Utata katika mtazamo...

entry

JF-Expert Member
Apr 11, 2018
248
464
Katika jamii yetu ni kawaida kusikia mwanaume akisema sifungi ndoa mpaka nimiliki kitu flani mfano nyumba au gari n.k. mtazamo wa mwanaume huyu katika jamii asilimia kubwa watakubaliana naye.

Sasa tuje upande wa mwanamke mwenye mtazamo kwamba siolewi ila na mwanaume anaemiliki kitu flani, jamii humuona mwanamke huyu kama hafai kuwa wife material.

Sasa naishia kujiuliza swali kwanini mapokezi ya mtazamo mmoja yamekuwa tofauti katika hizi jinsia mbili?
 
Hizi thread za kuumiza kichwa muda huu ambao k vant nimekaimisha maamuzi zinachosha saaana
 
Ni kwasababu tuu mwanaume ameandikiwa kutafuta kwa jasho,na mwaamke kaandikiwa kuzaa kwa uchungu....full stop
 
Kawaida mwanaume ni mtafutaji cku zote, akiwa na mtazamo huo ni sawa japo cyo lazima air akiwa na nyumba na gari,
 
Back
Top Bottom