Noncommited
JF-Expert Member
- Jun 22, 2012
- 1,125
- 369
Habarini Ndugu zangu wana Jamvi
Leo ningeomba tujadili kwa pamoja kwenye hili jambo la bishara ya vileo.
Kwa kuzingatia muongozo uliotolewa na Mh.Rais wa kuhusiana na kukamatwa kwa watu wanaouza pombe asubuhi na wateja wao.
Moja ningependa kufahamu uuzaji wa vileo ni biashara au burudani?
Ikiwa Vilabu vyote vya pombe wanalipia leseni ya biashara, wanalipa kodi TRA na wanaendesha maisha kwa kusomesha watoto shule kupitia hii shughuli ya uuzaji wa pombe. Kama ni biashara na inaingiza kodi serikalini kwa kwanini wapangiwe muda wa kufanya biashara yao.
Na kama ni burudani basi wasiilipe kodi na tozo nyinginezo.
Pili ningependa kufahamu hivi muda wa kazi ni saa Moja asubuhi mpaka saa tisa tu? Kuanzia hapo si muda wa kazi tena mtu akifanya kazi ni kiherehere chake tu?
Muda uliopangwa umewalenga wafanyakazi wa umma na binafsi wanaofanya kazi kwa mujibu wa sheria ya mikataba yao unatumika hadi kuwaongoza wasio watumishi wa umma?
Siku za mapumziko kiserikali Jumamosi na Jumapili inakuwa ruksa kuuza kuanzia asubuhi, ina maana wananchi wote ambao hatulipwi mishahara na serikali nasi tunatakiwa kupumzika siku hizo?
USHAURI KWA SERIKALI
Kwa nchi zilizoendelea hawana muda maalumu wa kufanya kazi kama ilivyo kwetu Tanzania, mtu anafanya kazi ndani ya muda wote wa masaa 24. Watu wanafanya kazi usikuna mchana.
Serikali inatakiwa itambue uuzaji wa vileo ni biashara na shughuli za kiuchumi kama zilivyo shughuli nyingine. Kitendo cha kuwapangia muda wa kufanya kazi ni kuwanyima fursa za kujiinua kiuchumi na kuikosesha serikali mapato. Kwani kadri mnywaji anavyokunywa ndipo serikali inavyoingiza mapato.
Kupitia hayo maagizo yameleta shida na ugumu wa maisha mtaani. Askari polisi wamekuwa wakikamata wananchi hovyo nyakati za usiku wanapopita kufunga mabaa ifikapo saa tano usiku na grocery ifikapo saa 3 usiku.
Ifikia mahali serikali inayojinasibu kwa HAPA KAZI TU itafsiri kwa vitendo kuwaachia wananchi Uhuru wa kufanya kazi kwa muda wote ili kuinua uchumina sio kuminya muda wa kufanya kazi. Madereva pikipiki wanakatazwa kufanya kazi ifikapo sa 5 usiku na ukikutwa unakamatwa na polisi.
Serikali inatakiwa itambue waliokuwa kwenye ajira rasmi ya serikalini na sekta binafsi ambao wanafanya kazi kuanzia saa moja asubuhi hadi saa tisa hawafiki hata milioni 10 kati ya watu milioni 40 ya watanzania.
MENGINEYO
Pia serikali itambue kwa maisha ya sasa, fursa zinajionyesha wazi wala haihitaji kulazimishwa na serikali. Mfano kitendo cha kutaka kuwalazimisha vijana wakalime na sio kukaa mjini si sahihi. Serikali tengeneza mazingira mazuri kwenye kilimo vijana wa mjini watakimbilia wenyewe bila hata kusukumwa. Mbona migodini wanakwenda wenyewe inapotokea madini yanapatikana.
Kilimo cha Tanzania kingekuwa kinatoa watu wasingekimbilia kwenye siasa na ajira za serikali wangekomaa mashambani.
Mnaohimiza suala la vijana kuondoka mjini nakwenda kulima ni bora mngeonyesha kwa mifano kwa kuachia nyadhifa zenu na kwenda kulima ili muweze kueleweka vizuri.