tofauti na wenzake nyie mbakie ametekwa na Polisi.
 
Wameenda polisi kutoa taarifa,kwa akili yako mtu hawezi kwenda polisi kama anatafuta kiki.
Swala ni haijulikani waliomchukua na ingefahamika tungejua aliko kama ilivyokua kwa Nay istoshe haieleweki sababu ya kuchukuliwa
 
Back
Top Bottom