Utata kwenye muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata kwenye muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gamba la Nyoka, Dec 23, 2011.

 1. Gamba la Nyoka

  Gamba la Nyoka JF-Expert Member

  #1
  Dec 23, 2011
  Joined: May 1, 2007
  Messages: 6,595
  Likes Received: 6,757
  Trophy Points: 280
  (1)Ni dhahiri kuna mambo ya muungano na yasiyo ya muungano, je Pindi Mzanzibari atakapokuwa raisi wa Tanzania nzima, ana uhalali gani wa kuiwakilisha/kutoa maamuzi juu ya mambo yasiyo ya Muungano yanayoihusu Tanganyika?

  (2)Maadamu mipaka ya Tanganyika haijawekwa wazi kikatiba, je Raisi wa Tanzania mwenye ajenda ya Uzanzibari ndani yake akiamua kuunda Mkoa mpya wa Tanzania(kwa kushauriana na Raisi wa Zanzibar ofcourse) kwa kuchukua ardhi ya kale ya Tanganyika let say Tanga akaunganisha na Unguja na kuuweka mkoa huu chini ya mamlaka ya serikali ya Zanzibar itakuwaje?.

  (3) Ni nini haswa Mtanganyika ananufaika nacho katika Muungano wa style yetu?, tunaona Mzanzibar anaweza kununua ardhi kwa wepesi kabisa mahali popote rasmi ndani ya Tanganyika, anaweza kuomba kupiga na kupigiwa kura ya Uraisi, udiwani, ubunge bila Sharti la Muda maalumu wa Kukaa Tanganyika, Swali ni je Mtanganyika ananufaika na nini kutoka Zanzibar?
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  mmmhh! anyaway,,siku zote natilia mashaka sana sababu zilizopelekea kuungana/muungano.shaka yangu huongezeka kila mara inapojidhihirisha viongozi wa ccm wanapoonekana wazi kutotaka/ruhusu majadiliano juu ya muungano wenyewe na muundo wake wala marekebisho!
   
 3. Nsabhi

  Nsabhi JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2011
  Messages: 1,096
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Huu Muungano haufai kabisa na kwa bahati mbaya kwenye mchakato wa uundwaji wa katiba mpya hawaruhusu kuhoji uhalali wa Muungano. Hii ni fitina ilifanywa na serikali ya Magamba kwa kushirikiana na nyumba ndogo yao (CUF). Lakini wazalendo wa Tanganyika tusirudi nyuma
   
Loading...